Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Gazeti la Mageuzi ya Kimsingi [Koklu Degisim]

Kifo cha Kishahidi cha Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Chini ya Mikono ya Wavamizi wa Urusi Katika Crimea!

(Imetafsiriwa)

Vikosi kutoka idara ya Huduma za Usalama ya Taifa ya kitengo Maalum cha Huduma cha Urusi vimevamia nyumba ya Ndugu Nabi Rahimov na kisha kumuuwa, kwa madai ya kukataa kukamatwa.

Mke wake, Sahba Burhanova, na watoto wawili, Maryam na Taqiud-Din, watafukuzwa nchini.

Wanasheria kutoka Crimea wamesema kuwa vikosi vya Huduma za Usalama vimevamia nyumba ya Rahimov mnamo tarehe 12/5/2021 saa 12 asubuhi. Rahimov mwanzo aliteswa na kisha kuuliwa. Wakati idara ya Taifa ya huduma za Usalama ikijaribu kufunika uovu huo chini ya kisingizio cha kupinga kukamatwa.

   
   

Wavamizi wa Urusi hawakuridhika na mauwaji ya Rahimov na madai ambayo hakuna mwenye akili anaeyakubali. Wavamizi wa Urusi wametaka Sahba Burhanova afukuzwe nchini. Mahakama katika eneo lililoshikiliwa la Sovetsky imeamuru kumuweka katika kituo cha muda cha kumshikilia kabla ya kuhamishiwa Uzbekistan.

Urusi imekuwa ikiweka mbinyo kwa Waislamu chini ya kisingizio cha kupambana na ugaidi tokea mwaka 2014. Mahakama za Urusi zimewafunga wa-Tatar katika Crimea hadi miongo kadhaa kutokana na uvamizi kinyume na sheria wa idara ya Taifa ya Usalama ya Urusi. Waislamu wakikumbana na hali ya dhulma ya Urusi chini ya kisingizio cha ugaidi bila hata kupata hata silaha moja.

Waislamu wanashikiliwa kwa madai ya ugaidi na siasa kali; wanafungwa jela, na kuwekwa kwenye kifungo cha upweke na mateso ya njaa kwa sababu utawala wa magereza unawapa nguruwe ili wale.

Kituo cha Haki za Binaadamu cha Memorial kimechapisha kwenye mtandao wake ripoti ya watu walioshikiliwa 297. Ripoti inaeleza kuwa  katika idadi hiyo takriban wote ni Waislamu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wengi ya takriban washikiliwa 191 ni wanachama wa Hizb ut Tahrir. Inaeleza kuwa ripoti hii haijakamilika na ni fupi, kwa vile majina katika ripoti ni ya watu ambao kesi zao zinaweza kuchunguzwa, na kuwa majina yaliofikiwa na Kituo cha Haki za Binaadamu cha Memorial ni kiasi cha mara tatu au nne ya majina ya ripoti. Sababu ikiwa ni kuwa faili hazina taarifa za kutosha au hazijakamilika.

Inatajwa katika ripoti kuwa Urusi inaishutumu Hizb ut Tahrir kuwa ni taasisi ya kigaidi na inawashutumu wanachama wa Hizb ut Tahrir kuwa ni magaidi bila kuwa na msingi wa kisharia.

Kwa kuongezea na uelewa wao wa matumizi ya sheria na uwepo wa utiliaji nguvu juu ya sheria hiyo. Kwa mujibu wa kifungu kipya, “kuandaa na kushiriki katika tukio la chama cha kigaidi”. Wanachama wa Hizb ut Tahrir wanashitakiwa kwa mujibu wa kifungu hiki kipya. Wanaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha maisha.

Mahakama zinaweza kutoa vifungo vya hadi miaka 24 jela.

Japokuwa kuishutumu Hizb ut Tahrir ni kubadilisha ukweli, kwa kuwa wote wa karibu na wa mbali wanajua kuwa Hizb ut Tahrir wanafuata mapambano ya kifikra, hoja na dalili, na kuwa Hizb ut Tahrir haitoiacha njia hii. Hii iko wazi katika fikra zake, thaqafa na harakati zake za kisiasa inazozitekeleza katika sehemu nyingi duniani. Licha ya ukweli wote huo, wanachama wa Hizb ut Tahrir bado wanabanwa ndani ya kesi za uongo na mashtaka ya kuzushwa.

Hizb ut Tahrir sio chama cha kigaidi, na madai yote yanayoelekezwa dhidi yake ni uongo wa wazi na uzushi. Kwa kuangalia historia ya Hizb ut Tahrir tokea mwaka 1953 hadi leo, inaonyesha kuwezekana kuukanusha uongo huo kirahisi.

Kwa kuzidisha makali ya sheria dhidi ya Waislamu, ukamataji ulioenea umefanyika katika Tatastan, Bashkortostan, Moscow, Petersburg, Chelyabinsk, Tyumen na majimbo mengine. Na baada ya uvamizi wa Crimea, Waislamu walishikiliwa pia katika Crimea. Suala halikusita kwa vikosi vya uvamizi kwenye uzuiaji wa utendaji kazi wa mahakama  na kuwafunga Waislamu katika hali ya kinyama, lakini pia walianza kuzua madai ya uongo hata katika upangaji wa haki za jinai. Haya ni baadhi ya matukio ya mateso hayo:

Mirzaparot Mirzasharibov alifungwa hadi miaka 5 jela katika Saint Petersburg kwa kuwa kwake Hizb ut Tahrir. Alipofungwa mnamo 21/3/2019, alipigwa kikatili na wanaharakati. Mirzaparot alipoingia kwenye chumba cha gereza “Russian Prison Execution”, afisa alimuelekezea kisu shingoni. Kisha afisa mwengine alie pamoja nae alianza kumuuliza masuali kuhusu Hizb ut Tahrir.

Mirzaparot aliyajibu masuali ya afisa na kuwaambia kuhusu kazi za chama. Alishadidia kuwa alikuwa akitekeleza mafunzo ya uchunguzi wa kifikra, na hajachukua hatua za kivitendo. Mirzaparot alifungwa tena jela hadi miaka 3 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 5, ambapo miaka 2 alitumikia kwenye vyumba vya jela na mwaka 1 katika gereza lenye ulinzi mkali. 

Galolin Rinat alikuwa ni mkaazi wa Chelyabinsk. Kwa sababu ya uanachama wake wa Hizb ut Tahrir, alifungwa hadi miaka 5 katika jela yenye ulinzi mkali. Siku alipoachiwa, aliwekwa rumande kwa mashtaka mapya, na hakuruhusiwa kutoka jela. Alifungwa hadi miaka 8 ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa uongo.

Rahman Hakayef Dhikr Allah alifungwa miaka 7 jela mjini Moscow kwa uanachama wake katika Hizb ut Tahrir. Baada ya kutumikia kifungo chake, walimshutumu kurejea tena kulingania Uislamu, alifungwa miaka 14 na nusu mnamo tarehe 13/12/2018. Kwa hivyo, Dhikr Allah alifungwa tena miaka 7 kwa kufanya kazi na Hizb ut Tahrir, kisha alifungwa tena kwa mashtaka sawa lakini kwa lugha mpya na kwa kifungo mara mbili yake.

Mnamo Januari 2021, Usmanov Zakher John, anayeishi Kazan, vilevile alifungwa kama hivyo. Mnamo 2017, alifungwa miaka 6 jela. Kwenye mwezi Oktoba 2020, Mahakama ya Kijeshi ya Mwanzo ya Mashariki ilimfunga miaka mingine 9. Alitakiwa kutumikia miaka mitano kati ya minane katika vyumba vya gereza.

Asghat Hafezov alifungwa miaka 17 na nusu mnamo Disemba 2017. Waliongeza kile kinachoitwa harakati za “kigaidi” alizoteuliwa kutekeleza (Kifungu 205/5-1 cha Sheria ya Jinai) na ibara ya siasa kali (Kifungu 282/2-1 cha Sheria ya Jinai) kwa kushiriki katika kinachoitwa harakati za “kigaidi” (Kifungu 205/5-2 cha Sheria ya Jinai).

Levi Panmarayov, mwanaharakati wa haki za binaadamu na mwenye ushawishi katika Urusi, amesema: ni vigumu kubakia kimya kuhusiana na unyama wa utawala. Levi Panmarayov amesema katika kongamano lililotayarishwa na Kituo cha Ukumbusho cha Kimataifa: “Waislamu wa Hizb ut Tahrir wanashutumiwa kutekeleza au kuandaa vitendo vya kigaidi. Hakuna mashtaka kama hayo, hakuna maamuzi ya kisheria. Wamefungwa hadi miaka 24, miaka 20 na 18 jela. Tunahitaji kulizungumzia hili kila pembe…

Kuna kesi zinazoendelea kila kukicha, na watu wanaendelea kufungwa. Wameshafikia mamia ya watu hadi sasa. Baadhi yao wamepata kifungo kwa mara ya pili. Kwa maoni yangu, huu ni ufashisti wa wazi.”

Chanzo: https://kokludegisim.net/haberler/rus_isgalci_kirimda_hizb_ut_tahrirli_genci_sehit_etti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu