Baada ya Kutazama Tu Mauaji ya Kinyama kwa Siku 467, Watawala wa Pakistan Sasa Wanasherehekea Usitishaji Vita
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
“Watu wa Pakistan wanaungana nami katika kukaribisha tangazo la usitishaji mapigano uliosubiriwa kwa muda mrefu nchini Palestina,” Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, aliandika kwenye ukurasa wa Twitter mnamo tarehe 16 Januari 2025. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kwa zaidi ya mwaka mmoja, utawala wa Munir-Sharif umekuwa ukitizama tu vifo na uharibifu huko Gaza, ambako mauaji ya halaiki ambayo hayajawahi kuonekana yalitokea, na walionusurika sasa kuganda kwa baridi hadi kufa. Walikuwa wakiyatazama haya yote, kana kwamba Pakistan haina jeshi kubwa zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu, na kana kwamba jeshi hilo nimeundwa kwa watu wasio na uwezo, dhaifu, waoga na vilema, kwa hivyo watawala hawawezi kufanya chochote kujibu ukatili huu isipokuwa kulaani, kushutumu na kupinga.