Jumatano, 13 Sha'aban 1446 | 2025/02/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhamisho au Ukombozi, enyi Umma wa Kiislamu?
(Imetafsiriwa)

Dhalimu wa Marekani, Trump, alisema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mhalifu Netanyahu jioni ya Jumanne, 4 Februari 2025: "Marekani itachukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya kazi nayo pia" Aliongeza, "Tutageuza Ukanda wa Gaza ulioharibiwa kuwa Riviera ya Mashariki ya Kati." Alizungumzia juu ya umiliki wake wa muda mrefu wa Gaza na alisisitiza taarifa yake ya awali kuhusu kuwahamisha watu wa Gaza, ambapo alisisitiza kutiishwa kwa watawala wa Misri na Jordan na wasaidizi wao, akisema: "Misri na Jordan zilisema hazitapokea wakaazi kutoka Gaza, na mimi nasema lazima watapokea." Hapo ndio watawala watiifu, wasaliti.

Trump anawatishia watu wa Palestina kwa janga jipya lisilopungua la Nakba ya 1948 au Naksa ya 1967. Anazungumza kwa kiburi kana kwamba Palestina ni milki yake au mkoa wa nchi yake. Huu ndio uhalisia ambao Waislamu hivi sasa wanauona kuhusiana na kadhia ya Palestina, ambayo imeachwa mikononi mwa Marekani na mataifa ya kikafiri.

Enyi Waislamu kwa jumla na hasa watu wa Ardhi Iliyobarikiwa:

Kutenganisha kadhia ya Palestina na Uislamu na Umma wa Kiislamu, na kuiachia Marekani na Kamati ya Kimataifa, na kuifungamanisha na maazimio ya kimataifa kutasababisha tu kufutwa kwa kadhia ya Palestina. Huu ni uhalisia ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu ametutahadharisha nao, akituita kwa tahadhari.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَى أَعْقَابِكُمْ فَتَنْقَلِبُوا خَاسِرِينَ * بَلِ اللهُ مَوْلَاكُمْ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ]

Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri. Bali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wenu, naye ndiye bora wa wasaidizi.” [Surat Aal-i-Imran:149-150].

Kuikabidhi kadhia ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa kwa tawala za wasaliti na Mamlaka ya Palestina kumeliwezesha umbile la Kiyahudi kuendelea, kupanua makaazi yake, na kutoa ulinzi kwa mauaji na kuhamishwa kwenu kutoka kwa ardhi yenu. Msidanganywe na kauli zao tupu za kukataa uhamishwaji; hawa ni washirika katika uhalifu. Yeyote anayekubali uharibifu atakubali uhamishwaji, na wale waliotiwa doa la khiyana na usaliti, ambao wameiacha ardhi, bila shaka watakubali kuhamishwa. Iwapo suala la Palestina halitarudishwa kwa Uislamu na Umma wa Kiislamu, na ikiwa majeshi ya Waislamu hayatahamasishwa kuzipindua tawala za vibaraka na kufanya jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuikomboa ardhi takatifu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt), Palestina na ardhi za Waislamu zitaendelea kukandamizwa na Marekani, Mayahudi na watawala wao vibaraka.

Enyi Waislamu: Kauli za Trump kuhusu Palestina, Canada, Panama, China na nyinginezo ni taswira ya kweli ya fikra za madhalimu wa kibepari. Kwao, dunia si kitu zaidi ya maslahi na faida. Hii ndiyo dhati ya mfumo wa kibepari, na nchi zote za Magharibi hufikiri kwa kuzingatia haya. Mfumo wa kibepari umejengwa juu ya utumizi na ubinafsi, wenye kuzalisha viongozi ambao ni wauaji na maadui wa wanadamu. Viongozi wa mfumo huu wamefanya mauaji ya kikabila katika koloni walizozikalia kimabavu.

Leo hii, dunia inaishi katika giza la ubepari na ukafiri na itaendelea kutangatanga katika mashimo haya ya giza hadi pale Khilafah itakapoiokoa. Kutokuwepo kwa Khilafah yenye nguvu kumepelekea vita viwili vya dunia, na kuua watu wapatao milioni 100, na mitambo yao ya kuua bado inafanya kazi kwa njia mbalimbali. Barani Afrika, zaidi ya watu milioni 20 waliokimbia makaazi yao wanateseka kwa njaa, magonjwa, na mizozo inayochochewa na dola kubwa za Magharibi. Ulimwengu leo ​​umesimama kwenye ukingo wa vita vyenye uharibifu ambavyo vitaangamiza watu na ardhi.

Ulimwengu mzima leo hii unauhitaji sana Umma wa Muhammad (swt), kwa kuwa ndio Umma pekee wenye uwezo wa kuokoa wanadamu. Sisi tuna ujumbe wa Mola Mlezi wa walimwengu wote, unaoondoa giza na unatupunguzia ugumu wa maisha. Ni Sharia ya Uislamu, rehma ya Mwenyezi Mungu kwa walimwengu.

Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu, Enyi Maafisa na Makamanda:

Je! haujafika wakati wa nyoyo zenu zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na yaliyo teremshwa kwa haki? Je, haujafika wakati wa nyinyi kusimama kwa heshima na kupindua viti vya watawala wanaokutiisheni nyinyi na Ummah wenu kwenye aina zote za udhalilishaji? Je, wakati haujafika kwenu kutambua kwamba Ummah wenu, Ummah wa Muhammad (swt), una uwezo wa kuokoa wanadamu?

Je, haujafika wakati wa nyinyi kutambua kwamba muna uwezo wa kuishinda Amerika, kuikomboa Bayt al-Maqdis, na kusimamisha uadilifu miongoni mwa watu?

Je, wakati haujafika wa nyinyi kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surat At-Tawba:38-9].

Enyi Umma wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt), enyi Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu:

Watu wa Palestina leo hii wanakabiliwa na kifo na kuhamishwa, na nyinyi hamna budi ila kusimama kwa ajili ya ukombozi, kujikomboa kutokana na watawala madhalimu na vibaraka wa Magharibi, na kuandamana na majeshi yenu kuelekea Bayt al-Maqdis ili kuikomboa na kuitakasa kutokana na uchafu wa wavamizi. Ucheleweshaji wowote au kusitasita katika kuwapindua watawala vibaraka katika ardhi za Kiislamu kutatugharimu sana katika damu, watoto na mali zetu.

Jukumu lenu kwa wanadamu, kama mulivyolazimishwa na Uislamu, linawawajibisha kutenda kwa nguvu zenu zote ili kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume na kuziunganisha ardhi za Kiislamu ili kusimama dhidi ya Marekani na maadui wa wanadamu miongoni mwa madhalimu wa kibepari.

Imani ya kweli, kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi, na kukata mafungamano na Shetani na washirika wake, ndivyo vinatufanya tustahiki ushindi wa Mwenyezi Mungu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surat Muhammad:7]. Endapo Mwenyezi Mungu atatunusuru, hakuna wa kutushinda:

[إِنْ يَنْصُرْكُمُ اللهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِنْ يَخْذُلْكُمْ فَمَنْ ذَا الَّذِي يَنْصُرُكُمْ مِنْ بَعْدِهِ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surat Aal-i-Imran:160]. Jihadharini na mfano wa Wamongolia; waliua mamilioni, lakini walishindwa na ikhlasi ya waumini wa Ain Jalut.

Kumtegemea kwetu Mwenyezi Mungu, Mtukufu, hakutenganishwi na imani yetu kwa Ummah wetu, ambao Mwenyezi Mungu ameukabidhi Kitabu chake na wahyi Wake. Msibabaishwe na nguvu na kiburi cha Marekani, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu zaidi juu yao, na nguvu zake zinakunusuruni. Simameni, enyi Waumini wenye nguvu, tangazeni haki, msiogope ila Mwenyezi Mungu, wapindueni watawala vibaraka, toeni ahadi ya utiifu (bay’ah) kwa Khalifa atakayesimamisha Dini baina yenu, na Mwenyezi Mungu atatimiza ahadi yake ya kudhihirisha Dini yake.

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surat At-Tawba:33]. Amesema Tamim al-Dari (ra): Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) akisema: «لِيَبْلُغَنَّ هَذَا الْأَمْرُ ‌مَا ‌بَلَغَ ‌اللَّيْلُ ‌وَالنَّهَارُ، وَلَا يَتْرُكُ اللهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ، إِلَّا أَدْخَلَهُ اللهُ هَذَا الدِّينَ يُعَزُّ عَزِيزٌ أَوْ يُذَلُّ ذَلِيلٌ، عِزّاً يُعِزُّ اللهُ بِهِ الْإِسْلَامَ وَأَهْلَهُ، وَذُلّاً يُذِلُّ اللهُ بِهِ الْكُفْرَ»  “Hakika jambo hili litafika kila mahali panapoguswa na usiku na mchana. Mwenyezi Mungu hataiacha nyumba ya udongo wala manyoa ila ataiingiza dini hii, na kuleta heshima kwa waheshimiwa na kuwafedhehesha waliofedheheka—heshima anayoipa Mwenyezi Mungu Uislamu na watu wake, na fedheha anayoifanya Mwenyezi Mungu juu ya ukafiri.”

Ewe Mwenyezi Mungu, tufikishie kheri hii, na zifungue nyoyo za Waislamu kwayo, na utujaalie kutoka Kwako mamlaka yenye kunusuru. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

H. 7 Sha'aban 1446
M. : Alhamisi, 06 Februari 2025

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu