Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 17/01/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 05 Rajab 1445 H sawia na 17 Januari 2024 M

Ndege za Kivita za Jeshi la Anga la Pakistan Zinahitajika katika Anga ya Tel Aviv, Sio kwa ajili ya Sherehe na Maonyesho ya Angani

Mnamo tarehe 2 Januari 2024, mkuu wa jeshi la Pakistan alihudhuria Sherehe ya Uanzishaji na Uperesheni katika kambi ya operesheni cha Jeshi la Anga la Pakistan. Kufuatia hafla hiyo, onyesho la anga lilifanyika. Hii ni wakati ambapo walipuaji wa umbile la Mayahudi wanazika wanawake na watoto wetu chini ya nyumba zao huko Gaza. Hakika, vikosi vya jeshi vinahitaji uongozi wa kisiasa wa Kiislamu. Ni uongozi huo ndio utakaohakikisha kufunguliwa kwa kambi za anga za Misri, Syria, Jordan na Lebanon kwa ajili ya ndege za kivita za Ummah. Ni uongozi huo ndio ambao utahakikisha kuangamizwa kwa umbile katili la Mayahudi ndani ya masaa machache. Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir, ili mutafute ushindi chini ya uongozi wa Khilafah kwa Njia ya Utume.

29 Jumada al-Akhir 1445 H - 11 Januari 2023 M

Mipaka ya Kitaifa ndio Chanzo cha Uhasama baina ya Waislamu

Msaidizi mkuu wa Kiongozi Mkuu wa Taliban ya Afghanistan alifanya mazungumzo na maafisa wa Pakistan mnamo tarehe 4 Januari 2024, huku kukiwa na uhasama unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili kuhusu “ugaidi wa mipakani.” Uhasama unaibuka kati ya Pakistan na Afghanistan, wakati mwingine juu ya mapigano na wakati mwingine juu ya usafirishaji wa bidhaa na watu kuvuka mpakani. Suluhisho pekee la tatizo hili ni kufuta mipaka ya kitaifa na kuunganisha maeneo haya mawili kupitia kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Kwa njia hii Waislamu wa eneo hilo wanaweza kuunganisha na kutatua matatizo yao kwa msingi wa Uislamu. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ,

[فَاِنۡ تَنَازَعۡتُمۡ فِىۡ شَىۡءٍ فَرُدُّوۡهُ اِلَى اللّٰهِ وَالرَّسُوۡلِ اِنۡ كُنۡتُمۡ تُؤۡمِنُوۡنَ بِاللّٰهِ وَالۡيَوۡمِ الۡاٰخِرِ‌]

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” [Surah An-Nisa 4:59]

30 Jumada al-Akhir 1445 H - 12 Januari 2023 M

Hekima Jumla ya Bunge Haina Thamani Mbele ya Mwongozo wa Mwenyezi Mungu

Wakati wa kesi mnamo tarehe 4 Januari 2024, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Upeo ya Pakistan alisema kwamba hekima ya pamoja ya majaji walioketi kwenye benchi haiwezi kuwa kubwa kuliko ile ya wabunge. Hii inatokana na fahamu potofu ya Kimagharibi. Kwa hakika, elimu jumla ya viumbe vyote kwa pamoja haina thamani mbele ya Hekima ya Mwenyezi Mungu ﷻ ambaye amesema,

[وَعَسٰۤى اَنۡ تَكۡرَهُوۡا شَيۡـًٔـا وَّهُوَ خَيۡرٌ لَّـکُمۡ‌ۚ وَعَسٰۤى اَنۡ تُحِبُّوۡا شَيۡـًٔـا وَّهُوَ شَرٌّ لَّـكُمۡؕ وَاللّٰهُ يَعۡلَمُ وَاَنۡتُمۡ لَا تَعۡلَمُوۡنَ]

“Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Surah Al-Baqarah 2:216]. Katika Khilafah (Caliphate) kwa Njia ya Utume, Khalifa hufanya maamuzi kwa mujibu wa Wahyi wa Mwenyezi Mungu ﷻ pekee.

01 Rajab 1445 H - 13 Januari 2024 M

Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan vinawajibika kwa Ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa Kimabavu

Waziri Mkuu wa Muda alisema mnamo tarehe 5 Januari 2024 kwamba jamii ya kimataifa ina wajibu kwa watu wa Kashmir inayokaliwa kimabavu, ili watekeleze haki yao ya kujitawala. Hata hivyo, ni jamii ya kimataifa, inayoongozwa na Marekani, ambayo inaruhusu India na umbile la Mayahudi kunyakua haki za Waislamu. Watawala wa Waislamu wamejitia upofu na uziwi kwa jinai hizo. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ,

[صُمُّۢ بُكۡمٌ عُمۡیࣱ فَهُمۡ لَا یَعۡقِلُونَ]

“ni viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo hawaelewi.” [Surah Al-Baqarah 2:171]. Ni wajibu wa vikosi vya jeshi la Pakistan kuwakomboa Waislamu wa Kashmir inayokaliwa kwa mabavu kutoka kwa dola dhalimu ya Kibaniani. Ili kufikia hilo vikosi vya jeshi lazima viuondoe uongozi wa khiyana, na kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

02 Rajab 1445 H - 14 Januari 2024 M

Ubepari ni Hatari kwa Deni

Benki ya Kuu ya Pakistan ilisema mnamo tarehe 5 Januari, 2024 kwamba deni la ndani la serikali ya federali liliongezeka hadi Rupia bilioni 40,955 mnamo Novemba 2023. Ni ongezeko la Rupia 7,985 bilioni ndani ya mwaka mmoja. Deni la serikali ya Marekani litafikia dolari bilioni 33,176 mwaka wa 2023. Ni ongezeko la dolari bilioni 2,248 kwa mwaka mmoja. Chini ya uhuru wa umiliki, ubepari hukabidhi rasilimali nyingi za madini za umma kwa sekta binafsi, huku sekta ya kibinafsi ikitawala viwanda. Serikali inalazimika kukopa. Uislamu unatangaza rasilimali kubwa za madini kuwa mali ya umma ambayo inasimamiwa na serikali. Inahakikisha serikali inajihusisha na viwanda vizito. Hivyo serikali ina rasilimali za kutosha zinazopatikana kwa matumizi yake, bila kuchukua mikopo. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume ndiyo itaiokoa Pakistan kutokana na deni kubwa.

03 Rajab 1445 H - 15 Januari 2024 M

Kujaribu Kuifurahisha Marekani Hakuna Maana

Mnamo tarehe 4 Januari 2024, Marekani iliiongeza Pakistan kwenye orodha yake ya “nchi zenye kutiliwa wasiwasi sana,” pamoja na nchi nyingine kumi na moja zilizohusika katika “ukiukaji mkubwa wa uhuru wa kidini.” Afisi ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilipinga vikali hatua hiyo mnamo tarehe 8 Januari 2024. Marekani haijaijumuisha Dola ya Kibaniani katika orodha hiyo. Nchini India watu wote wasio Mabaniani, wakiwemo Waislamu, wanafanyiwa ukatili mbaya zaidi unaofadhiliwa na serikali. Licha ya unafiki huu, watawala wa Pakistan wanadhani kwamba ni katika maslahi ya Pakistan kuiunga mkono Marekani. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ,

[قَدۡ بَدَتِ الۡبَغۡضَآءُ مِنۡ اَفۡوٰهِهِمۡ ۖۚ وَمَا تُخۡفِىۡ صُدُوۡرُهُمۡ اَكۡبَرُ‌ؕ]

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [ Surah Aal e Imran, 3:118]. Khilafah ijayo kwa Njia ya Utume itafichua unafiki wa Marekani kwa ulimwengu, hivi punde kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ﷻ.

04 Rajab 1445 H - 16 Januari 2024 M

Hizb ut Tahrir iko Tayari Kubeba Mzigo wa Mabadiliko

Hizb ut Tahrir ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa katika Ulimwengu wa Kiislamu. Mradi wake ni kung'oa uingiliaji kati muovu, ukaliaji kimabavu na ushawishi wa ukoloni kutoka kwa ardhi zote za Waislamu, ikiwemo Pakistan. Hizb ut Tahrir inatafuta Nusrah kutoka kwa majeshi ya Ummah ili kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah itang'oa muundo mzima wa wakoloni makafiri kutoka Pakistan, iwe ni afisi za ubalozi zao au kambi zao. Itang'oa sera zao haribifu za kielimu, kiutamaduni na kiuchumi, ambazo kupitia kwazo wanaingilia kati mambo yetu. Khilafah itang'oa uongozi wa wakala juu ya majeshi ya Ummah, ambao unaiwezesha Marekani kutumia askari wetu kama mamluki. Khilafah itakusanya majeshi yetu katika kutafuta ushindi au kufa kishahidi ili kuyalinda matukufu ya Umma wa Kiislamu.

05 Rajab 1445 AH - 17 Januari 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu