Mauaji Baada ya Mauaji Yanaendelea Gaza Huku Marekani Ikiendelea Kuwezesha Mauaji ya Halaiki na Dunia Imetulia Tuli
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 5 Januari, iliripotiwa kwamba umbile la mauaji la Kizayuni lililishambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza zaidi ya mara 100 katika muda wa siku 3 tu, na kuua zaidi ya watu 200 - wengi wanawake na watoto. Shabaha hizo zilijumuisha majengo ya makaazi, vikundi vya watu waliokusanyika barabarani na sokoni, na wale walio ndani ya makaazi yao. Pia iliripotiwa kuwa mtoto wa 8 aliganda hadi kufa katika Ukanda huo kutokana na baridi kali inayovumiliwa na wale wanaoishi katika mahema ya muda ambayo hayatoi ulinzi dhidi ya hali ya hewa ya baridi kali, na pia kutokana na kikwazo katili cha Wazayuni ambacho kinazuia mahitaji muhimu kama vile chakula, mafuta na nguo za majira ya baridi na blanketi kutokana na kuingia Gaza.