Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuporomoka kwa Marekani katika Muono Wake

(Imetafsiriwa)

Tokea wakati wa majanga ya vita vya Iraq na Afghanistan na kuibuka kwa China, wengi walizingatia kuwa kipindi cha kuwepo dola kuu moja pekee kina malizika. Wengi wanazingatia nguvu ya Marekani kidunia inaporomoka na kutaja hili kuwa ni dalili muhimu ya kumalizika kwa dunia yenye dola kuu moja. Kama Marekani ipo katika kuporomoka na hali ya uwepo wa dola kuu moja unamalizika basi itakuwa na athari kubwa duniani. Pindi Marekani ikiwa inaporomoka na kuwepo mbadilishano wa nguvu kuelekea kupatikana dunia yenye dola kuu nyingi, basi mpangilio huu utafungua hali tafauti katika kuwepo uwezekano wa kuibuka muundo mbadala wa ulimwengu.

Moja ya hoja zinazojitokeza zaidi kuashiria kuanguka kwa Marekani ni kuwa dunia inageuka kutoka kuwa na dola kuu moja kuelekea kuwa na dola kuu nyingi. Hili linarejewa mara nyingi katika vyombo vya habari na kawaida hMarekaniukumwa na upandaji wa kasi wa China na hivi sasa uvamizi wa UrMarekanii nchini Ukraine. Washauri mabingwa wengi nchini Marekani, Ulaya na kwengineko wanahubiri uoni huu. Hoja hii bila shaka ni maarufu zaidi hivi sasa kuhMarekaniu kuporomoka kwa Marekani.

Tunahitaji kuzingatia masuala kadhaa tunapochunguza maono haya. Je ni lengo la sera ya kigeni ya Marekani kuhakikisha ubwana wa dolari ya Marekani? Je, ni kuwa juu zaidi kiuchumi? Je, ni kuhakikisha kuwa hakuna dola shindani zinazoibuka zitazonufaika na fungu hilo hilo la utajiri wa kiuchumi? Pindi tunapoangalia masuala haya, tunayaona kuwa ni muhimu kwa Marekani na ni malengo yake, lakini sio wasukumaji wa sera za kigeni za Marekani. Kama malengo ya sera za kigeni za Marekani ilikuwa ni ubwana wa kiuchumi, kwa nini iliisaidia China katika kuiinua kiuchumi? Ilikuwa ni Marekani iliyoikaribisha China kwenye uchumi wa kilimwengu na WTO mnamo 1999 na kuiunganisha katika biashara za kimataifa na mifumo ya kifedha. Ilikuwa ni Marekani ilioruhMarekaniu fedha za China kuingia kwenye mali zake zisizohamishika, masoko ya kifedha na sekta za teknolojia.

Lengo kuu la sera ya nje ya Marekani tokea Vita vya Pili vya Dunia (WW2) limekuwa ni kuunda na kudhibiti mpango wa kiliberali wa dunia ambapo mataifa mengine yanashiriki na kujisalimisha nao. Hii iliihakikishia nguvu ya Marekani. Wakati China ikipata vichwa vya habari vingi kwenye mashirika kama BRICS, SCO na Benki ya Miundombinu ya Asia, haya sio mbadala wa mpango wa sasa. Bali, ni miundo iliyo sambamba na nchi washiriki zilizounganishwa kikamilifu kwenye mpango wa kiliberali wa dunia.

Wengi wanaamini kuwa kusinyaa kwa fungu la Marekani katika GDP (Pato Ghafi la Nchi) ya dunia dhidi ya mataifa mengine makubwa pia ni dalili ya kuporomoka kwa Marekani. Manguli wa uoni huu wanaamini kuwa GDP ni sawa na nguvu ya kiuchumi na hivyo inaathiri. Hoja hii kwa hakika inapata umaarufu tokea wakati wa mzozo wa kiulimwengu wa kifedha mwaka 2008, ambao uliziathiri zaidi Marekani na nchi za Magharibi, huku China kwa kiasi fulani ilijitenga na haikuhisi athari za kifedha kama nchi nyengine. Marekani ilikuwa na asilimia 50 ya GDP ya dunia baada ya WW2, ilikuwa na akiba kubwa zaidi ya dhahabu na ilikuwa muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta. Asilimia hii ya GDP imekuwa ikiendelea kuporomoka na hivi sasa ipo kwa kiwango cha asilimia 15.

Kama tutayaweka haya katika uoni, Himaya ya Uingereza mnamo katikati ya karne ya 19 ilikuwa katika kilele ikiwa na wastani wa asilimia 7 ya GDP ya dunia. Inategemewa zaidi kuwa mataifa mengine yataongeza GDP zao na kulimega fungu la Marekani. Ulaya na Japan zilidhoofishwa baada ya WW2 na ilikuwa malengo ya kimkakati ya Marekani kuzigeuza kuwa mifano ya mafanikio ya uchumi wa kirasilimali wa soko huru ili kushindana dhidi ya wito wa Ukomunisti wakati wa Vita Baridi. Ilikuwa ni lengo la sera ya kigeni ya Marekani kuunda fursa mwanana kwa nchi nyengine kuzifikia Marekani ikiwa ni mifano ya mafanikio ya uchumi wa Kirasilimali.

Data za kiuchumi na takwimu hakika zinaakisi kuporomoka uchumi wa Marekani. Kwa watu wengi, wanapoangalia sekta ya viwanda ya Marekani ikielekea nje ya nchi na kuongezeka deni la serikali ya Marekani na deni la walaji, kunaonyesha Marekani inakabiliwa na changamoto za kiuchumi. Hatuhitaji kuweka akilini kuwa dola kuu zote zinafikia kilele na ushukaji kiasi hicho na kuwa data za kiuchumi hazigusi kila kitu. Uvumbuzi wa teknolojia ya Marekani, kuongoza kijeshi na kuwepo kijeshi maeneo mengi duniani ni wa kipekee. Hivi leo Marekani ina mkono mrefu wa kiuchumi unaouwezesha kumiliki utajiri wa dunia kwa hasara ya wengine. Hii ndio sababu Marekani ni tajiri zaidi kuliko China, na ndio sababu ina rasilimali nyingi za ziada kuzitumia kwenye machafuko kuliko China.

Dunia inashuhudia migeuko mikubwa ya kisiasa na mingi isiyotarajiwa katika Mashariki ya Kati. Hata hivyo, hakuna kati ya matukio haya linaloakisi kuibuka kwa mpango wa kuwepo dola kuu nyingi duniani kwa maana ya kupunguza nguvu za Marekani na kuzuka nguvu shindani na jumuiya kwa kiwango chake cha uongozi wa dunia. Ili dola kuu ianguke kunahitaji kuwepo misukumo mikali ya nje na ndani, hasa ya nje kama Dola ya Uthmaniya ilivyofanya ilipokabiliana na mashambulizi ya mataifa koloni na kuteka maeneo yao, au Ujerumani ilipoondolewa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, wakati mataifa shirika yalipotishiwa na uvamizi wa Ujerumani barani Ulaya. Kwa hivi sasa, ima iwe China au Urusi, hakuna yenye kutaka kuchukua nafasi ya mpango wa mfumo wa dunia na kuingia katika mapambano ya kisiasa ili kuuweka. Hadi hapo itakapotokea, haielekei kuwa hali ya dunia itabadilika.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu