Kuondolewa kwa Umbile la Kiyahudi ndio Suluhisho Pekee, Sio Suluhisho la Dola Mbili, Safadi
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi, wakati wa kushiriki kwake katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos mnamo Jumatano, 22/01/2025, alisema kuwa mbinu yoyote ya baadaye ya Gaza lazima iegemee juu ya umoja wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi na lengo la kufikia amani tu kwa msingi wa suluhisho la dola mbili. Alisema: “Katika muktadha wa suluhisho la kisiasa, serikali ya Palestina ndiyo pekee inayoshikilia uamuzi wa amani na vita, na hakupaswi kuwe na makundi ya kisilaha nje yake.”