Jumatano, 13 Sha'aban 1446 | 2025/02/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kutangaza Jamhuri nchini Syria ni Usaliti wa Mapinduzi ya Kiislamu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ahmed al-Shara, ambaye alifanya ziara yake ya kwanza ya kigeni nchini Saudi Arabia baada ya kuchukua kiti cha Urais nchini Syria, alitoa taarifa muhimu kuhusu mustakabali wa Syria sambamba na ramani ya utendakazi ya kisiasa ambayo amedumisha katika mahojiano na televisheni ya Syria. Akiahidi kukuuza uchumi wa soko huru na vifaa vya uwekezaji, Shara alisema, "Syria ni nchi ambayo itahifadhi hali yake ya asili, muundo wa serikali utakuwa wa jamhuri, kutakuwa na bunge, tawi la utendaji na mamlaka zinazofanya kazi kwa ushirikiano kati yao." alitumia maneno yake. (Mawakala)

Maoni:

Ahmad al-Shara amewavunja moyo watu wa Syria na mujahidina wa dhati kwa kauli zake baada ya operesheni ya kijeshi iliyoanzishwa baada ya watu wa Idlib kuendelea kudai kufunguliwa tena kwa mipaka kwa miaka mingi na ambayo ilisababisha dhalimu Bashar al-Assad kutorokea Urusi mnamo 8 Disemba 2024. Zinaendelea pia kuwafurahisha makafiri wa Magharibi, haswa Marekani na washirika wao wa ndani katika kanda hii.

Shara ambaye alitoa msamaha kwa mabaki ya utawala huo mara tu alipochukua madaraka na kuwalingania wananchi kwenye amani na maridhiano kwa kusema kuwa hawatatenda kwa hisia za kulipiza kisasi, anajaribu kila njia kuhakikisha jina la mapinduzi ya Syria halinasibishwi na Uislamu. Kila Muislamu anayefuata siasa zake kwa akili anaona kwamba anajifanya kana kwamba anawajibika kwa Magharibi na mfumo wa kimataifa, na sio kwa watu wa Syria. Subhanallah!

Ahmad al-Shara hataji maamrisho na masuluhisho ya Uislamu katika hotuba yake yoyote, kana kwamba anauonea aibu Uislamu. Anazungumza kana kwamba itikadi na utaratibu wa Uislamu hauna uwezo wa kuwaunganisha watu wa Syria na kutawala kwa uadilifu, kana kwamba dini ya Mwenyezi Mungu haitoi ruwaza ya maendeleo. Akiongea hivi, anajidhalilisha yeye mwenyewe na mapinduzi ya Syria. Haijalishi ni maelezo gani yanaangaliwa, kuna makubaliano na kujisalimisha! Inamaanisha nini kutaka amani na umbile la Kiyahudi wakati liliposhambulia Syria, kuharibu nguvu zake zote za kijeshi, kupanua ukaliaji wake wa kimabavu wa Milima ya Golan? Watu wa Syria wamepiga kelele kwamba wanataka sharia na Khilafah kwa muda wa miaka 13, wamelipia gharama kubwa kwa hili, huku mujahidina kutoka pande zote za dunia walipigana kwenye njia hii, unamaanisha nini kusema "Syria itakuwa Jamhuri ya Kiarabu"?

Ina maanisha nini kuitelekeza bendera ya Tawhid na kuchukua bendera ya Sykes-Picot? Ina maanisha nini kumpongeza rais mwenye kiburi wa Marekani, kafiri mkoloni, adui mkubwa wa Uislamu na Waislamu, anayezifungamanisha Urusi na Iran, waungaji mkono wakubwa wa Bashar al-Assad, juu ya watu wa Syria, ambaye aliipa Uturuki nafasi ya kuyapotoa njia mapinduzi, na kusema kwamba anaamini kwamba ataleta amani na utulivu Mashariki ya Kati? Inamaanisha nini mara kwa mara kutumia misemo kama vile "serikali jumuishi" na "serikali ya kiraia" kuashiria na kutoa ahadi kwa vyombo vya habari vya Magharibi kwamba wanakumbatia demokrasia? Uislamu uko wapi katika hili? Izza iko wapi katika hili? Mtazamo wa kisiasa uko wapi katika hili? Je, kauli zote hizi eti zilitolewa kwa ajili ya Syria kuinuka kweli zitawaridhisha makafiri wa Magharibi? Hapana! Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha waziwazi:

[وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ]

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao...” (Baqarah 120)

Kila makubaliano yatakayofanywa yatapelekea kwenye makubaliano mengine. Pindi haramu ikisha fanywa, haramu nyingine itakuja kwa urahisi moyoni. Shetani atanong’ona kwamba hakuna njia nyingine isipokuwa kuingiliana na makafiri, akisema “dhurufu zinalazimisha jambo hilo. Ugaidi”; lakini mwishowe, makafiri hawa watawalizimisha Waislamu kuwaelekezea bunduki ndugu zao kwa badali ya uungaji mkono wao. Ukweli ni, kuuliwa kwa mujahidina nchini Syria kunaonyesha dhahiri hali hii. Mauaji haya yataelekezwa kwa wale wanaopinga Syria kuwa jamhuri ya kisekula ya Kiarabu chini ya kisingizio cha “kupambana na ugaidi”; wale ambao hawaridhiki na amani na Mayahudi, wale ambao wanawakumbusha wasimamizi wa mapinduzi na kutaka kusimamishwa kwa Khilafah ya Kiislamu nchini Syria. Ahmad al-Shara alisema, “Tumetupa vumbi la udhalilifu na unyonge juu ya Damascus.” Kwa maneno yake hayatabadilisha ukweli huu. Hakuna ushahidi unaotangaza kwamba mapambano ya Kiislamu baada ya madikteta kupinduliwa. Hata hivyo, kuna uthibitisho imara kwamba kuegemea kwa makafiri, kuingia katika miundo yao ya kifikra na kisiasa, na kuwafanya marafiki makafiri badala ya waumini kutawatia hasara duniani na kesho akhera!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua.” (Anfal 27)

Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) awape nguvu na busara watu wa Damascus na mujahidina wenye ikhlasi kuyalinda mapinduzi ya Syria dhidi ya khiyana na mitego, na awasaidie Waislamu wote kuendesha Sharia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Emin Yildirim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu