Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Masuali 3 kwa Majeshi ya Waislamu Kutoka kwa Vijana wa Kiislamu wa Magharibi

(Imetafsiriwa)

Sisi, vijana wa Kiislamu wa Magharibi, tumefanya kila kitu ndani ya uwezo wetu kuzuia uvamizi. Utawaona maelfu ya vijana wa Kiislamu wakilaani, kuandamana, wakitumia majukwaa yao ya mitandao ya kijamii, hata kufikia kufukuzwa mashuleni kwa msimamo wao wa kutoomba radhi.

Sisi, vijana wa Kiislamu wa Magharibi, tunataka kuweka wazi kuwa tunapinga usitishaji wowote wa mapigano na umbile hili la Kiyahudi lililo na madhara. Hakuna usitishaji wa mapigano na umbile hili ovu ambalo halikuuletea Ummah huu isipokuwa balaa kwa zaidi ya miaka 70. Usitishaji utafanyika tu baada ya umbile hili dhalimu kufutwa na kuwekwa bendera ya Uislamu. Sio kupitia kwa Waislamu waliozingirwa wa Gaza, wanaojihami kwa maroketi wala kwa Waislamu waliokaliwa kimabavu katika Ukingo wa Magharibi, wanaojihami kwa mawe, kuweza kuzikomboa ardhi takatifu. Wajibu unawaangukia wale wenye uwezo wa kupigana na majeshi, kama majeshi ya Waislamu wa Uturuki, Misri, Sudan, Tunisia, Pakistan, Bangaldesh na Indonesia.

Enyi Majeshi ya Waislamu! Ndugu zenu na dada zenu wa Magharibi wana maswali 3 kwenu:

1. Je, mna nyoyo za mawe?

Nyoyo zenu hazipati maumivu kwa ajili ya ndugu yenu aliyewaangalia mabinti zake wawili machoni, akiwadanganya kwa kuwaahidi watakuwa sawa, (haya yote) kutokana na makombora ya kuangamiza ya Mazayuni?

Nyoyo zenu hazichuriziki damu kwa ajili ya dada yenu ambaye matumaini yake na ndoto zake za baadaye zikizikwa ndani ya vifusi pamoja na mtoto wake aliye tumboni?

Nyoyo zenu hazivunjiki kwa ajili ya wavulana na mabinti zetu wakikimbia kujiliwaza kwenye mikono ya mama zao ikiangamizwa kiungo baada ya kiungo?

Au mmekaa ndani ya kambi zenu na nyoyo za mawe?

Enyi Majeshi ya Waislamu! Hamna ‘Izzah (utukufu) kwa Mola wetu, Kiongozi wetu, RasulAllah (saw)?

Haukuwa Msikiti wa Al-Aqsa ambao Yeye (saw) aliongoza Mitume (ahs) katika Swalah?

Vipi mnavumilia kiburi na majivuno yao wakati Mitume (ahs) wakisimama kwa Khushuu’ (unyenyekevu)?

Vipi mnawaruhusu kuitikisa ardhi wakati nyoyo za Mitume zikitingishika kutokana na kisomo chake (saw)?

Vipi mnaruhusu viatu vyao vichafu kukanyaga mahala ambapo uso Wake Mtukufu (saw) ulisujudu?! Chukizo la aibu mno linatokea kwenye utazamaji wenu!

Au mmezama kiasi cha kukosa ambacho kimewafanya kuwa kama maadui zetu na maadui zenu ambao nyoyo zao zimekuwa ngumu kuliko mawe?

 [ثُمَّ قَسَتْ قُلُوبُكُم مِّن بَعْدِ ذَلِكَ فَهِيَ كَالْحِجَارَةِ أَوْ أَشَدُّ قَسْوَةً وَإِنَّ مِنَ الْحِجَارَةِ لَمَا يَتَفَجَّرُ مِنْهُ الأَنْهَارُ وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَشَّقَّقُ فَيَخْرُجُ مِنْهُ الْمَاء وَإِنَّ مِنْهَا لَمَا يَهْبِطُ مِنْ خَشْيَةِ اللّهِ وَمَا اللّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ]

Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi, kwani kuna mawe yanayochimbuka mito, na kuna mengine yanayopasuka yakatoka maji ndani yake, na kuna mengine huanguka kwa sababu ya khofu ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyafanya.” [Al Baqarah:74]

2. Je, mmevunja ahadi yenu na Mwenyezi Mungu (swt)?

Enyi Majeshi ya Waislamu! Mlipojiunga na Uaskari wa Ummah huu mtukufu, mliungana na urithi wa miaka 1400 iliopita wa Mujahidiin kutokea wakati wa Masahaba (rah) na utaratibu huo utaendelea hadi siku ya hukumu. Mmeweka ahadi na Mwenyezi Mungu (swt) kuitumikia Dini Yake, na sio kuhudumia mipaka ya kitaifa iliochorwa na makafiri wakoloni. Mmeweka ahadi kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na sio kuwatii watawala wenu walio watiifu wa fikra za kijinga jinga. Mumeweka ahadi, enyi Majeshi ya Kiislamu, kuulinda Ummah!

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia…” [Al Anfal: 72]

Hamuhisi aibu kuwa Ummah umeweka matumaini kwenu?

Hamuhisi aibu kuwa wanawake wanapigana badala yenu?

Hamuhisi aibu kuwa Mola wenu amekuulizeni nyinyi zaidi ya mara moja:

“Nini kinakusibuni?”

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanaoonewa, wanaume, wanawake na watotot, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anye toka kwako.” [An-Nisa:75]

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]

“Enyi Mlioamini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu mnajitia uzito katika ardhi? Je mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Tawbah:38]

Mnang'ang'ania ardhi yenu (iliochorwa) ya kikoloni, hata hamvuki mipaka hiyo linapokuja suala la kuuliwa kwa wingi ndugu zenu wa kike na kiume? Je, huu ni urithi mnaotaka kuwaachia watoto wenu na watoto wao? Je, hamna uoni kwa ajili ya Uislamu?

Enyi majeshi ya Waislamu! Kama hamtazivunja pingu hizi ambazo zimeweka udhalilifu na fedheha juu ya Ummah huu basi mtafikwa na adhabu kali na mtabadilishwa badala yenu kwa watu wengine walio bora.

إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلاَ تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿

 “Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [TMQ At-Tawbah: 39]

Enyi majeshi ya Waislamu! Msiivuje ahadi yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt)! Msiwe kama maadui zetu na maadui zenu!

[وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَاقَكُمْ وَرَفَعْنَا فَوْقَكُمُ الطُّورَ خُذُواْ مَا آتَيْنَاكُم بِقُوَّةٍ وَاسْمَعُواْ قَالُواْ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَأُشْرِبُواْ فِي قُلُوبِهِمُ الْعِجْلَ بِكُفْرِهِمْ قُلْ بِئْسَمَا يَأْمُرُكُمْ بِهِ إِيمَانُكُمْ إِن كُنتُمْ مُّؤْمِنِينَ]

“Na tulipochukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni). Kamateni kwa nguvu haya tuliyokupeni na sikieni, wakasema tumesikia na tumekataa! Na wakanyweshwa nyoyoni mwao (imani ya) ndama kwa kufuru yao. Sema ni uovu mno iliyokuamrisheni imani yenu ikiwa ni wenye kuamini.” [TMQ Al-Baqarah:93]

3. Hivyo nyinyi mnatilia shaka ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw)?

Hayo mawe yanayorushwa, yakipigana badala yenu dhidi ya maadui wenu, karibuni yatawadhihirikia. ‘Abdulla bin Umar (ra) amepokea: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema, “Mayahudi watapigana na nyinyi, na mtapata ushindi dhidi yao ambapo jiwe litasema, ‘Ewe Muislamu! Kuna Yahudi nyuma yangu; muuwe!” (Sahih al Bukhari). Umbile la Kiyahudi karibuni litaangamizwa na mahala pake patakuwa Mji Mkuu wa Khilafah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: Suala hili (Khilafah) litakuwa baada yangu katika Madinah, kisha Al-Sham, kisha Jazira, kisha Iraq, kisha katika Madinah, kisha katika Bayt ul-Maqdis. Itakapokuwa katika Baytul Maqdis, basi hapo ni nyumbani kwake, na hakuna watu watakaoweza kuiondosha, hivyo itarejeshwa kwao moja kwa moja.” (Ibn Asakir, Tarikh Dimashiq 368)

Enyi majeshi ya Waislamu! Msiwe kama maadui zetu na maadui zenu wanaoshuku ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).

[يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الأَرْضَ المُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللّهُ لَكُمْ وَلاَ تَرْتَدُّوا عَلَى أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ * قَالُوا يَا مُوسَى إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىَ يَخْرُجُواْ مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُواْ مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ * قَالَ رَجُلاَنِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُواْ عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ وَعَلَى اللّهِ فَتَوَكَّلُواْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ * قَالُواْ يَا مُوسَى إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُواْ فِيهَا فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ]

"Enyi watu wangu ingieni katika nchi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika. Wakasema: ewe Musa! Huko wako watu majabari . nasi hatutaingia huko mpaka wao watoke humo. Wakitoka humo hapo tutaingia. Watu wawili miongoni mwa wachamngu ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, walisema: Waingilieni kwa mlangoni. Mtakapo waingilia basi kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. Wakasema: Ewe Musa! Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi tutakaa hapa hapa."  [TMQ Al-Maidah: 21-24]

Enyi majeshi ya Waislamu, tunakuulizeni masuala haya 3 mepesi, je, kuna yeyote ataejibu? Hatuhitaji kuyasikia majibu yenu, enyi majeshi ya Waislamu! Tunahitaji kuyaona majibu yenu.

#Aqsa_calls_armies                                                                              
  #AqsaCallsArmies
 #OrdularAksaya  #الأقصى_يستصرخ_الجيوش
 #AqsaYawaitaMajeshi

      Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Syed Fahad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu