Jumatano, 06 Sha'aban 1446 | 2025/02/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mauaji Baada ya Mauaji Yanaendelea Gaza Huku Marekani Ikiendelea Kuwezesha Mauaji ya Halaiki na Dunia Imetulia Tuli

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 5 Januari, iliripotiwa kwamba umbile la mauaji la Kizayuni lililishambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza zaidi ya mara 100 katika muda wa siku 3 tu, na kuua zaidi ya watu 200 - wengi wanawake na watoto. Shabaha hizo zilijumuisha majengo ya makaazi, vikundi vya watu waliokusanyika barabarani na sokoni, na wale walio ndani ya makaazi yao. Pia iliripotiwa kuwa mtoto wa 8 aliganda hadi kufa katika Ukanda huo kutokana na baridi kali inayovumiliwa na wale wanaoishi katika mahema ya muda ambayo hayatoi ulinzi dhidi ya hali ya hewa ya baridi kali, na pia kutokana na kikwazo katili cha Wazayuni ambacho kinazuia mahitaji muhimu kama vile chakula, mafuta na nguo za majira ya baridi na blanketi kutokana na kuingia Gaza. Mama wa mtoto alisema, “Hawakutoa hata dakika moja ya kujisikia furaha na mtoto wangu… Alikufa kwa sababu ya hali ya hewa ya baridi sana. Alilala karibu yangu na asubuhi nilimkuta akiwa ameganda na amekufa.” Hii ni katika wakati ambapo hospitali zote za kaskazini mwa Gaza zimefungwa kutokana na mashambulizi ya anga ya Wazayuni na uvamizi wa mara kwa mara katika vituo vya matibabu, na kusababisha maelfu ya watu kukosa huduma muhimu za afya ikiwa ni pamoja na njaa na kuwagandisha watoto. Wakati huo huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, Rais wa Marekani Joe Biden ameliarifu Bunge la Congress la Marekani kuhusu mpango wa mauzo ya silaha ya dolari bilioni 8 kwa ajili ya uvamizi huo ambayo yatajumuisha makombora yenye pauni 500 aina ya warheads, mabomu, makombora ya ndege na helikopta za mashambulizi, na makombora ya anga hadi anga, licha ya idadi kubwa ya vifo katika Ukanda huo.

Maoni:

Mauaji ya halaiki huko Gaza yamefichua kwa dunia ombwe la kimaadili lililopo ndani ya dola kubwa za dunia ambazo ziko tayari kufadhili na kuandaa umwagaji damu huu bila kujali kiwango kikubwa cha vifo, uharibifu na mateso ambacho zimesababisha. Stephen Zunes, profesa wa kisiasa katika Chuo Kikuu cha San Francisco, alitoa maoni yake kuhusu mpango wa kupeleka silaha zenye thamani ya dolari bilioni 8 kwenye uvamizi huo, “'Israel' inatumia silaha hizi kwa kasi kubwa, kama ilivyodhihirishwa na vifo hivyo vikubwa na uharibifu unaoendelea, na Biden yuko tayari kuzisambaza tena.” Agosti iliyopita, Washington iliidhinisha kifurushi tofauti chenye thamani ya dolari bilioni 20 kwa ajili ya umbile la Kiyahudi la mauaji ya halaiki, ambacho kilijumuisha ndege za kijeshi, magari ya kijeshi, na mabomu na makombora, huku mwezi Novemba, utawala wa Biden uliidhinisha kifurushi chengine cha silaha cha dolari milioni 680 kwa uvamizi huo.

Ni dhahiri kwamba mauaji ya halaiki na uvamizi huu hautakwisha chini ya mfumo wa sasa wa dunia ambapo hakuna dola, kiongozi, au shirika au taasisi ya kimataifa yenye nia ya kisiasa ya kuchukua hatua madhubuti kukomesha mauaji haya ya watu wengi. Mauaji haya hayatakwisha kwa kauli tupu za kulaani kutoka kwa Umoja wa Mataifa, au hukumu zisizo na nguvu kutoka kwa ICC au ICJ. Kuzitegemea taasisi hizo kukomesha mauaji haya ya halaiki au kupata haki kwa Wapalestina ni kupotea njia kukubwa, kwani zinatumikia maslahi ya dola kubwa za magharibi badala ya mataifa yanayodhulumiwa duniani. Kwa hiyo, kuendelea kuziamini serikali au taasisi za mfumo wa sasa wa dunia kukomesha kiwango hiki cha kiviwanda cha mauaji ya watu wengi, kunatoa tu matumaini ya uongo na hivyo kurefusha mateso, dhulma na masaibu ya kutisha ya Wapalestina. Fauka ya hayo, Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya juu ya kuweka imani kwa makafiri ili watusaidie na watulinde sisi waumini. Anasema (swt),

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41]

Ili kukomesha mauaji haya ya halaiki inatutaka sisi Waislamu kuchukua mambo yetu mikononi mwetu na kuyatatua kwa mujibu wa Dini yetu na yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) anayaeleza kuwa ndiyo njia ya kuuhami, kuulinda na kuukomboa Ummah wetu. Mtume (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao tu, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.” Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, kwa hiyo ndiyo njia ambayo kwayo Umma wa Kiislamu unajilinda wenyewe na Dini yake kutokana na kushambuliwa na maadui zake. Kwa kukosekana kwa Khilafah, kama tunavyoona leo, Waislamu wanakabiliwa na mauaji ya halaiki na mauaji ya kimbari bila dola au uongozi wa kuwatetea. Hakika Khilafah ndiyo mlinzi wa Umma wa Kiislamu na ardhi zao na Dini yao; na ni dola hii peke yake ambayo inasimamia maslahi ya Waislamu, inapigania mambo yao, na inawalinda dhidi ya dhulma. Ni dola hii pekee ambayo ina utashi wa kisiasa wa kuhamasisha jeshi lake kutetea damu ya Waislamu, bila kujali wanaishi wapi kama inavyoonekana mara kwa mara katika historia ya Kiislamu. Umma wa Kiislamu umekumbwa na mauaji ya halaiki na kampeni za mauaji ya kimbari hapo awali, kama tulivyoona katika uvamizi wa Watartari katika ardhi ya Waislamu katika karne ya 13 wakati ambapo karibu robo tatu ya ulimwengu wa Kiislamu ulikuwa unakaliwa kimabavu kwa mujibu wa baadhi ya makadirio; au uchunguzi wa Wahispania katika karne ya 15 wakati makumi ya maelfu ya Waislamu walipouawa na falme za Kikristo; au uvamizi wa Wakristo wa Palestina kutoka karne ya 11 hadi 13. Katika matukio yote hayo, Waislamu walipata ushindi dhidi ya maadui zao au waliokolewa na kupewa hifadhi kutokana na kuwepo dola ya Khilafah ambayo ilikusanya jeshi lake na kutumia muungano wa rasilimali za ardhi za Waislamu kuwalinda Waislamu.

Kama Waislamu, Dini yetu na historia yetu vinatufundisha somo muhimu katika maisha - ambalo ni kwamba mafanikio na ushindi dhidi ya maadui zetu hupatikana tu kwa kumtii Mwenyezi Mungu (swt), kuchukua masuluhisho kutoka kwa Dini yetu, na sio kuwategemea makafiri kwa ulinzi. Ikiwa tunataka mauaji ya halaiki mjini Gaza na Palestina yote yamalizike, na kila shubiri ya ardhi hii Iliyobarikiwa ikombolewe kutoka kwa uvamizi huu wa kikatili milele, basi ni lazima tulinganie kusimamishwa kwa Khilafah haraka, ambayo ndicho chombo pekee ambacho haya yatafikiwa. Kuweka matumaini yetu katika kitu chengine chochote, kunaupa nguvu tu mkono wa maadui zetu na kuwapa muda zaidi wa kuuchinja Ummah wetu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ * وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ]

“Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet'ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa. Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamwogopa Mwenyezi Mungu na wakamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.” [An-Nur: 51-52].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Asma Siddiq
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu