Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 IMF: Chombo cha Matatizo ndani ya Mfumo wa Kinyonyaji wa Kibepari

(Imetafsiriwa)

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ni taasisi ambayo wengi ya watu katika nchi zinazoendelea wanaitambua. Jukumu lake la kuwa ni ‘kimbilio la mwisho’ huwa linatangazwa sana, na mara nyingi huonyeshwa na wanasiasa kama ni muokozi wakati wa hali ngumu sana ya kiuchumi. Lakini hii sio hali ambayo wakati wote inaonekana na wananchi wanaolazimika kuishi ndani ya maamuzi yake na mahitaji ambayo yana athari ya madhara ya kuendelea juu ya maisha yao. Watu husubiria kwa hamu taarifa za ujio wa majadiliano na IMF, na taarifa zinakutana na viwango vya kutafautiana vya masikitiko au hasira. Wakati baadhi wanafahamu kuwa rikodi ya IMF haiko kubwa, wengine wanaishia kukata tamaa kuepukana na ugumu wa uchumi wao na wameelemea zaidi kuiangalia kama ni mkombozi wao.

Lakini kila mmoja anahitaji kufahamu kuwa IMF ni chombo ndani ya mfumo. Imeundwa kudhibiti Mfumo wa Kilimwengu wa Kibepari na kuuhakikishia utawala wake wa kuendelea, na kuwa unawanufaisha wakopeshaji na sio wakopaji.

Haya yapo wazi pindi tunapoiangalia dori ya IMF katika mfumo huu.

Wakati nchi inapokuwa ni sehemu ya IMF, lazima isaini ‘Vifungu vya Makubaliano’ ambayo yanahakikisha uungaji mkono wa IMF, na mfumo unaofanya kazi ndani yake. Moja ya masharti hayo ni kuhusiana na namna nchi itavyodhibiti viwango vya ubadilishaji wa fedha yake.

Tokea mfumo wa kimataifa uliposita kutumia Mfumo wa Dhahabu, sharti hili limeingiza makubaliano ya kutoegemeza tena thamani ya sarafu yake kwa dhahabu pamoja na makubaliano ya kuwataarifu wanachama wengine namna ya kuipata thamani ya sarafu yake.

Jambo la kushangaza ni kuwa, mwanzoni Makubaliano na IMF hayakuruhusu wanachama kuwa na viwango vya kubadilika vya ubadilishanaji wa sarafu. Lakini wakati sera za kimataifa zilipobadilika kwenye miaka ya 1970, kwa kuachana na mfumo wa Bretton Woods, IMF ilibadilisha kanuni zake kupitia msururu wa mikutano, na kubadilisha Vifungu ili mabadiliko yaruhusiwe, yenye kuhitajika hasa, na kile ambacho awali kiliruhusiwa hivi sasa kimekuwa haramu.

Lakini wakati kazi ya IMF upande wa mikopo kwa kawaida huwa yenye kulenga mjadala, usimamizi wake unajumuisha kazi ya uchunguzi, ambapo inaagiza ukaguzi wa kila mwaka wa wanachama wote. Uchunguzi ni mradi unaoendelea, na hufanyika aidha IMF inaisaidia nchi wakati wa mzozo ama la. Kazi hii inaakisi sababu ya uwepo wa IMF – ambayo ni ufahamu wa kuwa mzozo wa kifedha wa taifa moja mwanachama huweza kudhoofisha wengine au hata mfumo mzima, na hivyo kila mwanachama ana jukumu la pamoja kuhusiana na mazingira na sera yake. IMF ni kielelezo cha kitaasisi katika jukumu hilo na uchunguzi wake umepangwa kutanabahisha mataifa jumla pamoja na nchi husika juu ya mizozo inayotarajiwa.

Kifungu 1V (3) kinasema “Shirika litasimamia mfumo wa fedha wa kimataifa ili kuhakikisha utekelezaji wake wenye kufaa” na Shirika litafanya uchunguzi ulio imara juu ya sera za viwango vya ubadilishaji fedha kwa wanachama…”. Japokuwa, wanasema kuwa uchunguzi utaishia kwenye Kifungu 1V (3) kwenye “sera za viwango vya ubadilishaji fedha” na taarifa muhimu kwa uchunguzi kama huo.”

Yote haya yanaonyesha namna shirika la IMF lisivyokuwa huru. Ni shirika ambalo linafanya kazi kama sehemu ya mfumo wa kimataifa - likisawazisha ambapo ni lazima na kuhakikisha kuwa mataifa yanafuata sheria na maadili yaliowekwa kuhakikisha kuwa mfumo unadhibiti ubwana wake duniani.

Na hivyo, wakati nchi inakuwa sehemu ya IMF, inaahidi kuunga mkono mfumo huu.

Nchi inapokuwa mwanachama wa IMF, inaahidi kushirikiana na wanachama wengine wote katika kutatua matatizo ya kifedha ya kimataifa. Wanachama wanatakiwa kupeana taarifa juu ya masuala ya kifedha, kodi, uchumi, na sera za ubadilishanaji fedha ambazo zina athari kimataifa. Wanachama lazima waepuke kujizuia kuweka mipaka katika kubadilisha fedha za ndani kwa fedha za kigeni. Zinajifunga zenyewe kufuata sera za kiuchumi ambazo zitachochea ajira na biashara ya kimataifa kwa manufaa ya jamii nzima ya kiuchumi ya dunia.” (Chanzo)

Wanapotupatia mkopo, wanajumuisha masharti, ambayo ni sehemu ya “mipango yao waliyoorodhesha ya marekebisho ya muundo: kupunguza matumizi ya serikali, kupunguza mishahara na marupurupu, wanasisitiza kuwa mashirika yanayomilikiwa na serikali yanarejea kwenye sekta binafsi, kupunguza viwango vya chini vya mishahara, na kuzuia makubaliano ya pamoja baina ya wafanyikazi na waajiri.” (Reuters)

Ni muhimu kukumbuka kuwa dhumuni la IMF sio kuzisaidia nchi kuendelea… Bali ni la kifedha tu

Tunapoangalia IMF, ni muhimu sana kuweka dori yao ndani ya mfumo wa kimataifa kwenye muktadha sahihi. Kwa sababu mara tu tunapofahamu lengo kuu, kila kitu kitaeleweka.

Lengo muhimu zaidi la IMF sio kusaidia nchi kuendelea, lengo lake ni kuchangia kwenye utulivu wa kifedha wa kimataifa.

Likiwa na dhumuni hili, IMF huweza tu kukopesha kwenye nchi iliyo na matatizo ya karibuni ya urari wa malipo. Hutoa mikopo ya muda mfupi ya fedha za kigeni ambazo nchi inayokopa lazima itumie kugharamia utulivu wa sarafu yake yenyewe au mfumo wa fedha. Likiwa ni sharti la awali la mkopo, Shirika hili kwa kawaida linahitaji mkopaji kubadilisha sera zake kwa namna ambayo itawezesha utulivu wa kifedha kwa kipindi kijacho.

Na inategemea deni lake sio tu lilipwe, lakini pia kupata faida kutokana nalo. Kwa hiyo linapotoa mkopo hutoza malipo ya ziada kwa nchi zenye mikopo mikubwa kutoka IMF ambazo hazilipwi ndani ya muda mfupi.

“IMF inakisia nchi wakopaji zitalipa zaidi ya dolari bilioni 4 zikiwa ni malipo ya ziada juu ya malipo ya riba na ada kutokea mwanzoni mwa mzozo wa Covid19 hadi mwishoni mwa 2022. Vile vile, IMF inakisia malipo ya ziada yamekuwa ni chanzo kikubwa zaidi cha mapato ya Shirika, ikichukua takriban nusu ya mapato katika kipindi hiki. Pia inakisiwa kuwa FY2027, malipo ya ziada yatakuwa takriban thuluthi mbili ya mapato ya mikopo ya IMF—kiasi mara mbili ya kiwango katika FY2018.” (Chanzo)

Huku hoja ikiwa ni kwamba malipo ya ziada kuwa yanatozwa kuweka vikwazo kwa matumizi makubwa na ya muda mrefu ya rasilimali za IMF, huruhusu Shirika kuendelea na jukumu lake kuu la kuwa ni kimbilio la mwisho la kiulimwengu wakati wa mizozo, idadi ya nchi zilizokwama katika mtego wa madeni inatuonyesha kuwa dhumuni sio kuzisaidia nchi wakati wa haja.

“Kuna jumla ya nchi 93 zinazodaiwa na IMF, kukiwa na deni jumla lipatalo $155bn hadi Machi 31, 2023 au $115.2bn zikiwa ni haki maalum ya kupata fedha (SDRs), ambapo fedha za mkopo zimeongezeka kufuatia dhamana iliyokubaliwa karibuni kwa ajili ya kuendeleza chumi dhaifu. Pakistan ni ya tano kwa kuwa na deni kubwa zaidi la IMF, likiwa ni $7.4bn. Mnamo Agosti 2022, IMF ilitanua hadi $1.1bn kwa nchi za kusini mwa Asia ikiwa ni sehemu ya mpango uliokubaliwa wa $6.5bn mnamo Julai 2019.” (Chanzo)

Majaribio ya kulazimisha malipo kupita kiasi hayana tija kwa sababu yanashusha uwezo wa uzalishaji uchumi… Wakopeshaji na nchi zenyewe zinakuwa kwenye hali mbaya zaidi … I.M.F. haitakiwi kuwa katika biashara ya kinyonyaji kwa nchi zilizo na hali ngumu … Wanaziadhibu nchi wakati ambapo zipo katika hali ya dhiki, wanazilazimisha kufanya makato makubwa zaidi ili ziweze kulipa madeni.” (Chanzo: NY Times)

Wakati unapozingatia mazingira ambayo IMF inayaweka kwetu, unaona kuwa lengo sio kutusaidia kuendelea na kuwa wenye kujitegemea kupitia mabadiliko ya sera ambayo yanataka kutoka kwenye nchi zetu. Inalenga kuhakikisha kuwa tunalipa fedha inazodai, na kuweza kuhakikisha kuwa mfumo wa kifedha wa kimataifa unabaki imara.

Je tunaweza kushindwa na madeni ya IMF?

Katika nukta hii, tunahitaji kufahamu kuwa madeni ambayo nchi inadaiwa na IMF hayasamehewi - yanapangiliwa upya. Kwa hivyo vifungu vya makubaliano vinaweza kubadilishwa na kujadiliwa tena, tarehe inaongezwa, malipo yanasimamishwa hadi mzozo wa kisiasa au wa kiuchumi umalizike ili malipo yawezekane.

Lakini nchi lazima ilipe madeni yake kwa IMF.

Hivyo kushindwa kulipa sio uhuru - ni kauli tu tuna matatizo, tafadhali tupe muda wa kulipa madeni.

“Sio deni. Ni mbadilishano wa mali kwa mali. Ni mbadilishano wa sarafu ya nchi ambayo haina thamani kulinganisha na sarafu ambazo kwa hakika zinakupa nguvu sokoni.” (Financial times)

Hatuwezi kusema tu hapana… Kama tunataka kujiweka mbali na mfumo huu

Ni kweli kuwa IMF haina nguvu za kisheria au mamlaka ya kulazimisha mataifa kubadilisha sera zao au kuwaadhibu wale wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao… wao wenyewe.

Hatua muhimu, inayohusiana na kushurutisha na kutowafikiana, inapatikana katika Vifungu vya makubaliano.

“Ikiwa mwanachama ameshindwa kutimiza chochote katika majukumu yake chini ya Mkataba huu, Shirika linaweza kumtangaza mwanachama kuwa hastahiki kutumia rasilimali jumla za Shirika… Pindi, baada ya kumalizika kwa muda muafaka kufuatia tamko la kutostahiki … mwanachama akaendelea katika kushindwa kwake kutekeleza chochote katika majukumu yake chini ya Mkataba huu, Shirika linaweza, … kusitisha haki yake ya kupiga kura” na hatimaye “mwanachama huyo huweza kutakiwa kujitoa kutoka kuwa mwanachama wa Shirika.”

Kama kuna suala la kukubaliana na masharti ya mkopo mmoja, basi IMF inaweza kutishia kuzuia utoaji wa baadaye wa mkopo. Lakini nguvu zao nyingi huja kutokea kwenye mbinyo wa kitaasisi na ule usio rasmi, zikiwekwa pamoja nguvu za sarafu za aina tafauti katika uchumi wa kisiasa wa kimataifa: ushawishi wa kisiasa, kitisho cha heshima na kiwango cha mkopo, na juu ya yote pendekezo ambalo litatoa fursa kwa mikopo ya baadaye kuwa ina kwenda sambamba na tabia sahihi kulingana na mikopo ya sasa. Mambo haya yanaonyeshwa kwa umuhimu mdogo tu katika Vifungu vya Mkataba.

Sasa, inawezekana kuhimili mbinyo wao – pindi tu ukiwa na nguvu za kisiasa za kufanya hayo, na nyingi ya nchi zinazoendelea hazina. Hii sio kwa bahati mbaya – historia na hali ya sasa ya maendeleo ya kisiasa yanaonyesha namna mfumo wa kimataifa ulivyo andaliwa kuhakikisha mataifa yenye nguvu yalivyo na fursa dhidi ya mengine duniani. Mataifa yalio na mahitaji zaidi ndio ambayo, yenye uwezo mdogo zaidi wa msukumo kwenye mabadiliko katika IMF – mfumo wa upigaji kura unaotegemea idadi ya kikomo, ambao unaamuliwa na fedha   unazochangia kwenye Mfuko, na ni wazi kuwa nyingi ya nchi zinazohitajia mikopo zina fungu dogo.

Hivyo, kimsingi hata kama nchi zitashindwa kwa muda, hatimaye wanalipa deni ili ziweze kushiriki ndani ya mfumo wa kimataifa. Kwa sababu mwisho wa siku, mataifa ndani ya mfumo wa kimataifa wote ni watiifu kwa mfumo wa Kirasilimali – kwa sababu bila ya mfumo huo, dola za kitaifa hazitoweza kuwepo, na serikali na matabaka ya watawala hayatoweza kunufaika nao.

Kama hatukuweza kujitoa kutoka IMF – tuna chaguo gani?  

Sasa, ufafanuzi mwengine muhimu ni kuwa nchi kwa kawaida huwa inadaiwa na zaidi ya mdeni mmoja. Mikopo wanayodaiwa huwa chini ya ‘deni huru’. Na wakati nchi inaposema kuwa inaelekea ‘kushindwa’, inamaanisha kuwa haiwezi kulipa wadai hawa. Ndipo wanapoelekea kwa IMF kwa ‘dhamana’ iwasaidie kulipia madeni wanayodaiwa na wengine.

Na hii ndio sababu kwa nini hali inakuwa ya kufadhaisha namna hii.

Suala ni kwamba katika hali kama hizi, na baadhi ya nyengine, fedha za IMF huweza kuwa ni njia pekee ya kifedha inayopatikana kwa nchi zilizo katika mdororo wa madeni, na ni ufunguo wake wa kuibua vyanzo vyengine vya kifedha. Wakati wengine wasingekuwa tayari kutoa mikopo kwa nchi pindi wakiamini kuwa deni halitohimilika. Ndio maana utagundua kuwa nchi kama Saudi Arabia ilijizuia kuipatia mkopo Pakistan hadi walipokuwa na uhakika kuwa IMF na Pakistan zimeshakubaliana.

Kwa upande mwengine, katika hali ya karibuni zaidi ya Pakistan, IMF imeitaka kuonyesha kuwa tunaweza kuvifungua vyanzo vyengine vya fedha, hivyo lazima tuzikaribie nchi nyengine na kuweka mikataba nazo kupata mikopo ili IMF iweze kuzingatia kutupatia mikopo mipya. Hivyo, tunajikuta tumezama kwenye mtego wa madeni ya kujiimarisha. “Pakistan imeitaka IMF kuipatia dolari bilioni 1.1 kama nyongeza ya kutatua mzozo, lakini kutolewa kwake kumecheleweshwa kwa miezi kadhaa. IMF imetaka uhakikisho zaidi wa ufadhili kabla ya kuidhinisha kifurushi hicho.” (Chanzo)

Je, tuna chaguo jengine?

Tuchukulie, kwa muda tu kuwa Pakistan imeamua kusema kuwa imetosha. Itabakia ndani ya mfumo huu na kubaki kuwa dola ya kitaifa lakini haitolipa tena madeni ya IMF, au kuwaendea kwa ajili ya msaada kwa ajili ya kulipia madeni mengine.

Kisha nini?

Serikali inayapatia rasilimali zetu makampuni ya kigeni, kuyaruhusu kuchukua sehemu ya umiliki juu ya maliasili zetu, au kuweka viwanda kuziboresha. Hivyo, kama tutachukua hatua ya kujitenga na IMF - na hivyo kujitenga na mfumo wa kimataifa - hatutokuwa na mamlaka juu ya rasilimali zilizopo ndani ya nchi zetu, ambazo tungezihitajia ili tuweze kuendelea.

Nchi nyengine zinaweza kusitasita kufanya biashara na sisi, katika kulipiza kisasi kwa ‘usaliti’ wetu na makampuni ya kimataifa ambayo tunayategemea kwa vitega uchumi yanaweza kutokuwa tayari kufanya kazi na sisi kwa sababu wanaweza kutuona kama ni mzigo kwao.

Kwa akili zao, kuwa mwanachama wa IMF, inasaidia nchi kutenda kazi ndani ya mfumo wa kimataifa kwa sababu wanatambulikana kuwa wanafuata kanuni za maadili ya IMF. Hii inawahamasisha wadau wengine – nchi, makampuni, watu binafsi – kuweka vitega uchumi na kufanya biashara nao.

Kwa hivyo, tunajikuta tumenaswa ndani ya hali ambapo ulimwengu unaoendelea umebanwa na mataifa yenye nguvu, yamenaswa ndani ya duara lisilofikia mwisho la madeni na kutoweza sisi wenyewe kuendelea katika namna ya maana.

Haya yote yanaweza kuonekana kutokuwa na matumaini. Lakini ni uhalisia ambao unaimarisha ukweli ambapo kama tunataka kujikwamua kutoka IMF basi lazima tubadilishe mfumo.

Kuna sababu ya kwa nini taasisi hiyo iliyo asisiwa mnamo miaka ya 1940, kuwa imeweza kudhibiti dori yake katika mfumo huu - licha ya upinzani dhidi yake. Na kama tulivyoonyesha, sababu ya kuwepo kwake sio kuhakikisha kuwa dunia inakuwa mahala bora zaidi. Lakini IMF ni sehemu isiyotenganishwa na mfumo huu, na hatuwezi tu kuachana nao. Wala hatuwezi kujaribu kubadilisha hali hii kwa kufanya kazi ndani ya mfumo huu.

Kama tunataka mabadiliko, tunahitaji kubadilisha mfumo

Unaweza kushangaa vipi hayo yatawezekana. Hatuna fursa juu ya rasilimali zetu kwa muda huu, na Khilafah itakapokuja, hatutoweza kufanya kazi ndani ya mfumo huu. Lakini hiyo ni fikra mgando tuliobebeshwa nayo, tokea wakati tupokuwa wadogo.

Tunaweza kuwa na fursa ya rasilimali zetu, na tutakuwa katika hali bora bila kuwa tumenaswa na kanuni za kinyonyaji za mfumo wa sasa wa kimataifa. Inawezekana, lakini tu tutakapofuata Njia ya Mtume wakati tutapoisimamisha tena Khilafah.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surah Al-Maida: 51].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu