Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 24/01/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 12 Rajab 1445 H sawia na 24 Januari 2024 M

Ni kwa Kuunganisha Ardhi za Waislamu kuwa Khilafah Pekee ndipo Umma wa Kiislamu Utakuwa Nguvu Kuu

Mkutano wa pili wa Pakistan, Saudia Arabia na Uturuki, chini ya bendera ya Ushirikiano wa Ulinzi wa Nchi Tatu, ulifanyika katika Makao Makuu ya Jeshi huko Rawalpindi mnamo tarehe 8 Januari 2024. Habari kama hizo zinatoa hisia kwamba nchi za Kiislamu zinaungana. Uhalisia ni kinyume chake. Manufaa halisi ya aina hii ya ushirikiano ni kwa dola za kikoloni za Magharibi, haswa Marekani. Hii inadhihirishwa na Muungano wa Kijeshi wa Kiislamu wa nchi 41 za Kiislamu. Unahamasisha malengo ya Marekani lakini unatazama uharibifu wa Waislamu wa Kashmir na Palestina bila kutaharaki kwa aina yoyote kwa ajili ya nusra. Umma wa Kiislamu unaweza tu kuwa nguvu kuu pekee kupitia kuangamiza mipaka ya kitaifa na kuunganisha rasilimali za Waislamu chini ya Khilafah moja kwa Njia ya Utume.

6 Rajab 1445 H - 18 Januari 2023 M

Jeshi la Pakistan Limehukumiwa kuwa Jeshi la Ulinzi la India katika Kanda hili?

Vikosi vya jeshi la Pakistan vimeshuka kutoka kuwa ni jeshi la saba lenye nguvu zaidi duniani, hadi nafasi ya tisa, kwa mujibu wa orodha mpya ya Global Firepower Index ya 2024. Kushuka kwa jeshi la Pakistan sio ajali. Ni matokeo ya moja kwa moja ya sera ya Marekani. Uongozi kibaraka wa Pakistan unapunguza idadi ya wanajeshi, huku ukiita saizi sahihi. Unatanguliza uchumi na kilimo, badala ya kuzingatia ubora wa kijeshi dhidi ya maadui wa Uislamu na Waislamu. Sera ya Marekani ni kwa Pakistan kuwa mlinzi mwenye silaha kwa India, ili kuilinda dhidi ya mienendo yoyote ndani ya Waislamu. Enyi makamanda wa jeshi la Pakistan! Ni wakati sasa wa kuupindua uongozi wa khiyana na kuipa Nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

7 Rajab 1445 H - 19 Januari 2023 M

Mvutano kati ya Waislamu wa Pakistan na Afghanistan Unainufaisha India na Bwana wake, Marekani

Mnamo tarehe 13 Januari 2024, wakati wa operesheni iliyofanywa na vikosi vya usalama katika eneo la jumla la Buleda, Wilaya ya Kech, magaidi walilipua Kifaa Kutengezezwa kienyeji cha Mlipuko kwenye gari la vikosi vya usalama, na kufuatiwa na makabiliano makali ya risasi. Vita kati ya Waislamu katika maeneo ya kikabila huwanufaisha tu maadui zao. Inashirikisha Jeshi la Pakistan kwenye mpaka wa Magharibi, na kuipa India uhuru kwenye mpaka wa Mashariki. Inawazuia mujahidina kuishambulia India katika Kashmir Inayokaliwa kimabavu, kama walivyofanya mara kwa mara katika historia. Kuhusu bwana wa Modi, Marekani, inaihitaji India kukabiliana na China na Waislamu wa eneo hilo. Uislamu peke yake unaweza kujenga mafungamano imara baina ya Waislamu. Uislamu pekee unaweza kuunganisha majeshi ya Pakistan na wapiganaji katika eneo la kikabila. Khilafah kwa Njia ya Utume itawalazimisha maadui kurudi nyuma.

8 Rajab 1445 H - 20 Januari 2024 M

Khilafah, Kama Sio Sasa, basi Lini?

Marekani na Uingereza, viongozi wa ukafiri, sasa wanaishambulia Yemen, huku wakiunga mkono vita dhidi ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hali katika nchi za Sudan, Pakistan, Uturuki na Libya pia zinatatizika kutokana na kuingiliwa na wakoloni. Makafiri wa Mashariki na Magharibi wameungana dhidi ya Waislamu, huku watawala wa Waislamu wakiwa ni washirika wa makafiri katika kupigana dhidi ya Umma wa Kiislamu. Suluhisho la hali hii ni Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itapindua mipango yote ya makafiri. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ikiwa sio sasa, basi lini? Ipeni Nusrah yenu Hizb ut-Tahrir iliyoko miongoni mwenu, yenye maandalizi kamili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

9 Rajab 1445 H - 21 Januari 2024 M

Isusieni Demokrasia Ambayo Inahakikisha Kuendelea kwa Mfumo wa Dunia wa Marekani

Malengo makuu ya serikali mpya baada ya uchaguzi, tayari yameamuliwa na kuidhinishwa na Marekani. Orodha hiyo inajumuisha usawazishaji mahusianao na Dola ya Kibaniani, utekelezaji wa mpango mpya wa uharibifu wa Mfadhili wa Fedha wa Kimataifa, muendelezo wa umwagaji damu kwenye mpaka wa Afghanistan, mazishi ya mwisho ya suala la Kashmir, maendeleo ya suluhisho la dola mbili kulitambua umbile la Kiyahudi na kujisalimisha kwa benki zenye riba kubwa na wakopeshaji fedha duniani. Jenerali Asim Munir amepokea maagizo yake wakati wa ziara yake ya hivi majuzi jijini Washington na sasa anayatekeleza. Enyi Waislamu! Ususieni uchaguzi wa vibaraka zaidi wa Marekani. Kuwa sehemu ya kuzalisha mfumo mpya wa dunia kupitia kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ipeni Nusrah Hizb ut-Tahrir na muuvunje mfumo wa Marekani.

10 Rajab 1445 H - 22 Januari 2024 M

Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni ni Sumu ya Kiuchumi

Rais wa Pakistan alisema mnamo 12 Januari 2024, kwamba serikali inachukua hatua kukuza Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni nchini Pakistan. Katika mfumo wa kibepari, dola za kikoloni zinaweka utawala wao juu ya nchi dhaifu na ndogo, kupitia Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni. Kupitia mpango huu, uchumi wa nchi unaimarishwa kwa muda. Hata hivyo, wawekezaji hao wa kigeni wana uwezo wa kutoa mitaji yao wakati wowote wanapotaka, na kuharibu uchumi wa nchi. Mfano ni mgogoro wa Indonesia mwaka 1997. Khilafah kwa Njia ya Utume hutoa mazingira ya kusisimua kwa wafanyibiashara wa ndani, wawekezaji na wajasiriamali, kupitia utekelezaji wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu. Inapelekea kuasisiwa kwa uchumi wa Khilafah juu ya msingi imara. Khilafah pia inalindwa kutokana na tamaa za wakoloni wa kigeni.

11 Rajab 1445 H - 23 Januari 2024 M

Mfumo wa ndani wa Kisekula Huwatayarisha Vijana wetu kwa Uchumi wa Kigeni, Sio Kujenga Uchumi Imara wa Ndani

Waziri Mkuu Msimamizi Khyber Pakhtunkhwa alisema mnamo Januari 13, 2024, kwamba serikali ya mkoa inajitahidi kuhakikisha ajira katika nchi mbalimbali za kigeni kwa kutoa ujuzi na mafunzo kwa vijana 500,000. Katika zama za Khilafah, vyuo vikuu bora zaidi duniani vilikuwa katika Ulimwengu wa Kiislamu. Watu kutoka pande zote za dunia walikuwa wakija katika Khilafah kwa ajili ya elimu. Hata hivyo, baada ya kuvunjwa Khilafah na kutabikishwa kwa mfumo wa kisekula, Ulimwengu wa Kiislamu ulipoteza uongozi wake. Maendeleo ya jamii hayatatokea kwa kupoteza vijana wetu kwa uchumi wa nje. Kwa kuutabikisha Uislamu ndani ya nchi, Khilafah kwa Njia ya Utume itaendeleza kikamilifu elimu, utafiti, kilimo na viwanda imara ndani ya nchi.

12 Rajab 1445 H - 24 Januari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu