Watoto wa Mashariki Mwa Ghouta Wanaangamizwa! Ni Nani Atakaye Hifadhi Damu Zao?!!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo 22 Februari, shirika la Kiingereza la kuchunguza haki za kibinadamu za watu wa Syria lilisema kuwa zaidi ya watu 400 waliuwawa, ikiwemo watoto 150 katika shambulizi baya la mabomu lililopita la siku 5 Mashariki mwa Ghouta lililofanywa na majeshi katili ya Syria na Urusi, ambayo yanalenga kiholela nyumba za raia, maduka, mashule, mahospitali na masoko, yakiwaacha watoto wakiwa wamezikika katika vifusi vya majumba. Watoto wamelazimika kutafuta hifadhi katika mapango, mashimo au mivungu ya nyumba zao huku 'wakisubiri zamu yao kufa'.