Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Siasa za Chuki na Migawanyiko ni Dalili Tosha ya Kufilisika Kifikra kwa Siasa ya Demokrasia na Wafuasi Wake

Hatimaye, rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kuhudumu kwa muhula wa pili kwenye sherehe iliohudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali na kususiwa na wanasiasa wa upinzani. Hafla hii imekuja huku nchi ikighubikwa na migawanyiko ya kikabila, semi za chuki na umwagikaji wa damu.

Soma zaidi...

Watoto wa Rohingya Wanadhalilishwa Mikononi mwa Mabudha! Je, Wanaye Mtetezi?

Shirika la misaada la Médecins Frontiéres, limeripoti kuwa zaidi ya nusu ya wasichana katika kambi ya wakimbizi wa Rohingya eneo la Cox's Bazar, Bangladesh ambao limewatibu baada ya kudhulimiwa kimapenzi na kubakwa nchini Myanmar wako chini ya umri wa miaka 18, na wengine wako chini ya miaka 10. Limeeleza kuwa mamia ya wasichana wa Rohingya wamepewa usaidizi wa kimatibabu na wa kisaikolojia katika kliniki yake mjini Kutupalong inayotibu wahanga wa dhulma za kijinsia lakini likasisitiza kuwa hao ni sehemu tu ya wale wanao amanika kudhulumiwa kimapenzi na kubakwa na majeshi katili ya kibudha tangu kutokea kwa kampeni ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Rohingya mnamo Agosti

Soma zaidi...

Wala Msiwe Katika Washirikina Katika Wale Walioitenga Dini Yao Na Wakawa Makundi Makundi Kila Kikundi Kinafurahia Kilicho Nacho

Hatua ya mahakama ya juu kuamuru marudio ya uchaguzi Oktoba 26, 2017 imezusha fukuto la kisiasa nchini. Baada ya kuubatilisha uchaguzi wa mwezi Agosti 2017, kumeshuhudiwa vuta ni kuvute juu ya usimamizi wa uchaguzi mpya baina ya mirengo miwili ya kisiasa (Jubilee na Nasa).

Soma zaidi...

Gharama Kubwa Inayolipwa na Raia Eneo la Deir al-Zour Na Watawala wa Waislamu katika Meza ya Majadiliano kwa Kuketi na Kukutana na Muuwaji

Ndege za kivita za Urusi, kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kimaeneo kutoka Deir al-Zour, zimefanya mashambulizi ya msururu wa mabomu juu ya feri za mtoni zilizokuwa zimebeba maelfu ya raia wanaokimbia eneo la Deir al-Zour kuelekea maeneo mengine, yakisababisha zaidi ya vifo hamsini na maelfu kujeruhiwa, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake.

Soma zaidi...

Huku wakitelekezwa na Serikali Zisizo na Utu za Waislamu, Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wakimbizi wa Rohingya Wanakabiliwa na Baa la Njaa, Maradhi na Vifo Nchini Bangladesh

Mnamo Jumapili 17 Septemba, shirika la msaada la ‘Save the Children’ lilionya kuwa wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh huenda wakafariki kutokana na uhaba wa chakula, makao, na bidhaa msingi za usafi. Zaidi ya Waislamu wa Rohingya 410,000 wamekimbia Myanmar na kwenda Bangladesh tangu Agosti 25 kutokana na kampeni ya mauaji ya halaiki inayotekelezwa na jeshi la Burma. Kwa mujibu wa shirika la UNICEF, asilimia 80% ya wakimbizi hawa ni wanawake na watoto, 92,000 kati yao wako chini ya umri wa miaka 5, na takriban wanawake 52,000 ni waja wazito au wananyonyesha.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu