Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 31/01/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 19 Rajab 1445 H sawia na 31 Januari 2024 M

Kuunganishwa kwa Pakistan na Nchi za Ghuba Kutaifanya Khilafah Kujitosheleza

Vyanzo vya Wizara ya Fedha vilisema mnamo tarehe 16 Januari 2024 kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu unatarajiwa kuikopesha Pakistan dolari bilioni 2 kwa mwaka mmoja. Licha ya kuwa na nguvu ya nyuklia na jeshi la saba kwa ukubwa duniani, Pakistan inalazimika kukopa kwa malipo ya nje. Kulingana na Global SWF, jumla ya mali ya hazina saba za utajiri huru za kambi ya mataifa sita ya Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC) ni dolari bilioni 3,690. Hata hivyo, nchi hizi za Ghuba haziwezi kujilinda. Zinahakikisha usalama wao kwa kutoa kambi za kijeshi kwa dola za kikoloni. Kuziunganisha dola za Kiislamu, kunaunganisha nguvu zao na kuondoa udhaifu wao. Khilafah kwa Njia ya Utume itauimarisha Ummah na kukomesha utegemezi wake wa ukoloni.

13 Rajab 1445 H - 25 Januari 2023 M

Hebu Makombora ya Pakistan na Iran sasa na Yainyeshee Tel Aviv

Baada ya mashambulizi ya droni na makombora ya Iran katika wilaya ya Panjgur ya Pakistan, Pakistan pia ilifanya mashambulizi katika eneo la Sistan nchini Iran. Mashambulizi ya kujibu yanathibitisha kwamba upotofu wa fahamu ya dola ya kitaifa ndiyo sababu halisi ya mgawanyiko, na matokeo ya udhaifu, wa nguvu za Waislamu. Kwa hivyo, Iran iliipiga Syria, Iraq na Pakistan baada ya kuuawa shahidi Waislamu katika mji wa Kirman wa Iran, na kisha Pakistan ikapiga Iran. Hata hivyo, kuuawa shahidi kwa Waislamu 24,000 huko Gaza na Ukingo wa Magharibi hakutoshi kuwakusanya wanajeshi waumini wa Iran na Pakistan ili kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa na Al-Masjid Al-Aqsa. Hakika ni upotofu kuyapa thamani zaidi maeneo ya dola ya kitaifa, kwa msingi wa utaifa, kuliko matukufu ya Uislamu, kwa msingi wa maamrisho ya Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume wake ﷺ.

14 Rajab 1445 H - 26 Januari 2023 M

Dola ya Kitaifa ni Sanamu ya Batili la Uongozi wa Kijeshi na Kisiasa wa Pakistan

Masaa machache baada ya kuuawa kwa watoto wa Panjgur, katika jimbo la Balochistan, Pakistan ilimfukuza balozi wa Iran. Vikosi vya kijeshi vya Pakistan viliwekwa katika tahadhari nyekundu na kuhamasishwa kwa ajili ya operesheni ya "Marg Bar Sarmachar" (Kifo kwa Waasi). Hapo awali, mnamo Februari 2019, kwa kukabiliana na mashambulizi ya angani ya Dola ya Kibaniani huko Balakot, vikosi vya jeshi vya Pakistan vilikusanywa ndani ya masaa machache, na kujibu kwa jibu la nguvu na la kuvunja taya. Hata hivyo, Mayahudi wa Kizayuni wanaiangamiza Gaza, huku wakifanya uhalifu ambao hata wanyama porini wangeweza kuukwepa. Hata hivyo, siku 100 zimepita na uongozi wa kijeshi haujajibu kilio cha Waislamu wa Gaza, kwa operesheni ya "Kifo kwa Uvamizi wa Kizayuni". Hakuna wokovu kwa Waislamu bila ya kuuzika uovu wa dola hii ya kitaifa, ambayo itazikwa tu kwa kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.

15 Rajab 1445 H - 27 Januari 2024 M

Kujisalimisha kwa Watawala kwa Dola ya Kitaifa ndio Udhaifu Wetu

Mashambulizi ya hivi majuzi ya Iran yalithibitisha kwamba maombi kuhusu kudhoofisha uchumi, "matatizo mazito ya usalama wa ndani na kisiasa" ya Pakistan na hofu ya vikwazo vya kimataifa ni visingizio tu vya kusikitisha. Kuchafuliwa kwa sanamu la serikali la dola ya kitaifa hakukubaliki, isipokuwa wakati bwana wa Marekani anapokiuka mistari mekundu ya dola ya kitaifa. Washington yenyewe ni kibla cha usalama cha uongozi wa kisiasa na kijeshi. Walakini, nje ya unajisi wa sanamu hili, hakuna risasi inayofyatuliwa, wala uhusiano wa kidiplomasia haukatiwi kwa kumfukuza balozi. Hakuna kinachofanyika ikiwa Kitabu kilichoteremshwa cha Mola wa Wanaadamu wote, Quran Tukufu, kitachomwa moto, au kuna jaribio la kuvunja utakatifu wa kipenzi chetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, au ikiwa Waislamu watauawa shahidi katika mji baada ya mji, kwa miezi, au hata miaka.

16 Rajab 1445 H - 28 Januari 2024 M

Ujenzi wa Hekalu la Ram kwenye Magofu ya Babri Masjid

Damu na utakatifu wa Waislamu umefanywa kuwa dhihaka, kutokana na kutokuwa na aibu ya ugumba wa watawala wa Pakistan. Baada ya wafuasi wa itikadi kali za Kibaniani kuuvunja msikiti mmoja wenye umri wa miaka 500 kwa jina la Hindutva, sasa wanajenga hekalu juu ya magofu hayo. Mahakama ya India inaidhinisha maamuzi ya watu wenye msimamo mkali. Mashambulizi dhidi ya Waislamu yanazidi kuongezeka. Umma wa Kiislamu unatazamia majeshi yenye nguvu ya Pakistan kwa ajili ya kuinusuru Dini. Hata hivyo, uongozi wa kijeshi na kisiasa haujali suala hilo. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Uondoeni uongozi unaokuzuieni kuwanusuru Waislamu wa Gaza, Kashmir na India. Toeni Nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ili kuufanya Uislamu kutawala tena katika Bara Dogo la India, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi kabla.

17 Rajab 1445 H - 29 Januari 2024 M

Kunyamazia juu ya Ukatili mjini Gaza ni Chanzo cha Aibu

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Sifa yenu imechafuliwa machoni pa Waislamu. Kulia mithili ya wanawake majumbani mwao kwa matukio yenye uchungu ya Gaza, kumedhoofisha cheo chenu machoni pa adui zenu. Umma wa Kiislamu, wakiwemo Waislamu wa Pakistan, wana kila haki ya kukuulizeni, "uko wapi ushujaa wenu, heshima na roho ya Kiislamu"? Mwenyezi Mungu (swt) wala Waumini hawakubali udhuru wenu kwamba “hatukupata amri.” Msiruhusu utiifu wenu wa vibaraka wasaliti wa Marekani ukuongozeni kwenye kuteketezwa katika moto wa Jahannam pamoja nao. Hata hivyo, uongozi wa Waislamu ni laini kama hariri kwa makafiri, lakini unazungumza na Waislamu kwa lugha ya moto na baruti. Uislamu unawajibisha kupigana Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu ﷻ ili kuzikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, hivyo waondoe wasaliti hawa wanaosimama katika njia yenu.

18 Rajab 1445 H - 30 Januari 2024 M

Ukosefu wa Ruwaza Husababisha Ukuaji Mdogo. Ruwaza Kubwa Huongoza kwenye Mwamko

Mkuu wa jeshi la Pakistan alisema mnamo 16 Januari 2024 kwamba njia ya maendeleo ya kitaifa imedhamiriwa na sekta za ndani kama vile Viwanda vya Silaha vya Pakistan. Maendeleo yoyote ambayo Pakistan imefanya katika uimarishaji viwanda, haswa katika sekta ya ulinzi, ni kwa sababu ya hamu ya kushinda nguvu ya dola ya Kibaniani. Ikiwa kutokana na ruwaza hii ndogo, Pakistan ilipata teknolojia ya nyuklia na makombora, basi Pakistan inaweza kuimarika kiasi gani ikiwa itatabanni ruwaza ya kumaliza mfumo wa sasa wa kilimwengu wa kikafiri na kuufanya mfumo wa kilimwengu wa Uislamu kutawala. Waarabu walipoutabanni mfumo wa Uislamu, wachungaji wa kondoo, mbuzi na ngamia majangwani walienea hadi mabara matatu, na wakawa ndio dola kuu ya kilimwengu. Kusimamishwa tena kwa Khilafah kwa Njia ya Utume ndiko kutakakoturudisha kwenye nafasi hii.

19 Rajab 1445 AH - 31 January 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu