Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Huku Taliban Ikielekea Kabul, Hofu Kubwa ya India Huenda Ikapatikana

(Imetafsiriwa)

Wakati Taliban ikijikusanyia wilaya zaidi na kusonga kuelekea Kabul, serikali ya India imeendelea kukosa subira kwa kuwa ushawishi wake jijini Kabul utafutika kabisa. Kwa miaka, New Delhi imeisaidia serikali ya Afghan kwa fedha, silaha na utaalamu, na kuwa na umakini mchache sana na harakati ya Taliban na wafuasi wao. Hivi sasa India inajisogeza kwa shida kufungua majadiliano na Taliban, ikiwa ni sehemu ya jitihada mpya za Modi kubakisha ushawishi katika nchi iliyovurugwa kwa vita. Kuna sababu tatu kwa nini India inashughulishwa sana na kuibuka kwa Taliban.

Kwanza, tabaka teule la Mabaniani linajali sana juu ya kwamba kihistoria Afghanistan mara kadhaa imefanya mashambulizi ndani zaidi ya India ili kusimamisha utawala wa Kiislamu. Wakati wa utawala wa Mahmud Ghazni (971-1030) Afghanistan, India ilivamiwa mara kumi na saba na kutanua maeneo ya utawala wake, kukusanya kodi na kutekeleza sheria za Kiislamu na utengamano. Pia alibomoa masanamu maarufu ya Somnath, Kangra, Mathura na Jwalamukhi kuwafanya Wahindu watambue kuwa masanamu yao yalikuwa hayana nguvu kujilinda yenyewe na kuwa kujilinda ni kupitia tawhid pekee. Utawala wa Ghurid (1175-1206) ulifanya mashambulizi saba nchini India na kuzitabikisha sheria za Kiislamu katika maeneo kama Anhilwara, Thanesar, Chandawar, Multan na Lahore. Hata Ufalme maarufu wa Delhi (1206 hadi 1526) uliotawala sehemu kubwa ya India kwa miaka 320 asili yake inatoka Afghanistan. Muasisi wake Qutb ud-Din Aibak alikuwa jenerali mtumwa chini ya komandi ya Utawala wa Ghurid. Mwishowe, India yote iliwekwa chini ya Utawala wa Kiislamu wakati wa Utawala wa Mughal (1526-1857). Baber – muasisi wa Utawala wa Mughal – alijikita jijini Kabul mwanzoni kabla ya kukiuka Mapito ya milimani ya Khayber kumshinda Ibrahim Lodhi katika Panipat. Baada ya kifo cha Aurangzeb mwaka 1707, Utawala wa Durrani ukiwa na kambi Afghanistan uliingilia Punjab mara kadhaa kurejesha amri za Uislamu. Hivyo, tishio la uvamizi kutoka Afghanistan limepata umashuhuri katika nyoyo za tabaka teule la Mabaniani.

Pili, kadhia hii ya kihistoria iliochanganyika na tishio la Pakistan imeisukuma sera ya India kuelekea kuiunga mkono serikali iliyoanza baada ya Septemba 11, 2001. Zaidi ya hayo, Amerika kuikumbatia India kwa kuikabili China kumeongeza hamasa zaidi jijini New Delhi kuisaidia serikali ya Kabul. India imewekeza jumla ya dolari bilioni 3 katika miradi ya mabwawa, barabara, miundo mbinu na biashara nchini kwa miongo miwili iliopita. Mwaka 2011, Makubaliano ya Ushirikiano ya Kimkakati ya India na Afghanistan imewajibisha msaada wa India kwa Afghanistan katika juhudi za kuijenga Afghanistan na biashara ya pande mbili, ambayo hivi leo inafikia dolari bilioni 1.5. Mbali ya jitihada za ujenzi mpya, India pia imevifunza na kuviwezesha kwa vifaa vikosi vya usalama vya Afghanistan na kutumia mtandao wake wa kibalozi kutekeleza operesheni za kijeshi za siri katika Baluchistan. Hata wakati Taliban ilipokusanya nguvu kutekeleza mashambulizi kuelekea Kabul, India bado imekuwa ikisafirisha silaha kwa jeshi la Afghanistan. Mnamo Julai ndege 16 aina ya C-17 za Kikosi cha Anga cha India (IAF) ziliwasili kwenye Kambi ya Anga ya Kandahar na kupeleka tani 40 za makombora ya 122mm. Taliban walijibu kwa ukali kipindi cha nyuma kuhusiana na hilo na hadi sasa imepuuza mazungumzo ya awali ya amani. Suhail Shahiin, msemaji wa kundi hilo amesema, “Tuna taarifa kutoka kwa makamanda wetu kuwa India inatoa silaha kwa upande wa pili. Itawezekanaje wawe wanataka mazungumzo na Taliban lakini kivitendo wanatoa silaha, droni, na kila kitu kwa Kabul? Hii ni kujikinza.” Lengo kuu la India nyuma ya hatua hizi ni kuhakikisha Afghanistan inabakia kuwa nchi ya kisekula na kuzuia Uislamu kuichukuwa nchi hiyo.

Tatu, baada ya udhalilifu wa Kargil mwaka 1999 na kuondoshwa Taliban madarakani mnamo Disemba 2001, kanuni za kijeshi za India na sera za kigeni nchini Afghanistan zimepitia mabadiliko mengi. Sifa za mkakati huu zimezingatia hasara ya ya kina cha mkakati cha Pakistan – kutokana na ushindi wa Amerika dhidi Taliban na kusimamishwa kwa serikali mpya jijini Kabul inayoegemea sura ya Kongamano la Bonn. Hivi leo, hesabu za kisiasa za India zipo kwenye kukuuza mazingira ya kiuadui juu ya mipaka ya Magharibi na Mashariki ya Pakistan, na kuinasa mtegoni baina ya Afghan na vikosi vya usalama vya India. Haya ndio takriban yaliyopelekea mvutano wa kijeshi baina ya mataifa mawili yenye nguvu za nyuklia mapema miaka ya 2000, hadi Amerika kuingilia kati kuituliza hali. Hata hivyo, uadui wa Afghanistan kupinga maafikiano yoyote na Pakistan umebakia kuwa ni nguzo kuu ya sera ya India kwa miaka ishirini iliyopita. Hata hivyo, mafanikio ya kustaajabisha waliyoyapata Taliban hivi karibuni yanahatarisha kuiangusha mantiki hii ya kimkakati kwani matarajio ya Pakistan ya kusimamisha tena kina chake cha kimkakati nchini Afghanistan yanaonekana kuwa karibu zaidi kuliko wakati mwengine wowote katika miaka ishirini iliopita. Haya yanajiri katika wakati mbaya zaidi kwa New Delhi kwa sababu India inakumbana na uwepo wa kijeshi unaoongezeka kwenye mipaka yake na China na inakabiliana na mapambano mabaya na Jeshi la Ukombozi la Watu wa Laddakh. Wakati huo huo, India inahangaikia kwa taabu kufungua njia na Taliban kuhakikisha ni kwa kiasi gani marekebisho yafanyike kwenye kanuni zake za kijeshi na sera ya nje nchini Afghanistan.

Waafghan waliwashinda Waingereza mwaka 1862, Wasovieti mwaka 1989 na Waamerika 2021. Kwa mazingira kama haya India haitopeleka vikosi ikihofu matokeo sawa na hayo. India pia inahofu kuwa Taliban itafikia mamlaka Kabul. Lakini wasiwasi mkubwa wa tabaka la mang'weng'we wa Kibaniani ni kwa wenye kupendelea Uislamu kuchukua mamlaka jijini Islamabad na kisha kuunganisha Pakistan na Afghanistan chini ya bendera ya Shahada. Hiyo haitomaanisha tu mwisho wa uchokozi wa India kwa Waislamu, bali pia itaharakisha kusimamishwa Uislamu nchini India na kusimamisha hukmu za Sharia katika bara hilo dogo la India.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na

Abdul Majiid Bhatti

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu