Katika ripoti iliyo chapishwa na kituo cha habari cha Al-Jazeera idhaa ya Kiingereza, maafisa wa Umoja wa Mataifa (UM) walishutumu kuendelea kukamatwa kiholela kwa watoto katika Ardhi Tukufu (Palestina) na umbile la Kiyahudi, ikisema kuwa “Unyimaji uhuru huu kwa watoto hawa ni wa kitaasisi, kinidhamu, na ulio enea pakubwa”. Msururu wa ripoti za UM zilizo wasilishwa katika lile linaloitwa Baraza la Haki za Kibinadamu zimeonyesha jinsi hali za maisha za watu wa ardhi tukufu ya Palestina na Ukingo wa Magharibi na Gaza zilivyo zidi kudorora kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, na jinsi watoto wanavyo himili ukatili wa uvamizi wa umbile la Kiyahudi, kwa mujibu wa Kate Gilmore, Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa UM.