Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Miaka 22 Ndani ya Korokoro Maalumu ya Utawala:

Waislamu 10 Wamefungwa ndani ya Kazan

Mnamo 5 Februari 2020, ndani ya Kazan katika kikao cha mahakama inayotembea, Mahakama ya Kijeshi ya Wilayah ya Volga imewahukumu Waislamu kumi kwa kushiriki katika harakati za Hizb ut Tahrir. Kwa mujibu wa maamuzi ya Mahakama Kuu ya Urusi ya 14 Februari, 2003, Chama kimetambuliwa kuwa ni harakati ya kigaidi.

Washtakiwa wameshtakiwa chini ya Sehemu 1 ya Kipengee 205.5 cha Kanuni ya Uhalifu ya Urusi (Kanuni ya Uhalifu) “Kupangilia shughuli za shirika la kigaidi”; kwa Sehemu 1 ya Kipengee 205.5 cha Kanuni ya Uhalifu ya Urusi “Kushiriki katika shughuli za shirika la kigaidi”;  Sehemu 1 ya Kipengee 205.1 cha Kanuni ya Uhalifu ya Shirikisho la Urusi “Msaada kwa shughuli za kigaidi”; Sehemu 1 ya Kipengee 205.2 cha Kanuni ya Uhalifu ya Shirikisho la Urusi “Kuulingania umma shughuli za kigaidi, kuusadikish ugaidi au propaganda ya ugaidi kwa umma ugaidi kwa kutumia angavu”; Sehemu 1 ya Kipengee 205.2 cha Kanuni ya Uhalifu ya Shirikisho la Urusi “Kuulingania umma shughuli za kigaidi, kuusadikish ugaidi au propaganda ya ugaidi kwa umma ugaidi.”

Ilnar Zyalilov alihukumiwa miaka 22 korokoroni, Ruslan Gabidullin na Azat Gataullin miaka 19 korokoroni, Abdukakhor Muminjanov amepewa miaka 17 korokoroni, Sergei Derzhipilsky – miaka 16 korokoroni, Zulfat Sabirzyanov, Komil Matiev na Farid Kreyv miaka 15 katika korokoro yenye ulinzi mkali, Rustem Salakhutdinov miaka 14 katika korokoro yenye ulinzi mkali, Ilnaz Safiullin miaka 11 katika korokoro yenye ulinzi mkali. Ilnar Zyalilov na Azat Gataullin mwanzoni walitiwa hatiani na walitumikia vifungo katika jela za Urusi kwa kujihusisha na Hizb ut Tahrir.

Washtakiwa wote walikamatwa katikati ya mwezi Machi 2017. Kwa muda wote huo wamewekwa kizuizini katika vituo vya kabla ya hukumu. Washtakiwa hawakukana uwanachama wao ndani ya Hizb ut Tahrir, lakini hakuna kati yao aliyekiri shtaka, kwa kuwa wameshawishika kwamba kimsingi hakuna kosa katika vitendo vyao. Wameeleza kuwa mashtaka yamezushwa na vitengo vya jinai vya ujasusi vya Urusi.

Kituo cha Haki za Binaadamu, Memorial, kimewatambua washtakiwa wote kuwa ni wafungwa wa kisiasa, kwa kuwa wote wamenyimwa uhuru wao kwa licha ya kukosekana shtaka msingi na tukio la uhalifu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu