Jumatano, 06 Sha'aban 1446 | 2025/02/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Wauyghur Pia Ni Sehemu ya Umma Bora, Musiwasahau

Tunapokaribia kumbukumbu ya mwaka wa 104 wa kuvunjwa kwa Khilafah, Umma wa Kiislamu unaendelea kupokea habari za ukandamizaji kutoka kwa maadui wake kila mahali, kuanzia Palestina hadi Syria, Sudan, Misri na China, ambako Waislamu wa Uyghur wanavumilia mateso na vikwazo vikali katika kila nyanja ya maisha yao.

Soma zaidi...

Katika Kumbukumbu ya Kila Mwaka ya Kuvunjwa Khilafah na ukingoni mwa kuregea kwake, Tunaulingania Umma wa Kiislamu Uharakishe Kuisimamisha

Tangu Khilafah ilipovunjwa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, Ummah umekuwa ukipitia majanga na kushindwa mfululizo; kuanzia mgawanyiko wa ardhi yake, mpaka kunyang'anywa mali yake, na kuwaua wanawe, na kudhihakiwa matukufu yake na mashambulizi dhidi ya Sharia yake. Hata hivyo, leo Khilafah iko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kurudi, Rayah (bendera) yake iko tayari kupeperushwa kwa mara nyengine tena juu ya ardhi za Waislamu. Kwa hakika, tunaishi katika wakati unaokumbusha usiku ule watu wa Madina walipokuwa wakishauriana, wakikubaliana kwamba wakati umefika wa kumpa Bay'ah bwana wetu Muhammad (saw) kama kiongozi wao wa kisiasa na mkuu wa dola.

Soma zaidi...

Nani Anasherehekea Maadhimisho ya Isra na Mi’raj?

Tawala za ulimwengu wa Kiislamu zinatoa wito wa kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka huu, licha ya kuwa wametambua uwepo wa umbile linaloinajisi ardhi iliyobarikiwa ya Isra na Mi’raj. Wamesimama kando, wakishuhudia mito ya damu ya Wapalestina ikitiririka, mabomu yaliyosababisha nyumba kuwa vifusi, na uharibifu ulioharibu vitongoji, mazao, na vizazi. Wametazama huku hofu ikiwashika wazee na vijana, huku njaa isiyo kifani ikiwasibu, na huku baridi ikigandisha miguu na nyoyo za watu.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Kenya Iliandaa Msururu wa Amali katika Kumbukumbu ya Miaka 104 ya Kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah

Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 104 ya kuondolewa kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir/Kenya ilifanya kampeni nchi nzima katika mwezi mtukufu wa Rajab 1446 H. Kampeni hii iliyoanza mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Rajab ilihusisha shughuli mbali mbali; Darsa, Semina na Visimamo. Hii ilikuwa ni kuukumbusha Ummah kuhusu hali yake ya kusikitisha ambayo umekuwa ukikabiliana nayo tangu kuondolewa kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M.

Soma zaidi...

Kuondolewa kwa Umbile la Kiyahudi ndio Suluhisho Pekee, Sio Suluhisho la Dola Mbili, Safadi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi, wakati wa kushiriki kwake katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos mnamo Jumatano, 22/01/2025, alisema kuwa mbinu yoyote ya baadaye ya Gaza lazima iegemee juu ya umoja wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi na lengo la kufikia amani tu kwa msingi wa suluhisho la dola mbili. Alisema: “Katika muktadha wa suluhisho la kisiasa, serikali ya Palestina ndiyo pekee inayoshikilia uamuzi wa amani na vita, na hakupaswi kuwe na makundi ya kisilaha nje yake.”

Soma zaidi...

Pesa Zilizotumika Kutuua, Tunawezaje Kujitolea Kuzilipa?!

Katika mahojiano na gazeti la ‘Financial Times’, waziri wa mambo ya nje wa Syria alifichua ruwaza ya serikali mpya ya Syria baada ya Assad, akisisitiza kwamba nchi hiyo “haitaki kuishi kwa msaada,” na kwamba suluhisho liko katika kupunguza vikwazo vya Amerika na Ulaya. Aliongeza kuwa serikali haina mpango wa kusafirisha mapinduzi hayo ng’ambo au kuingilia masuala ya nchi nyingine. Hivyo, ikionyesha mabadiliko makubwa katika sera ya kigeni. Pia alionyesha katika mahojiano yayo hayo nia ya kubinafsisha bandari na viwanda vinavyomilikiwa na serikali na kuvutia uwekezaji wa kigeni, licha ya changamoto kubwa zinazoikabili Syria, ikiwemo madeni ya dolari bilioni 30 kwa washirika wa zamani wa Assad; Iran na Urusi.

Soma zaidi...

Machafuko na Ghasia nchini Sudan Kusini Zinasisitiza Haja ya Umma kuwa na Kiongozi mwenye Kuwalinda

Ulimwengu umefuatilia machafuko ya Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, ambayo yalilenga watu waliokimbia makaazi yao na wakaazi kutoka Sudan Kaskazini. Matukio haya yalichochewa na ripoti zinazowatuhumu wanajeshi wa Sudan kwa kuwaua watu kutoka Sudan Kusini huko Wad Madani baada ya jeshi kuutwaa tena mji huo. Kulingana na gazeti la ‘Sudan Tribune’, Wasudan watatu waliuawa mjini Juba, na wengine saba kujeruhiwa.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu