Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Ripoti ya Habari 23/10/2020

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iligawanya toleo katika mji mkuu, Khartoum, na miji mingi ya Sudan, mnamo Jumanne 13/10/2020, na toleo hilo lilikuwa na anwani: "Enyi Wateja wa Benki na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, imetosha gharama ya juu ya maisha, umasikini na udhalilifu!!"

Siku hiyo hiyo, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan - eneo la Omdurman kaskazini - ilifanya muhadhara kubwa wa umma katika eneo la Al-Thawra 17 uliopewa kichwa: "Kutiwa saini ya mwisho ya Makubaliano ya Juba, ikiagiza kuvunja kilichobakia katika Sudan." Inatekelezwa na vyombo vya habari dhidi ya watu, na mchango wa vyombo vya habari wa kupitisha njama kuu kwa manufaa ya nchi za kikafiri za Kimagharibi.

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya maandamano mbele ya Baraza la Mawaziri jijini Khartoum, mchana wa leo, Jumatano tarehe 14/10/2020, na maandamano hayo yalipewa kichwa: "Maagizo ya mfuko huo yanasababisha umaskini na kuua masikini, na wateja pekee ndio wanaoweza kuyatekeleza”, wakati ambapo wafanyikazi wa chama hiki waliinua mabango na bendera zilizoandikwa juu yake:

1. Tunaikataa serikali kibaraka inayoamiliana na IMF.

2. Serikali ya kisekula, ya kiraia pamoja na ya kijeshi ni serikali mkusanyiko.

3. Khilafah kwa njia ya Utume ndio dola pekee ya uangalizi mzuri.

4. Serikali, na sera zake zilizofeli, imeidhoofisha pauni na kuwataka masikini kulipa tofauti za bei.

5. Kuondoa usaidizi ni ukandamizaji kwa masikini na maslahi kwa maadui, ambayo inamaanisha kuwa tuna serikali ambayo ni kibaraka wa Magharibi.

6.  Miongoni mwa mambo ambayo dola inawajibishwa kuyachunga ni kuleta bidhaa na kuwaruhusu raia wake kuzimiliki, namna itakavyokuwa gharama yake.

7. Petroli ni mali ya umma, sio mali ya dola.

8. Mali ya umma ni haki ya raia wa dola kwa gharama ya ufikishaji wake kwao.

9. Kipengee sawia kati ya serikali ya Hamdok na serikali ya zamani ni: Utekelezaji wa Urasilimali – Maagizo ya Mfuko – Sera ya Mshtuko.

10. Nidhamu za Uislamu hutekelezwa na Khilafah na ndio njia pekee ya mabadiliko ya kweli.

11. Utekelezaji wa sera ya ukombozi unaunga mkono Magharibi koloni ya kikafiri.

12. Serikali ya Mpito inaendelea kusababisha umasikini na kuua masikini.

13. Janga la serikali za kitaifa ni muungano wa wakala wa kifikra na kisiasa.

14. Kile ambacho Serikali ya Mpito imefanya kwa uchumi wa nchi hii na sarafu yake ni uhalifu wa uhaini mkubwa.

15. Kupitia kuongeza bei, serikali inawalipisha masikini kwa kufeli kwake.

Mnamo siku ya Alhamisi 15/10/2020, Mashababu wa chama hiki katika eneo la Dukhainat walihutubia muhadhara mkubwa wa kisiasa saa kumi unusu alasiri katika soko la Lafah, ambapo Ustadh Abdullah Hussein, mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ilizungumza kwa anwani: "Kuondoa ruzuku juu ya mafuta ... athari na tiba."

Mnamo siku ya Ijumaa, 16/10/2020, chini ya kichwa: "Makubaliano ya Amani ni farasi wa Trojan ili kutekeleza ajenda ya kafiri Magharibi nchini Sudan," Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan – eneo la Omdurman Kaskazini - ilifanya hotuba ya kila wiki ya umma ambayo mwanachama wa Hizb ut Tahrir Mh. Muhammad Hamed alitoa hotuba.

Mnamo siku ya Jumanne 20/10/2020, Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika eneo la Khartoum Bahri waliandaa kisimamo cha kupinga huko Hajj Youssef, makutano ya barabara moja, kushutumu sera ya serikali inayotaka kuondoa ruzuku ya mafuta inayodaiwa chini ya jina la kuikomboa bei ya mafuta.

Halafu, Alhamisi, 22/10/2020, chini ya kichwa: "Matukio ya Mashariki ni hatua katika hatua za kuirarua nchi," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan- katika mji wa Gadharif, walifanya hotuba yao ya kila wiki saa kumi jioni, karibu na Hospitali ya Gadharif - Kituo cha Meno, ambapo Ustadh Maysara Yahya Mohamad Nour – mwanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilionyesha uzito wa matatizo za kikabila na matokeo yake ambayo yaliletwa kwao na kafiri Magharibi na ala zake ili kuirarua nchi.

Mashababu paza kauli mbiu na kubeba mabango yaliyo angazia mada kuu.

 Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu