Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 10 Jumada II 1439 | Na: 1439/013 |
M. Jumatatu, 26 Februari 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto wa Mashariki Mwa Ghouta Wanaangamizwa!
Ni Nani Atakaye Hifadhi Damu Zao?!!
Mnamo 22 Februari, shirika la Kiingereza la kuchunguza haki za kibinadamu za watu wa Syria lilisema kuwa zaidi ya watu 400 waliuwawa, ikiwemo watoto 150 katika shambulizi baya la mabomu lililopita la siku 5 Mashariki mwa Ghouta lililofanywa na majeshi katili ya Syria na Urusi, ambayo yanalenga kiholela nyumba za raia, maduka, mashule, mahospitali na masoko, yakiwaacha watoto wakiwa wamezikika katika vifusi vya majumba. Watoto wamelazimika kutafuta hifadhi katika mapango, mashimo au mivungu ya nyumba zao huku 'wakisubiri zamu yao kufa'. Madaktari wameishia kuchunga watoto wachanga na wanaozaliwa kabla ya muda wao kufika ndani ya chupa za mashini (incubators) katika mivungu huku wakikabiliwa na kifo kutokana na baridi kali. Katibu Mkuu wa UM ameisifu hali hii kuwa "Jahannam ardhini". Zaidi ya hayo, chakula, mafuta na madawa viko katika uhaba mkubwa kutokana na vikwazo vya serikali ya Syria kwa takriban miaka 5, vinavyo pelekea baa kubwa la njaa linalo athiri watoto zaidi. Kwa mujibu wa UM, takriban asilimia 12% ya watoto chini ya miaka 5 wanasemekana kuanza kukabiliwa na ukosefu wa lishe bora. Hali hii ni mbaya mno kiasi ya kuwa kina mama wa watoto hawa wanatamani Allah azichukue roho za watoto hawa ili kumaliza mateso kwao, au basi watoto wao wapate angaa afueni ya kushiba kabla ya kifo kuwachukua ambacho wanakiona kisichokuwa budi kutokana na mashambulizi haya ya mabomu.
Tunaiona mvua ya mabomu ikinyesha vichwani mwa watoto wenye njaa wa Mashariki mwa Ghouta huku wakikabiliwa na maangamivu. Tunaziona safu baada ya safu za watoto waliouwawa waliokafiniwa kwa sanda zilojaa damu. Tunayaona machozi ya kina mama wa Ghouta wakililia tonge ya chakula kuwalisha watoto wao wadogo wanaokufa kwa njaa. Na tunauona uharibifu mkubwa kwa ardhi hii tukufu, na ndugu zetu na dada zetu wakichinjwa ili wajisalimishe, wakijizatiti dhidi ya uvamizi wa ardhini wa makatili wauwaji wa Assad, pengine mabaya zaidi kuliko yaliyo tokea mjini Aleppo. Na mbali na hayo licha ya maovu yote haya, jamii ya kimataifa, UM, serikali za ulimwengu wa Kiislamu wamesalia kutazama, kupuuza umwagaji damu huu, na kutoa idhini kwa Assad na wahalifu washirika wake – hawa wauwaji wa watoto – kuendelea kuchinja pamoja na kukiuka sheria. Wamekwenda katika makongamano yao yote kwa lengo la kulinda maisha ya wanadamu, haki za kibinadamu, na haki za watoto! Ni dhahiri, hata hii 'Jahannam ardhini' haitoshi kutingisha utu wao! Kwao wao, mito ya damu, iliyoundwa kutokana na watoto wa Ghouta ni gharama inayostahili kulipia maslahi yao ya kisiasa yanayo churuza damu katika eneo hili! Kwa yakini, inaonesha kuwa hakuna mpaka kwa ukatili huu ambao wako tayari kuushuhudia ili kupata malengo yao ya kibinafsi.
Kwa hakika hakuna dalili zaidi inayo hitajika kuonesha kuwa hatuwezi kuweka matarajio yetu hata kidogo kwa serikali za Kimagharibi zilizojaa ubinafsi na kukosa utu, UM, au serikali zilizoko katika ulimwengu wa Kiislamu kuulinda Umma nchini Syria wakati ambapo wamewatelekeza watoto wa Ghouta wakifariki, huku ile inayoitwa mipango ya amani, mapatano na mapendekezo ya suluhisho yakimpa katili Assad muda zaidi kuangamiza, kubaka na kuuwa Waislamu. Tunayoshuhudia katika runinga zetu ya maovu eneo la Mashariki mwa Ghouta, lililopewa lakabu ya "eneo linalopunguzwa makali" katika mchakato wa amani wa Astana wa mwaka jana, ndio sura halisi ya ule unaoitwa 'mpango wa amani' machoni mwa Urusi, Uturuki, Iran na jamii ya kimataifa!
Kutokana na majanga haya yanayo vunja moyo tunayo shuhudia eneo la Ghouta, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimeanzisha kampeni mtandaoni chini ya anwani, "Ni Nani Atakaye Wahami Watoto wa Ghouta?". Kinausihi Umma, na hususan watu wenye kumiliki nguvu katika majeshi ya Waislamu kusimamisha kwa haraka Khilafah kwa msingi wa manhaj ya Utume, kwani ni uongozi huu wa Kiislamu pekee ndio unaojali kwa dhati utukufu wa maisha ya wanadamu na ambao utakuwa ngao ya waumini, itakayo komesha Jahannam hii ardhini pamoja na uchinjaji na idhilali kwa Waislamu ulimwengu mzima.
(وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا)
“Na mna nini msipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako?” [An-Nisaa: 75]
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |