Hizb ut Tahrir / Kenya Iliandaa Msururu wa Amali katika Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 104 ya kuondolewa kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir/Kenya ilifanya kampeni nchi nzima katika mwezi mtukufu wa Rajab 1446 H. Kampeni hii iliyoanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab ilihusisha shughuli mbali mbali; Darsa, Semina na Visimamo. Hii ilikuwa ni kuukumbusha Ummah kuhusu hali yake ya kusikitisha ambayo umekuwa ukikabiliana nayo tangu kuondolewa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M.