Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kujiunga kwa Al-Burhan na Hamdok na Gari ya Moshi ya Usaliti Kunathibitisha Kujitolea Kwao kwa Maadui na Uaminifu Wao Kwao

Na Yawajibisha Kazi ya Kusimamisha Khilafah
(Imetafsiriwa)

Watawala wa Sudan walijiunga na treni ya usaliti, baada ya kukubali rasmi kuanza hatua kuelekea usawazishaji wa mahusiano na umbile la Kiyahudi, kufuatia mazungumzo ya watu wanne ambayo yaliwakutanisha Al-Burhan, Hamdok, Netanyahu na Trump, muda mfupi baada ya Trump kutia saini uamuzi wa kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi, Na ilielezwa katika taarifa ya pamoja kwamba "viongozi hao wanne walikubaliana kusawazisha mahusiano kati ya Sudan na 'Israel', na kumaliza hali ya uhasama kati ya nchi zao mbili" (Sudan Tribune). Watawala wa Sudan wamewafanya maadui zetu kufurahia huzuni yetu, kama anavyosema Netanyahu, akimaanisha kubadili hapana tatu kwa ndio: "Ni mabadiliko ya kipekee, leo Khartoum inasema ndio kwa amani, ndio kutambuliwa, ndio kwa kusawazisha mahusiano" (France 24). "Tumehama kutoka kwa hapana tatu hadi ndio tatu," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Morgan Ortagus alisema. (Tovuti ya kituo Al-Hura)!!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan hatuwategemei watawala hawa; Hifadhi ya maovu na usaliti, kwa sababu wao ni vibaraka wa Magharibi kikoloni ya kikafiri, na hawana uhusiano wowote na Umma wao, bali tunautarajia Umma wetu, na tunataka ujifunze mafunzo yake ya sasa huku ikishikilia kwa mkono wa chuma juu ya mambo yafuatayo:

Kwanza: Palestina, ambayo ni Masra (sehemu aliyopaa) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ni ardhi takatifu ya Kiislamu, iliyo barikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) ambaye anasema:

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Isra: 1]. Ardhi hii ni haramu kuipoteza hata shubiri moja yake, na lazima ikombolewe kutoka kwa uchafu wa Mayahudi.

Pili: Watawala wa Waislamu; Ima wale walio katika sare za jeshi, au wale walio katika mavazi ya kiraia, wote ni sawa katika usaliti na utumwa, na katika kuhudumia ajenda ya Magharibi mkoloni. Huduma zao ni duni kufikia kiwango cha kuuza matukufu wa Waislamu, kwa badali ya Trump kushinda muhula wa pili, kwa sababu hawana thamani yoyote, na hamu yao ni kuendelea kubakia katika viti vya serikali venye maguu mabovu.

Tatu: Nguzo mbili za wakoloni ambazo ziliteka nyara mapinduzi ya Sudan; Viongozi wa jeshi, mabwana wa ukoloni wa kisasa, ambao hupokea maagizo yao kutoka kwa Trump na Pompeo, na wanasimamiwa na ubalozi wa Amerika; Wamiliki wa nguvu halisi, wanataka watawala wa kiraia; Mabwana wa kikoloni wa zamani ambao wanapokea maagizo yao kutoka kwa Ubalozi wa Uingereza, kuwa daraja la kuvukisha ajenda ya Magharibi kafiri; Usawazishaji mahusiano, utekelezaji maagizo ya IMF, ufukarishaji watu wa nchi hii, usalimishaji mali na rasilimali kwa kampuni za Kimagharibi, na ukaushaji sheria na kanuni kutokana na hukmu zozote za kisheria. Na endapo watu wa Sudan watalalamika; Wanajeshi wanazinyakua tena hatamu za uongozi!

 

Nne: Demokrasia ambayo inajengwa juu ya kutenganisha dini na maisha, na kuchukua manufaa kama kipimo, ni moja ya madaraja muhimu zaidi ambayo ajenda ya Mkoloni kafiri Magharibi inavukishwa, ili Umma urithi udhalilifu na kujisalimisha kwa adui yake. Kwa hivyo, taarifa ya kusawazisha mahusiano inasema: "Amerika na 'Israeli' pia zimejitolea kufanya kazi pamoja na washirika wao ili kuwasaidia watu wa Sudan katika kuimarisha demokrasia yao" (Sudan Tribune).

Enyi Waislamu: Hawa watawala vibaraka wataendelea kuzikanyaga hadhi na hisia zetu, na watashirikiana na maadui zetu, na watayapuuza matukufu, ardhi, heshima, na utajiri. Na hali yetu haitarekebishwa isipokuwa kwa lile suluhisho lililofuatwa na kizazi cha kwanza cha Umma huu; Uislamu mtukufu unaotabikishwa na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) chini ya bendera ya Khilafah, ambayo inaondoa udhalilifu na kurudisha izza ya Umma, na kung'oa ushawishi wa makafiri wakoloni kutoka katika nchi za Waislamu, na kisha wale madhalimu ndipo watakapojua hatma yao.

Enyi Watu wetu wapendwa nchini Sudan: Je! Wakati haujafika kwenu kujua kwamba (serikali) ya kiraia na ya kijeshi ni pande mbili za sarafu moja; Hadhara ya kikafiri ya kimagharibi, na vipimo vya hadhara hii ni manufaa?! Na kujua kwamba Umma huu hautakombolewa isipokuwa kupitia Uislamu, kulingana na vipimo vyake vya Halali na Haramu, ambao utabikishwa na dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume?! Huu ndio mradi halisi wa mwamko, mbali na adui kafiri Magharibi, ambayo kwayo tunahamasisha nguvu za Umma kuileta madarakani, kumridhisha Mola wetu, na kutafuta maisha bora, yaliyojaa fahari, hadhi, na uongofu. Hivyo, simameni Enyi Waislamu, kumtii Mwenyezi Mungu (swt):

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].

 

H. 7 Rabi' I 1442
M. : Jumamosi, 24 Oktoba 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu