Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muda wa Kuufikiria Upya Urasilimali

Kutokana na hali ya sasa ya Covid-19, inaonekana kuna mkazo mkubwa juu ya kuhifadhi uchumi kuliko kuhifadhi maisha, ambapo Hazina ya Taifa kwa sasa inajaza matrilioni ya dolari ili kuhakikisha uchumi unabakia laini. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa uchumi wa dunia umekuwa katika hali ngumu kabla ya kuzuka Covid-19. Virusi hivi sio sababu ya kushuka kwa uchumi, bali ni kichocheo, lakini inaelekea kuwa serikali zinakusudia kuweka lawama kwenye virusi kuliko kwenye ulegelege wa uchumi uliokuwepo kabla. Jambo msingi la kulengwa lilikuwa liwe ni juu ya utatuzi wa mgogoro wa Covid-19, kisha utatuzi wa uchumi lakini hili haliwezekani kutokana na mvurugiko wa hali ya sasa ya uchumi, ambapo hisa zimejazwa na kuandaliwa katika hatua zisizo na mwisho kwa muda mrefu hata kabla ya mkurupuko wa virusi hivi.

Uchumi wa Amerika umeegemea zaidi juu ya uchocheaji wa matumizi kwa mikopo, ambapo mara tu watumizi wanapopoteza matumaini katika mfumo, uchumi wote utasimama, ambapo pia utapelekea kuvurugika uchumi wa dunia. Sababu ya uchocheaji wa matumizi kwa mikopo ni kutokana na mashirika makubwa kuziwekeza upya fedha zao katika kuzinunua tena, dhamana na bidhaa nyenginezo za kifedha ili kuongeza faida ya muda mfupi. Hivyo, kufufuka kwa uchumi kunabakia patupu na badala yake, kutokuwepo usawa na mishahara iliotuama ni hali inayoendelea, inayopelekea matumizi yaliobanika na kupunguza nguvu za uwekezaji kwenye vitu ndani ya uchumi uliofurika utajiri katika sekta ya fedha baada ya mgogoro wa makaazi.  Sheria ya Dodd-Frank ilianzishwa kuweka na kudhibiti mfumo tulivu wa kifedha lakini, badala yake, imekuwa si chengine zaidi ya kufeli tu. Kufeli kwa Sheria kumepelekea vifo zaidi vya biashara ndogo ndogo na za wastani baada ya mgogoro wa 2008. Kwa sababu Amerika ni yenye uchumi wa muelekeo wa watumizi, kuendelea kushuka kwa uchumi halisi kunaishia kuathiri uwezo wa ununuzi wa ummah. Sababu ni kuwa, hakuna mzunguko wa utajiri kutokana na kukosekana kukua ndani ya jamii mitaani. Kutoka 2000 na 2010, uwekezaji katika viwanda vipya na utafiti na maendeleo umeshuka kwa zaidi ya asilimia 21.

Wenye nguvu kubwa hupenda kukazania fikra ya soko kujisawazisha lenyewe; hata hivyo, muda hauonyeshi kuwa ni kweli. Madoido haya huwekwa ili mashirika ya fedha na mashirika mengine makubwa yaweze kudhibiti uhuru wa kuzalisha faida kubwa kadiri iwezekanavyo. Baada ya yote kuvurugika, ndipo serikali huingia kuokota vipande. Hii inaonyesha kuwa serikali huingilia tu wakati maslahi ya wenye nguvu yako hatarini, bila ya kusahau kuwa serikali ndio iliolazimisha sera za uchumi wa ki-liberali mwanzoni. Jukumu msingi la serikali ni kusimamia mambo ya watu juu ya misingi sahihi, lakini hapa, zinaongoza mambo ya watu wachache kwa misingi isio sahihi.

Pesa zinazolazimishwa na kanuni ya serikali ndio sababu inayoongoza ya kupatikana uibukaji na udorororaji wa ghafla katika uchumi. Tatizo katika pesa hizi ni kuwa hazidhaminiwi kwa kitu kilicho na thamani halisi kama dhahabu au fedha; kwa hivyo, utumiaji wa kuendelea wa sera za fedha hufanyika na Hazina ya Serikali. Thamani ya pesa hizi hutegemea pekee juu ya tamko la Serikali, thamani hutolewa juu ya mwenendo wa uchumi na ukokotoaji mgumu wa mahesabu. Ili pesa hizi zinazolazimishwa na kanuni za serikali ziweze kufanya kazi, utumiaji wa kudumu wa viwango vya riba ni sharti ufanyike ili kuinua ukuaji katika uchumi. Hivyo, mchakato wa uingizaji fedha mpya wa benki kuu kwenye mzunguko hutekelezwa ili kuzikopesha kwa ummah na kuongeza ukuaji wa uchumi.

Kwa upande mwengine, viwango vidogo vya riba kwa muda uliorefushwa vinaweza kuchochea ushukaji thamani wa fedha. Endapo jambo hili halitoshughulikiwa ndani ya muda muwafaka, basi hatimaye litapelekea kwenye viwango vya juu vya madhara ya mfumko wa bei kwa uchumi. Ili kuugeuza mtanziko huu, sera ya kuzipunguza fedha hutekelezwa ili kupunguza ukopeshaji, kuongeza thamani ya sarafu na kudhibiti mfumko wa bei. Kwa kuwa sera ya kuzipunguza fedha huongeza kiwango cha riba, huduma ya mikopo huwa ni suala la watumizi. Hivyo, hii hupelekea kwenye mzunguko unaoendelea wa kuongeza nguvu kwa ukuaji bandia na kudhibiti mfumko wa bei kupitia utumiaji wa viwango vya riba. Mzunguko huu pia unachukua nafasi ya deni la ummah lililopita kwa deni jipya kuregelea ukuaji wa kiuchumi hadi kufikia kiwango, ambapo uingizaji wa fedha mpya kwenye mzunguko hauwezi tena kusawazisha mzigo wa madeni wa ummah.

Hii humaanisha kuwa mdororo wa uchumi ni natija isiyo epukika kwa sababu ukuaji wa uchumi hauepuki kushuka. Kwa kila kipindi cha miaka 10 hadi 13 marekebisho mapya ya kiuchumi hufanywa ili kununua deni la ummah na kulibadilisha kwa aina ya deni-kiputo kipya. Kwa kawaida wahamiaji siku zote ndio walengwa wakuu wa kulaumiwa lakini hivi sasa ni tofauti. Hivi sasa mlengwa wa kulaumiwa ni Covid-19 ili kuhalalisha uingiziwaji wa mtaji, ili ummah usipoteze imani katika mfumo wa urasilimali.

Umilikaji katika Urasilimali ni unakaribia kuwa haupo kabisa kwani wengi katika jamii hawamiliki kitu chochote kwa sababu yote hutegemea juu ya rehani na mikopo. Hivyo, uhuru wa kumiliki upo tu kwa wachache. Kwa kuwa uhuru wa kumiliki ni fikra inayo jitokeza zaidi katika mfumo wa ki-liberali wa ki-sekula. Hivyo, kuurekebisha urasilimali hakutosuluhisha suala la viputo kupasuka hivi sasa wala katika mustakbali. Hii ni kwa sababu mfumo mzima unazunguka pambizoni mwa urasilimali. Suluhisho halipaswi kuwa ujamii ambao pia umefeli, tena vibaya mno. Suluhisho mbadala lahitajika livuliwe kupitia mchakato wa fikra angavu na sio kupitia mchakato wa nadharia ya vitendo, ambayo itatupelekea kwenye mzunguko wa mafumbo ya uibukaji na udororaji wa ghafla wa uchumi. Badala yake, kinachohitajika ni nidhamu tulivu ya uchumi ulio jengwa juu ya msingi wa dhahabu na fedha na usio na riba, ambao hautaporomoka kutokana na virusi, na ambao unatoa imani kwa watumizi katika jamii, nidhamu ulio jengwa juu ya thamani halisi, na sio mfumko wa thamani bandia ambapo watu hubakia katika taharuki ya kuendelea kuhusiana na kuangamia kwa mustakbali .

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na

Hashim Abid

        #ReturnTheKhilafah    #YenidenHilafet  #SimamisheniTheKhilafah  #أقيموا_الخلافة    

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 10 Aprili 2020 12:23

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu