- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Kuongezeka kwa Uhasama nchini Sudan
(Imetafsiriwa)
Swali:
Al Arabiya Net ilichapisha kwenye tovuti yake mnamo tarehe 4/2/2025: "Jeshi na vikosi vyake vya usaidizi viliingia katika maeneo ya kusini-mashariki ya Jimbo la Khartoum wakati wa saa zilizopita, wakitokea Jimbo la Al-Jazeera.." na tovuti ya Youm7 ilichapishwa mnamo tarehe 2/2/2025: "Mwandishi wa Kituo cha Habari cha Cairo aliripoti katika habari mpya zinazochipuka kwamba jeshi la Sudan linachukua idadi kadhaa ya vijiji mashariki mwa mto Nile katika Jimbo la Khartoum." Kabla ya hapo, mnamo tarehe 11/ 1/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka vilishindwa na jeshi la Sudan katika mhimili wa Jimbo la Al-Jazeera na mji mkuu wake, Wad Madani, “na kamanda wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, Hemeti, alikiri katika kanda ya sauti iliyohusishwa naye kwamba vikosi vyake vilishindwa katika Jimbo la Al-Jazeera...” (Al-Jazeera 1/13/2025). Kisha mwelekeo wa vita vyote katika miji mikuu mitatu (Khartoum, Bahri na Omdurman) ukageuka na kupendelea jeshi la Sudan, kwa hiyo likachukua udhibiti wa maeneo kadhaa muhimu katika miji hii na kuondoa mzingiro wa Kamandi Kuu. Je, vitendo hivi vyote vya ndani vinatokana na kuibuka kwa ghafla kwa kikosi cha upande mmoja, jeshi la Sudan, au vita hivi vina vipimo vya kimataifa katika mzozo wa Sudan?
Jibu:
Ili kufafanua majibu ya maswali hayo juu, tutahakiki mambo yafuatayo:
Kwanza: Kuharakishwa kwa operesheni za kijeshi nchini Sudan:
1- Ndio, ni kweli kwamba kasi ya uhasama nchini Sudan inashangaza.
Baada ya kuzuka kwa vita kati ya pande mbili zilizokuwa madarakani nchini Sudan tangu Aprili 2023, vita vilikuwa vikifanyika kwa mduara wa siri katika suala la udhibiti wa ardhi, huku kila upande ukiendelea kushikilia nyadhifa zake, na maendeleo ya upande mmoja kuelekea mwingine katika miezi iliyopita yalikuwa kidogo. "Na katika mwaka mzima wa vita vilivyoanza Aprili 15, jeshi halikupata maendeleo yoyote makubwa isipokuwa kuregeshwa kwa makao makuu ya Redio ya Kitaifa na Televisheni na maeneo mengine huko Omdurman, mnamo Machi 2024, na kudumisha mbinu ya kujihami ili kuhifadhi makao makuu ya jeshi." (Tovuti ya Al-Rakoba ya Sudan, 1/25/2025).
2- Lakini hali uwanjani imekuwa ikibadilika tangu Septemba 2024, wakati jeshi la Sudan lilipoanza kukusanya safu zake, kukunja mikono yake ya shati, na kuvunja kile ilichokiita "uvumilivu wa kimkakati" na "pumzi ndefu." Lilianza kufungua mipaka dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka, kwa hivyo likachukua udhibiti wa Daraja la Halfaya na Nile Nyeupe na kufungua barabara kuelekea katikati mwa mji mkuu wa Khartoum Bahri. Kisha, matukio ya uwanjani yalichukua mkondo wa haraka zaidi chini ya mwezi mmoja uliopita, wakati jeshi lilipochukua udhibiti wa mji wa Wad Madani mnamo 11/1/2025, mwaka mmoja baada ya kupoteza udhibiti wake kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Ni mji mkuu wa Jimbo la Al-Jazeera, ambalo liko katikati mwa Sudan. Hili lilionekana kuwa vita muhimu katika mzozo kati ya pande hizo mbili, kwa kuwa mji huu ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan, na kwa suala la eneo lake katika majimbo ya Sudan na uwezo wa upande unaoudhibiti kusambaza vikosi vyake katika majimbo mengine, haswa eneo la mji mkuu. Udhibiti huu wa jeshi la Wad Madani ulikuwa mshtuko mkubwa kwa harakati zao. Kwa kupotea kwake, uwezo wa Vikosi vya Msaada wa Haraka wa kusambaza vikosi vyake katika eneo la Khartoum unadhoofika, na kutoka upande mwingine, Vikosi vya Msaada wa Haraka vilipoteza mahali pa kuanzia ambapo vilikuwa vikipatumia kuunganisha maeneo mengine ya Al-Jazeera, Sennar, Nile Nyeupe na mashariki mwa Sudan, na hivyo ndoto na matumaini yake yalififia. (Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito na Kamanda wa Jeshi, Luteni Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, alidokeza wakati wa ziara yake katika mji wa Wad Madani baada ya kukombolewa, mipango inayoendelea ya kuanzisha shambulizi kubwa la kijeshi dhidi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka vilivyobaki ndani ya mji mkuu, Khartoum, na viunga vya miji mingine. (Independent Arabia, 20/01/2025).
Pili: Baada ya kuudhibiti Wad Madani, jeshi lilianza kushambulia kwa nguvu ndani ya eneo la mji mkuu:
1- Jeshi la Sudan lilitangaza kuwa limedhibiti tena Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Khartoum, kilichoko kaskazini mwa Khartoum Bahri, baada ya mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na Vikosi vya Msaada wa Haraka. (BBC, 25/01/2025)
2-Mwandishi wa Al Arabiya ameripoti leo, Ijumaa, kwamba jeshi la Sudan limeondoa mzingiro ambao Vikosi vya Msaada wa Haraka vilikuwa vimeweka kwa Kamandi Kuu ya Jeshi huko Khartoum kwa mwaka mmoja na nusu. Ripoti za ndani za Sudan pia zilisema kwamba vikosi vya jeshi pia viliondoa mzingiro wa kambi ya Signal Corps, baada ya mapigano katikati mwa Khartoum Bahri. (Al Arabiya, 24/01/2025)
3- Jeshi lilipata mafanikio makubwa zaidi ya kijeshi katika mji mkuu, Khartoum, baada yake na vikosi vya washirika kuweza kuondoa mzingiro kwenye makao makuu yake mawili, ya kwanza ikiwa ni makao makuu ya makamanda wake katikati mwa Khartoum na ya pili ikiwa ni makao makuu ya Signal Corps, na kuunganisha makao makuu hayo mawili na makao makuu ya kamandi yake ya kijeshi katika eneo la kijeshi la Wadi Saydna, kaskazini mwa Omdurman. Pia lilipata udhibiti wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Jelei na maeneo yanayozunguka makaazi na jeshi. (Tovuti ya Al-Rakoba ya Sudan, 25/01/2025)
4- Al Arabiya Net ilichapishwa kwenye tovuti yake mnamo tarehe 4/2/2025: "Jeshi na vikosi vyake vya usaidizi viliingia katika maeneo ya kusini-mashariki ya Jimbo la Khartoum katika saa zilizopita, wakitokea Jimbo la Al-Jazeera."
5- Tovuti ya Al-Youm Al-Sabea ilichapishwa mnamo tarehe 2/2/2025: "Mwandishi wa Chaneli ya Habari ya Cairo aliripoti katika habari za hivi punde kwamba jeshi la Sudan linaregesha udhibiti wa idadi ya vijiji mashariki mwa Mto Nile katika Jimbo la Khartoum."
Tatu: Kwa hivyo, jeshi la Sudan lilianzisha vita vikubwa ili kuvifukuza Vikosi vya Msaada wa Haraka kutoka katika miji mikuu mitatu, na kuirudisha kwenye udhibiti wa jeshi, ambayo ni nembo ya serikali ya Sudan, huku Burhan akikataa kufanya mazungumzo na waasi. Kwa kutafakari vitendo hivi, tunapata yafuatayo:
1- Jeshi la Sudan linahitimisha sera ya "uvumilivu wa kimkakati" na "pumzi ndefu", na linafanya hivyo bila usawa mkubwa katika mizani ya kijeshi kati ya pande mbili, ikimaanisha kuwa liliibuka kutatua suala hilo na liliweza kufanya hivyo tangu kuzuka kwa vita mnamo Aprili 2023, lakini halikufanya hivyo, na hili halitokei bila sababu!
2- Ni kweli kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka vinapata hasara katika mji mkuu baada ya kupoteza mji wa Wad Madani, lakini vikosi vyake vinaondoka kwenye maeneo ya vita na kuelekea Darfur, ambavyo vinadhibiti miji yake mikuu minne kati ya mitano, kumaanisha kwamba halijileti lenyewe msaada katika eneo la mji mkuu kutoka maeneo ambayo nguvu yake imemakinika (Darfur), badala yake linajiondoa kwenye maeneo hayo. Kwa hakika, vita vimepamba moto tena huko Darfur, ambako RSF ina mkono wa juu, kana kwamba inaacha maeneo yake ya udhibiti kwa ajili ya kutawala ukumbi wa Darfur. Pia inaonekana kwamba jeshi, badala ya kulisukuma lijisalimishe, linafungua njia kwa ajili ya RSF kuelekea Darfur!
3- Kinachoashiria haya yote ni kile ambacho Independent Arabia iliripoti mnamo tarehe 20/1/2025, kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka vinatumia madaraja ya Manshiya na Soba mashariki mwa Nile ili kujiondoa katika maeneo wanayoyadhibiti huko Jebel Awliya, ambako huko barabara ndiyo karibu pekee iliyo wazi kwao kuelekea magharibi mwa Sudan, kufikia Darfur, na kwamba kujiondoa kwao ni pamoja na familia zao, wafanyikazi wa usalama na wale wanaoshirikiana nao. Ilisema: "Mkusanyiko wa hasara kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka katikati mwa Sudan unasukuma makundi makubwa yao kuondoka kila siku kuelekea Darfur kupitia njia ndogo na zinazojulikana, ambazo jeshi limewacha wazi kama sehemu ya mipango yake ya muda," na ilisema kwamba RSF inaendesha operesheni kubwa ya usajili huko Darfur: "Kwa hiyo, limeendelea kuwaandikisha vijana kutoka kwa makabila ya Kiarabu yaliyotiifu kwake ili kushinikiza viongozi wa makabila huko, ... na Vikosi vya Msaada wa Haraka vilifichua kwenye Telegram kwamba makabila kadhaa huko Kass na Wad al-Fursan kusini mwa Darfur yametangaza utiifu wao kamili kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka na wamesukuma wapiganaji 50,000 katika safu zake.”
Nne: Kwa hivyo, Darfur inatayarishwa kama ukumbi wa vita vijavyo, ambapo mkono wa juu unashikiliwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka, ambao wanachukulia kuwa kiota chake maarufu:
1-Taarifa ya msemaji rasmi wa RSF ilisema kuwa jana, Jumamosi, iliweza kuweka udhibiti wake kamili juu ya maeneo ya Al-Halaf - Drishqi - na Mao katika Jimbo la Darfur Kaskazini. (Independent Arabia, 20/01/2025.)
2- Pia mapigano makali yalizuka huko Al-Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka na Vikosi vya Pamoja vya Sudan, ikiwemo jeshi, makundi ya waasi, polisi na vitengo vya ndani vya ulinzi. (France 24, 25/01/2025).
3- Pia: Ama kuhusu mhimili wa Magharibi, na kufuatia maonyo yake na kuwapa jeshi na vikosi vya pamoja muda wa masaa 48 kuondoka katika mji wa Al-Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur, RSF ilianzisha mashambulizi ya pande nyingi katika mji huo. Makabiliano kati ya jeshi na vikosi vya pamoja yaliendelea kwa zaidi ya masaa sita baada ya mapambazuko ya Januari 24. (Independent Arabia, 25/01/2024)
4- Yote haya yanaonyesha kuwa kasi ya matukio uwanjani nchini Sudan yanaelekea upande mmoja, ambao ni jeshi kuregesha udhibiti wa maeneo mengi nchini Sudan na kuliacha eneo la magharibi, Darfur haswa, kwa RSF. Endapo mwelekeo huu utakamilika, nchi itaelekea kwenye mgawanyiko halisi. RSF ambayo inadhibiti maeneo makubwa ya Darfur (isipokuwa El Fasher), waliweza kusambaza vikosi vyao huko Al-Jazeera na eneo la mji mkuu, lakini walijiondoa kutoka maeneo hayo kuelekea Darfur licha ya fujo zote kutoka kwao. Hii inaashiria upande wa kimataifa ambao unapanga harakati za uwanjani kana kwamba unacheza mchezo wa chesi ambazo unazidhibiti nchini Sudan!
Tano: Ni wazi kwamba mabadiliko haya ya haraka uwanjani yanasadifiana na nyadhifa mpya mtawalia zilizotolewa na Washington:
1- Mnamo Januari 7, siku chache kabla ya kukabidhi madaraka kwa utawala mpya, utawala unaoondoka wa Biden ulituhumu Vikosi vya Msaada wa Haraka kwa kufanya "mauaji ya halaiki katika eneo la Darfur" magharibi mwa Sudan. Kulingana na tuhma hizo, uliweka vikwazo vya kifedha kwa viongozi wa RSF na makampuni saba yanayoaminika kufadhiliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu. Lakini siku chache tu baadaye, mnamo tarehe 16 mwezi huo huo, utawala huo huo wa Marekani ulimwekea vikwazo kamanda wa jeshi la Sudan na mtawala mkuu wa nchi hiyo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ukimtuhumu kwa "kuvuruga na kuzuia mabadiliko ya demokrasia nchini Sudan," na kwa hivyo kufungia mali yoyote ambayo Burhan anaimiliki nchini Marekani (BBC, 26/01/2025).
2- Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba mabadiliko katika jukwaa la Sudan ni majibu ya moja kwa moja na akisi ya mabadiliko nchini Marekani. Wakati Amerika ilipofungua faili ya Sudan na hii ilionekana kwa kuweka vikwazo kwa pande zote mbili, pande za vita nchini Sudan zilianza kujipanga upya kulingana na ramani mpya ya udhibiti. Amerika inafanya uhakiki usiotangazwa wa sera zake, na hatua ya kukabidhi utawala wa Biden kwa utawala mpya ndiyo iliyolazimu uhakiki huu. Inaonekana kuwa Rais mpya wa Marekani Trump anachukua mwelekeo mpya kwa utawala wake kutafuta suluhu kwa masuala motomoto ambayo yanaafiki maslahi ya Marekani na kuinua hadhi yake. Anaona kwamba ana Makubaliano ya Abraham ya kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, na anataka kuyapanua na anataka kujumuisha Sudan ndani yake. Kabla ya kuapishwa kwake, alichangia katika kufanikisha mpango wa Gaza, na anataka kuonekana kama mpenda amani kutoka kwenye nafasi yenye nguvu. Mtazamo huu mpya huko Washington unajumuisha Sudan na vita huko pia. Rais Trump anataka kuishinikiza Sudan kushiriki katika Mkataba wa Abraham kwa ajili ya kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani na mtafiti katika masuala ya Afrika, David Shinn, alitarajia kwamba utawala mpya wa Rais Donald Trump utashuhudia msukumo mkubwa zaidi wa juhudi, "hasa kwa vile Waziri mpya wa Mambo ya Nje Marco Rubio anavutiwa sana na faili ya Sudan," akieleza kuwa utawala wa kwanza wa Trump ulikuwa na hamu na Sudan na jitihada zilifanikiwa wakati huo katika kuhalalisha mahusiano kati ya Sudan na Israel ndani ya mfumo wa Mkataba wa Abraham. (Al-Hurra, 25/01/2025).
3- Haya yote pia yanathibitishwa na kile alichosema Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Ali Youssef: (Waziri alifichua kuwepo kwa ruwaza na programu ya kuhakiki sera ya Marekani nchini Sudan, ambayo itaanza baada ya utawala mpya kuchukua majukumu na mamlaka yake, na kuongeza, “Kuna wakati wa kuamiliana na utawala mpya wa Marekani.” (Gazeti la Al-Sharq, 23/01/2025). Gazeti la Akhbar Al-Sudan liliripoti mnamo 25/1/2025: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alikutana na mwenzake wa Misri Badr Abdel-Ati ndani ya muundo wa kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Marekani na Misri. Mawaziri hao wawili walijadili kuhusu maendeleo ya hali ya Sudan, ambapo walisisitiza haja ya kushinikiza pande zinazozozana kukomesha uhasama na kupanua wigo wa misaada ya kibinadamu.
Sita: Kutokana na hayo, kuna uwezekano mkubwa kwamba maendeleo uwanjani nchini Sudan yanapangwa na kusimamiwa na Trump na kwamba yanalenga kufikia yafuatayo:
1- Kuharakisha mpango wa Marekani wa kuandaa mazingira kwa kuigawanya nchi kati ya vibaraka wa Marekani kwa misingi ya Darfur chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (Rapid Support Forces) na utawala wa Hemeti, huku jeshi linaloongozwa na Burhan linadhibiti kati na mashariki mwa Sudan, kwa hivyo maumbo mawili yanaonekana nchini Sudan, na suala hili liliwekwa kwa nguvu ya udhibiti wa Hemeti juu ya Darfur. Hapo awali tumetaja mpango huu katika kujibu swali la tarehe 19/12/2023, ambapo tulieleza wakati huo "kwamba Amerika inatayarisha mazingira kwa ajili ya mgawanyiko ... pindi maslahi ya Amerika yatakapohitaji hivyo. Hata kama maslahi ya Amerika yanahitaji mgawanyiko mwingine baada ya Sudan Kusini, itafanya mgawanyiko huu huko Darfur ... na inaonekana kana kwamba wakati wa mgawanyiko huu bado haujafika kwa sasa... lakini kutayarisha mazingira kwa ajili yake ndiyo yanayoendelea kwa sasa.” Haya ndiyo tuliyoyasema hapo awali, na inaonekana kwamba hamu ya Marekani inakaribia kuharakisha utenganishaji wa Darfur kama ilivyokuwa Sudan Kusini... na hili ni hatari sana iwapo Trump atafanikiwa kulitekeleza... kwa hiyo Umma lazima usimame usoni mwake na usinyamaze kam ulivyo nyamaza wakati Sudan Kusini ilivyotenganishwa!
Kuisukuma Sudan na kuitayarisha kupanda gari moshi ya Trump ili kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, tulijibu hapo awali mnamo 19/03/2023, juu ya kuhalalisha mahusiano na Sudan, na ikasemwa kwamba kuhalalisha mahusiano [(kidini ni haramu kwa sababu ni utambuzi wa mnyakuzi wa Palestina, moja ya ardhi ya thamani zaidi kwa Waislamu, wanaoshambulia watu wake mchana na usiku, wanaovunja nyumba zao, wanauwa watoto wao, na kupora mali yao. Hata hivyo, Baraza la Utawala wa Sudan lilitangaza kwamba rais wake, Abdel Fattah Al-Burhan, alikutana na Cohen jijini Khartoum na kujadiliana kuhusu kuongeza matarajio ya ushirikiano wa pamoja, hasa katika nyanja za usalama na kijeshi), na Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan ilisema kwamba pande hizo mbili "zilikubaliana kusonga mbele katika kuhalalisha mahusiano kati ya pande hizo mbili." (Shirika la Habari la Sudan 2/2/2023)], na inaonekana kuwa Rais wa Marekani Trump anafanya udanganyifu ili kutekeleza hili bila kulifanya hatua kwa hatua kama mtangulizi wake Biden alivyofanya.
Saba: Yote haya yanaiweka wazi picha ya matukio ya Sudan na jinsi Washington ndiyo inayoyaendesha, ili watu wa Sudan na Waislamu kwa jumla watambue kwamba vita hivi, ambapo makumi ya maelfu waliuawa na zaidi ya Wasudan milioni 12 walilazimishwa kukimbia, na ambapo mfumo wa kilimo ulianguka katika nchi ambayo ilizingatiwa kuwa "kapu la chakula la dunia", na sekta muhimu za kiuchumi ziliporomoka, yote haya ni kutokana na vita vya kipuzi kati ya vibaraka. Burhan, Hemedti, na wale walio karibu nao wanaendesha vita hivi ili kutumikia maslahi ya Marekani na kuleta utulivu wa ushawishi wake nchini Sudan, na kuvirudisha nyuma vikosi vinavyoshirikiana na Wazungu, na hivi ndivyo ilivyotokea. Pande zote mbili hazikujali utakatifu wa damu ya Waislamu, na wafuasi wao walipaswa kuacha njia yao ya uhalifu, lakini uhamasishaji wa kila kundi dhidi ya jengine na udhalimu wa damu umepofusha macho ya pande zote mbili, kwa hivyo hawakuona ukali wa uharamu wa Uislamu wa kumwaga damu za Waislamu kwa mikono yao wenyewe: Imesemwa katika Hadith tukufu ya Al-Bukhari iliyopokewa na Al-Ahnaf bin Qais, aliyesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: «ِإذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ. قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ هَذَا الْقَاتِلُ فَمَا بَالُ الْمَقْتُولِ؟ قَالَ: إِنَّهُ كَانَ حَرِيصاً عَلَى قَتْلِ صَاحِبِهِ» “Iwapo Waislamu wawili watakutana kwa panga zao basi (wote wawili) muuaji na aliyeuawa wamo Motoni.” Nikasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ)! Ni sawa kwa muuaji, lakini vipi kuhusu yule aliyeuawa?’ Alisema, ‘Aliyeuawa alikuwa na shauku ya kumuua mpinzani wake.” Basi, vipi ikiwa mapigano haya ni kwa maslahi ya Marekani na vibaraka wake? Bila shaka ni jambo zito na uchungu zaidi.
Hatimaye, kiongozi Hizb ut Tahrir, asiye wadanganya watu wake, anakuiteni, watu wa Sudan:
Nyinyi ndio mliomuitikia Khalifa Uthman, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, na mkaubeba Uislamu aliokuitieni katika mwaka wa 31 H, na mkawa watu wake kwa mamia ya miaka. Na nyinyi ni vizazi vya Ali bin Dinar, aliyeasisi Abyar Ali katika Miqat ili kuwatumikia mahujaji, kisha akauwawa shahidi katika vita dhidi ya makafiri, na akapata moja ya kheri mbili.
Tunakulinganieni musimame dhidi ya mfumo huu wa kihalifu wa utatu, ambao ni: kuigawanya nchi kwa kuitenganisha Darfur baada ya kuitenganisha kusini ... kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu Ardhi Iliyobarikiwa na kueneza ufisadi ndani yake ... hivyo vita hivi kati ya Waislamu ni vya dhambi.
Hivyo tibueni utatu huu, na hakikisheni kwamba nchi ina jeshi moja ambalo linaelekeza bunduki zake dhidi ya wakoloni makafiri, kwani katika hilo umo ushindi mkubwa.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]. Je, mtaitikia?
7 Shaaban 1446 H
6 Februari 2025