Katika Kumbukumbu ya Kila Mwaka ya Kuvunjwa Khilafah na ukingoni mwa kuregea kwake, Tunaulingania Umma wa Kiislamu Uharakishe Kuisimamisha
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tangu Khilafah ilipovunjwa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, Ummah umekuwa ukipitia majanga na kushindwa mfululizo; kuanzia mgawanyiko wa ardhi yake, mpaka kunyang'anywa mali yake, na kuwaua wanawe, na kudhihakiwa matukufu yake na mashambulizi dhidi ya Sharia yake. Hata hivyo, leo Khilafah iko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kurudi, Rayah (bendera) yake iko tayari kupeperushwa kwa mara nyengine tena juu ya ardhi za Waislamu. Kwa hakika, tunaishi katika wakati unaokumbusha usiku ule watu wa Madina walipokuwa wakishauriana, wakikubaliana kwamba wakati umefika wa kumpa Bay'ah bwana wetu Muhammad (saw) kama kiongozi wao wa kisiasa na mkuu wa dola.