- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Ripoti ya Habari 11/01/2020
Uthibitisho kwa ulimwengu kwamba usawazishaji mahusiano ni usawazishaji wa watawala na sio usawazishaji wa watu, na kukataa watawala wa Ruwaibidha, na kufuchuliwa kwa habari potofu na uzushi inaofanywa na Al-Burhan, Mwenyekiti wa Baraza Kuu kuwa watu wengi wa Sudan wanaunga mkono usawazishaji mahusiano. Nchini Sudan, katika miji yake anuwai, tunauliza swali ili kuthibitisha wako wapi hao wengi wanaosema wanaunga mkono usawazishaji mahusiano? Lakini wako wapi watetezi wa usaliti na usawazishaji mahusiano, ewe mwongo? Tunasema kuwa watu wetu nchini Sudan wangali wanashikilia kaa la moto la kadhia hii.
Wiki iliyopita ilikuwa imejaa vitendo vikubwa na mawasiliano mazito na umati wa Waislamu ili kuendelea kueneza utambuzi na kuliendeleza taifa la Kiislamu kutokana na mporomoko mbaya ambao limefikia. Katikati ya umati mkubwa wa watu, uhudhuriaji wa hali ya juu, na maingiliano yasiyo na kifani, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Omdurman kaskazini – ilifanya minbar yake ya kila wiki ya mara kwa mara katika Soko la Sabreen Ijumaa Oktoba 23 chini ya kichwa "Kufeli kwa serikali mtawalia kutawala Sudan na mabadiliko yasiyokuwa na budi kwa msingi wa Uislamu."
Mnamo siku ya Jumapili, Oktoba 25, 2020, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iligawanya toleo katika mji mkuu na miji mingi mbali mbali ya Sudan, lililokuwa na kichwa: "Kujiunga kwa Al-Burhan na Hamdok na Gari ya Moshi ya Usaliti Kunathibitisha Kujitolea Kwao kwa Maadui na Uaminifu Wao Kwao Na Yawajibisha Kazi ya Kusimamisha Khilafah." Lililopokewa kwa takbir na tahlil.
Mashababu wa chama katika mji wa Gadharif walikuwa katika safu ya ulinzi wa Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambapo Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mji wa Gadharif walifanya kisimamo cha kulaani kilichopewa anwani: "Usawazishaji Mashusiano na Mayahudi ni kumsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini ” mbele ya Msikiti wa Abdul Qadir Abdul Mohsen baada ya swala ya adhuhuri.
Mnamo siku ya Jumatatu, Oktoba 26, 2020, Mashababu wa Hizb ut Tahrir jijini Khartoum eneo la Bahri waliandaa kisimamo cha kulaani katika kituo cha kikuu - Soko la Bahri kupinga uhalifu uliofanywa na serikali ya mpito nchini Sudan kwa kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi.
Oktoba 27, 2020, Hizb ut Tahrir katika eneo la Omdurman kaskazini la Mapinduzi ya 17 ilitoa hotuba kali ya kisiasa iliyopewa kichwa: "Serikali ya Mpito inakubali uhalifu wa kusawazisha mahusiano kwa kujisalimisha na amri ya Trump!!", ambapo Ustadh Fadlallah Ali alizungumza. Alisisitiza umuhimu wa kadhia hii akilini mwa Waislamu, na kwamba imefungamanishwa na aya na hadithi ambazo haziwezi kufutwa au kukanganywa.
Miongoni mwa kampeni zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan misikitini, ambayo maarufu zaidi ni hotuba iliyotolewa na Mhandisi Basil Mustafa Jumatano, Oktoba 28, 2020 katika Msikiti wa 19 huko Kalakila Mashariki, ambao ilikuwa na kichwa "Ukweli wa Umbile Ovu na Jinsi Mahusiano wa Kimataifa Yalivyo katika Uislamu" Ambapo waumini walifanya maingiliano yasiyo na kifani, na mapema siku hiyo hiyo, Jumatano Oktoba 28, 2020, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika maeneo ya Kalakila na Dukhainat waliandaa kisimamo cha kulaani.
Jumatano haikuisha, kwani ilikuwa siku ndefu iliyowakemea watawala hawa wasaliti; mji wa Wad Madani, ambako Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walifanya kisimamo cha kulaani mbele ya Mnara wa Kazi kupinga uhalifu wa kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi. Mabango na machozi yao yanatiririka chini na kutaka ushindi katika Uislamu, kwa kupinga uhalifu huu ambao uliowasibu watu wa Sudan na utu wao kupitia watawala hawa Ruwaibidah.
Halafu, mnamo siku ya Alhamisi, Oktoba 29, 2020, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Dukhainat katika Soko la Kalakila Al-Lafah katika eneo la Al-Shuqilab walifanya hotuba yao ya kila wiki, ambayo ilikuwa chini ya kichwa "Usawazishaji ... Usaliti wa Aqeeda ya Watu wa Sudan."
Amali zote hizi ni ujumbe wazi kwa watawala hawa vibaraka na ufichuzi wa uwongo na uzushi uliotangazwa na kiongozi wa Baraza la Kuu, al-Burhan, kwamba watu wengi wa nchi hii wanakubali usawazishaji mahusiano. Hii hapa miji anuwai ya Sudan, ukiwemo mji mkuu, na baada ya kuandaa visimamo vyote hivi vya kulaani na hotuba, inapinga uhalifu wa kusawazisha mahusiano.
- Click to open image! Click to open image!

https://domainnomeaning.com/sw/index.php/dawah/sudan/1215.html#sigProId3076817b7a