Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Fikra ya Uislamu juu ya Mfumo wa Ulimwengu

Suala la Mpango wa Ulimwengu limeungana kwa karibu na linavyojiangalia taifa au jamii. Namna gani jamii inavyojiangalia yenyewe? Ni nini ujumbe wa jamii hiyo? Ni nini utambulisho wa jamii hiyo? Na ni vipi uangaliaji huu binafsi wa taifa unahusiana na jamii nyengine na mahusiano ya Ulimwengu? Kwa hivyo takwa la Mfumo wa Kiulimwengu ni takwa la taifa au jamii kwa ajili ya mahusiano yake pamoja na nchi na jamii nyengine katika Ulimwengu, katika namna ambayo itaimarisha na kuthibitisha kujiangalia sura ya taifa au jamii hiyo. Hivyo ubora, maumbile na muundo wa Mfumo wa Kiulimwengu katika wakati wowote ni natija ya moja kwa moja ya mwelekeo wa kiitikadi, maslahi na tamaa ya taifa au mataifa yenye nguvu zaidi kwa wakati huo. Kwa hivyo ni sawa zaidi kuuona Mfumo wa Kiulimwengu kuwa ni matokeo ya kimaumbile ya mashindano baina ya mataifa makubwa yenye nguvu, ambapo kila taifa au jamii hutaka kuingiza mtazamo wake kuhusiana na namna ya kuendesha mahusiano baina ya jamii tofauti, juu ya wengine, na kwa kile tukionacho kuwa ni uundaji wa mwisho wa mahusiano, baina ya mataifa tofauti au jamii za Ulimwengu, ni kazi ya nguvu na ushawishi wa mataifa yenye nguvu zaidi kujiingiza katika mashindano haya. Hivyo ni muhimu kulielekea suala la kuwekwa kwa Mfumo wa Kiulimwengu kwa namna ya tahadhari. Mfumo wa Kiulimwengu haufasiriwi na haupaswi kufasiriwa kama mpangilio wa kitaasisi usiobadilika wa kuongoza mahusiano baina ya jamii tofauti za Ulimwengu katika namna ya kudumu. Kwa mtazamo kama huo ni kutofahamika mahusiano ya kimataifa na haitofautishi baina ya jamii ya ndani na jamii ya kimataifa.

Kile ambacho kinaiunda jamii ya ndani mbali na ile ya kimataifa ni suala la udumishaji katika maumbile ya mahusiano kwenye jamii ya ndani, ambayo hayapo katika mahusiano ya kimataifa. Jamii ya ndani hujumuisha mahusiano ya kudumu baina ya washiriki wa jamii na hivyo washiriki wa jamii huendeleza fikra, imani na vigezo katika upangaji wa mahusiano haya. Baada tu ya makubaliano kuhusu mahusiano haya yaliowekwa kufikiwa, jamii ya ndani humchagua mtawala au mamlaka kuendesha mahusiano haya ya kudumu ya jamii, kulingana na fikra, imani na vigezo ambavyo jamii ya ndani imevishika kuelekea mahusiano haya. Ni muhimu kuzingatia kuwa kile kinachobadilika katika jamii ya ndani kutokana na mabadiliko ya kiitikadi ni fikra, imani na vigezo vya jamii kuelekea kupanga mahusiano baina ya washiriki wake, na sio udumishaji wa mahusiano baina ya washiriki wa jamii ya ndani. Udumishaji huu wa mahusiano hushurutisha muundo usiobadilika wa upangaji wa jamii ya ndani ambayo hushirikisha watu, fikra zenye kuwatawala, na hisia kuhusu mahusiano katika jamii, na mamlaka, yenye kudhibiti mahusiano hayo, kulingana na fikra zenye kutawala na imani za jamii.

Hali hii haipo katika jamii ya kimataifa. Hakuna kilicho cha kudumu kuhusu mahusiano baina ya jamii tofauti. Kwa kuwa mahusiano baina ya jamii tofauti ni kazi ya mtazamo wa hali ya nchi moja moja, kwa namna ya nchi hizi zinavyojiangalia zenyewe, na hivyo mahusiano yao na Ulimwengu. Hivyo, hakuna makubaliano ya kudumu kuhusiana na maumbile ya mahusiano ya kimataifa yanayoweza kuwepo miongoni mwa mataifa tofauti ya Ulimwengu. Kikawaida, kama hakuna mahusiano ya kudumu baina ya mataifa, hakuna mamlaka yanayohitajika kuyadhibiti mahusiano ya kimataifa baina ya jamii tofauti. Kwa hivyo, takwa la taasisi za kudumu kusimamia Mfumo wa Kiulimwengu, kwa mahusiano ya muundo maalum baina ya nchi ni takwa la uongo. Bali ni msimamo wa kiitkadi wa Wamagharibi na mtazamo wao maalum kuhusiana na usimamiaji wa masuala ya Ulimwengu.

Hata hivyo inawezekana kuuona udumishwaji na uthabiti katika kuelekea kwenye kupanga mahusiano maalum ya taifa na sehemu zilizobakia za Ulimwengu, wakati taifa linachukua njia ya kudumu, imara na isioteteleka katika mtazamo wa kuelekea kupanga mahusiano yake na maeneo mengine ya dunia. Mtazamo kama huo utachukuliwa na mataifa ya kimfumo ambayo huchukua njia imara katika mwenendo wa mahusiano yao ya nje. Hata hivyo, udumishwaji huu wa mtazamo unatokana na taasisi ya ndani ya taifa hilo na mtazamo wake kuhusu maisha na jinsi linavyojiangalia. Haitouunda Ulimwengu moja kwa moja katika muundo wa mahusiano thabiti yasiobadilika. Udumishwaji wowote katika mahusiano baina ya mataifa tofauti ya Ulimwengu utaonekana tu pindi taifa la kimfumo lenye mtazamo thabiti kuelekea mahusiano ya kigeni utakuwa mkubwa na taifa kuwa lenye ushawishi mkubwa zaidi Ulimwenguni. Taifa kama hilo litatumia nguvu zake na ushawishi kulazimisha dunia juu ya uoni maalum kuhusu namna mahusiano baina ya mataifa tofauti ya Ulimwengu jinsi yanavyojipanga.

Uoni wa Wamagharibi kuelekea Mfumo wa Kiulimwengu hutaka kuweka udumishaji wa mahusiano ya kimataifa, yaani kukusudia kuunda mahusiano haya kulingana na mtazamo wa Kimagharibi. Wazo la kimsingi la imani ya Wamagharibi la Mfumo wa Kiulimwengu ni fikra ya ubwana wa dola, uliotokana na mataifa adui ya Ulaya katika mwaka 1648 katika jimbo la Ujerumani la Westphalia. Katika Westphalia, majimbo yakijulikana kama ni vitengo vya kisiasa vilivyo huru na Makanisa yaliokuwa yamefungamana nayo, amani ya ndani ya Ukristo iliwafikiwa, iliomaliza vita vya makundi katika Ulaya na fikra ya nchi kufungika na mipaka ya eneo, katika sura ya mataifa yenye mizizi katika ukabila yalio na historia ya uwepo wa jamii moja au ndani ya mipaka maalum ya kijiografia. Hivyo mahusiano ya kimataifa huweza sasa kufanyika kwa udumishwaji fulani katika maumbile yake, ya mbele yao ni kukiuka haki ya mipaka ya eneo la nchi, kufafanua utambulisho wa jamii kama taifa ima limechipuka hasa au ni mjumuiko wa makabila au watu waliofungamana na mipaka maalum ya kijiografia na kujifunga kuheshimu na kulinda haki maalum za jamii kuainisha mwelekeo wake wa kimfumo. Badala ya mataifa kutekeleza mahusiano yao ya kigeni kwa mujibu wa mtazamo wao kuhusu mahusiano kama hayo, Mataifa yanatakiwa kujifunga katika misingi iliotajwa katika utekelezaji wa sera zao za kigeni, ambapo huweka msingi wa mpangilio wa kimataifa, ambao utaunda mahusiano juu ya kanuni zilizotajwa hapo juu. Suali la kimaumbile ambalo huzuka kuhusiana na mwelekeo wa mahusiano ya kimataifa lilikuwa; vipi ikiwa nchi moja au zaidi zimekataa kufuata kanuni zilizotajwa hapo juu katika utekelezaji wa mahusiano ya kigeni? Ilikubaliwa kuwa muungano wa Mataifa utahamasishwa kulazimisha taifa au mataifa pinzani kuregea kwenye kanuni zilizokubaliwa katika amani ya Westphalia. Hivyo, takwa la udumishaji katika mahusiano ya kimataifa yalio juu ya kanuni fulani limetowa fursa kwa hitajio la mamlaka ya kimataifa kuhakikisha kuwa udumishwaji huo unahakikishwa na kanuni hizo zinazingatiwa. Fikra hii ya kuhakikisha kujifunga kwa mataifa juu ya kanuni zilizokubaliwa katika Westphalia, kupitia uhamasishaji wa mataifa ya muungano ulibuniwa kwa kuudhibiti Uzani wa Nguvu, moja ya ufafanuaji wa usimamizi wa kanuni za nidhamu ya Mfumo mpya wa Kiulimwengu, mwanzoni ulipigiwa debe na Ulaya na baadaye Amerika, ambao kwa wepesi waweza kuchukuliwa kama ni ufahamu wa Westphalia wa Mfumo wa Kiulimwengu. Kongamano la Vienna lililofanyika 1814- 1815 lilipangwa kuuregesha nyuma Mpangilio wa Ulaya kwenye Mizani ya Nguvu wa kabla ya enzi ya Napoleon ambapo Uingereza, Austria, Prussia na Urusi ziliunda muungano wa Mataifa kuuzuia mpango wa Ufaransa wa upanuzi na kufanya marekebisho ya siasa kwa namna zinavyo athiriwa na jiografia, kama kuyaunganisha majimbo mengi ya Ujerumani kwa Prussia kuiongeza nguvu kama nchi, ili iweze kuzidhibiti Nguvu za Ufaransa katika Bara la Ulaya. Mashauriano ya pamoja ya Ulaya yanawakilisha Mizani ya Nguvu ya Ulaya katika hatua mbili, ya mwanzo kutokea 1815 hadi mwanzoni mwa miaka ya1860, na ya pili kutoka mwanzoni mwa miaka ya 1880 hadi 1914. Hatua ya mwanzo ya mashauriano ya Ulaya, yakijulikana kama Mfumo wa Kongamano au Mfumo wa Vienna baada ya Kongamano la Vienna (1814-15), ulitawaliwa na Mataifa matano yenye nguvu ya Ulaya: Australia, Ufaransa, Prussia, Urusi, na Uingereza. Zikihitaji kudhibiti Mizani ya Nguvu katika Ulaya, Ufaransa, Urusi na Uingereza zilitangaza vita dhidi ya Ujerumani vilivyopelekea Vita vya Kwanza vya Dunia baada ya tangazo la Ujerumani la vita dhidi ya Urusi. Na ilikuwa ni juhudi ya kuregesha Mizani ya Nguvu katika eneo la Ulaya na Asia kuwa katika hali yake ya mwanzo ya maandalizi ambapo Amerika, Uingereza, Ufaransa na Urusi ya Kisovieti ziliunda muungano wa nchi dhidi ya Ujerumani, Italia, na Japan katika Vita vya Pili vya Dunia kuangazia mipango yao ya utanuzi. Na ilikuwa ndio muundo wa Muungano wa Kaskazini ya Atlantiki katika Ulaya (NATO), uliokusanya mataifa ya Ulaya na Amerika uliokusudiwa kuweka Mizani ya Nguvu katika Ulaya dhidi ya utanuzi wa Usovieti na baadaye Urusi.

Fikra ya Mizani ya Nguvu katika uhalisia wake ilikuwa ni kielelezo cha uhalisia wa ukweli wa nguvu katika bara la Ulaya. Hakukuwa na utawala wenye nguvu katika Ulaya uliokuwa na uwezo peke yake wa kutosha kuitawala Ulaya yote. Japokuwa katika hali tofauti, mataifa tofauti yenye nguvu yaliweza kutawala mataifa mengine yalio na nguvu katika mapambano yao binafsi, ushindi kamili dhidi ya muungano wa mataifa yenye nguvu haukuweza kupatikana. Ilikuwa ni kielelezo hiki cha uhalisia wa ukweli wa nguvu katika Ulaya ambacho kimepelekea fikra juu ya operesheni ya Mizani ya Nguvu, iliotumika kwa ajili ya kumdhibiti na kumsimamia mkaazi wa Ulaya na kisha baadaye Mfumo wa Kiulimwengu.

Fikra ya ubwana wa Westphalia sio fikra isiobadilika yenye ukomo wa mipaka juu ya mipaka ya nchi. Bali ilikuwa ni kuzuia na kuangalia juu ya tamaa za Mataifa yenye Nguvu yalio na uwezo, hamu na tamaa ya kubadilisha mipaka yao binafsi na ya nchi zingine. Hivyo katika asili yake, fikra ya Ubwana wa Westphalia na dhana inayohusiana nayo ya Mizani ya Nguvu imetaka kugawa nguvu miongoni mwa Mataifa Makuu ya wakati husika; na sio lazima ugumu wa kuweka kikwazo juu ya utanuaji wa mipaka ya nchi na himaya zao. Hivyo, tunaona Urusi inaendelea kutanua mipaka ya nchi yake katika karne zote nne zilizopita.

Ujerumani imetanua mipaka yake mwanzoni na katika nusu ya mwisho ya karne ya kumi na tisa, wakati Ufaransa na Uingereza zikiendelea kutanua himaya zao Afrika, Asia na Amerika kuanzia karne ya 17 na kuendelea, kwa upande wake Amerika imeendelea kujitanua katika mipaka yake katika sehemu kubwa ya karne ya kumi na tisa. Utanuzi wote huo umekubalika muda wa kwamba Mataifa mengine yenye Nguvu hayakuhisi kuwa utanuzi huo ni tishio hatari kwa maslahi yao nyeti. Ilikuwa ni baada tu ya Vita vya Pili vya Dunia ndipo Amerika imepata ujasiri na kutoa uzingatiaji mkubwa zaidi wa mipaka ya mataifa, kama inavyotaka kushindana na Umoja wa Kisovieti na kuzuia utanuzi wake katika Ulaya Mashariki na Asia ya Kati.

Hivyo fikra ya Mamlaka ya Westphalia na dhana inayofuatia ya Mizani ya Nguvu inataka kuweka udumishwaji katika namna ya vipi maeneo tofauti ya Ulimwengu yanatawaliwa na vipi nguvu zinagawanywa duniani. Taasisi hii maalum ya mahusiano ya kimataifa sio matokeo yasiofikiwa ya maendeleo ya historia, bali ni uundaji wa makusudi wa mahusiano ya kimataifa katika sura ya mtazamo wa Wamagharibi kuhusu namna ya mahusiano kama haya kuweza kupangwa.

Kama ufahamu kamili wa Ulaya Magharibi wa kusimamia mambo ya dunia yalioibuka katika Ulaya Magharibi, kama yalivyo masuala mengi ya ustaarabu wa Kimagharibi, fikra ya Mamlaka ya Westphalia, kama ilivyoonyeshwa awali, ilitaka kusitisha au kuhifadhi hali ilivyo ya mgawanyo wa nguvu za Ulimwengu. Chombo kilichotumika kufikia mwisho huu kilikuwa ni imani ya mamlaka ambayo iliota mizizi katika jamii ilioshikamana kikabila au jamii ambayo ilikuwepo kihistoria kama ilioungana na ambayo iliishi katika eneo maalum la kijiografia kwa muda mrefu. Pia mamlaka ya Westphalia hayakudhaniwa kuwa ni fikra iliojengwa juu ya taasisi ya ndani ya jamii, bali ilikuwa ni fikra ilioendelezwa ilioegemea uhalisia wa jiografia ya kisiasa na mgawanyo wa nguvu kama ilivyopatikana katika Ulaya wakati wa amani ya Westphalia. Wakati himaya za Wazungu zilipo anguka, na Amerika na Umoja wa Kisovieti kuibukia ubwana wa ulimwengu, tawala hizi mbili zilisukumwa katika kumaliza ukoloni kupunguza na kuondoa ushawishi wa Ulaya katika masuala ya kiulimwengu. Wimbi hili la kuondoa ukoloni lilipelekea uhuru wa mataifa mapya kadhaa katika hatua ya kiulimwengu, ambayo ilizingatiwa katika desturi za mamlaka ya Westphalia. Hii imekuwa moja ya athari ya kimsingi katika taasisi ya mambo ya kiulimwengu, pamoja na kuligawanya vipande vipande eneo la awali la Dola ya Khilafah kuwa dola za kitaifa, ilioambatana na Makubaliano ya Sykes-Picot ya 1916. Fikra ya mamlaka ya Westphalia ilitanuliwa kuelezea taasisi za ndani za jamii, ambapo jamii mpya zilikatwa katika maeneo tofauti ya duniani ikiegemea juu ya dhana ya jamii, yakichipuka katika ukabila au kundi la makabila na ambalo limeunganishwa pamoja kuunda jamii mpya moja moja. Fikra hii ya jamii hata hivyo haikuwa mara zote ni kamilifu hata katika hali ambapo jamii mpya ziliundwa kutokana na makabila ya asili moja. Mshikamano wa utambulisho ulioegemea ukabila wa pamoja sio mshikamano pekee wala kuwa ni wenye nguvu ambao huiweka jamii pamoja. Jamii ni wazo pana zaidi la mkusanyiko wa mahusiano ya kudumu baina ya watu mmoja mmoja wanaoishi pamoja kwa muda mrefu. Kudumu huku katika mahusiano kunaenea katika mpangilio mpana wa mahusiano, unaoendelea katika uzima baada ya kuishi pamoja kwa kipindi cha kutosha, ikiisukuma jamii binafsi, iliotokana na mahusiano haya kuendeleza fikra, imani na vigezo, katika kudhibiti mahusiano haya na hatimaye kuteua mamlaka, yanayotawala jamii hii kwa mujibu wa imani ilioibeba. Imani hii ya jamii iliotanuka zaidi na kuzalikana kihistoria imekosekana kutoka mataifa mengi mapya yalioibuka juu ya fikra ya Mamlaka ya Westphalia. Kwa kukosekana mfumo wenye nguvu wa kuifunga jamii pamoja na ulegevu wa historia kubakisha udumishaji wa mahusiano ulioanzishwa kipindi kirefu, dola hizi mapya za kitaifa zilikuwa dhaifu katika hali nyingi na ni dhahiri kuwa sio la kimaumbile katika hali za nchi nyingi. Zaidi ya hayo, katika baadhi ya hali jamii hizi mpya zilikuwa na historia zilizotekeleza dhidi ya utendaji wao. Nyingi ya jamii hizi hazikuwa na uzoefu wa mamlaka halisi. Kihistoria zilikuwa zikiongozwa na himaya za jirani au Nchi Kubwa zenye nguvu na katika mazingira ya mamlaka ya ndani, yakiwa ni majimbo yanayosimamiwa na Mataifa Mkubwa au yakiwa mipakani mwa Mataifa Makubwa. Hata kama yalikuwa yakijitawala katika baadhi ya hali, kikawaida hayakuwa yakijisimamia au yalikuwa na uzoefu mdogo au mfupi wa sera za kigeni na kijeshi. Baadhi ya jamii hizi mpya hazikuwahi kuwa na uzoefu wowote wa kujitawala wenyewe na zilikuwa zikitawaliwa na Mataifa Makubwa ya wakati wao au yalipoteza utawala wao binafsi kwa muda mrefu kwa hamu ya utanuzi wa Mataifa Makubwa. Hivyo ilikuwa sio ajabu kwa dola hizi mpya za kitaifa kuwa dhaifu na kukumbana na tawala imara na masuala ya kiutawala. Katika hali nyingi Mataifa haya mapya yaliendelea tu na muundo wa uendeshaji wa kikoloni au kibeberu, na hazikuweza kujiendeleza kiasili na kuwa na muundo wa uhai na mifumo ya hukumu na utawala.

Hivyo kile ambacho dunia inakumbana nacho leo juu ya suala la “dola zilizofeli” na zilizo nyuma kimaendeleo “Ulimwengu wa Tatu” ni matokeo ya moja kwa moja ya ueneaji wa fikra ya Mamlaka ya Westphalia kuwa ya kiulimwengu na usisitizaji wa udumishaji wa mahusiano ya kimataifa yaliojengwa juu ya maadili ya wana wa Westphalia. Imepelekea maafa makubwa na kukata tamaa kwa mamilioni ya wanaoishi katika dola za kitaifa ambayo yalizingatiwa kuwa ni mapya, na katika hali nyingi yalikuwa kwa hakika, ni jamii za kubuniwa. Sio ajabu kuwa mengi ya mataifa haya yanakabiliana na masuala ya mshikamano wa ndani, ukiegemea juu ya changamoto kutoka kwa utaifa wa chini ulio imara, ambao unadai uhuru kutoka kwa mataifa mama, unaotegemea maadili ya wana Westphalia wa dola iliozalikana na ukabila. Mataifa mapya mengi hadi sasa, yanahitaji kujifunza utaifa mpana, kupitia sera za taifa zilizopangwa, kumfanya mtu ashangae kuhusu hekima ya kuundwa dola kama hiyo, ambayo hujaribu kutoa dhumuni na maana kwa jamii inayotawala baada ya kuwa imeshaundwa. Katika baadhi ya hali juhudi kama hizo za kujifunza utaifa mpana kuiunganisha jamii zimeendelea kwa miongo kadhaa, baada ya uanzishaji wa awali wa taifa hilo, bila ya mafanikio makubwa. Jambo hili la mataifa dhaifu na yalioshindwa yaliopo katika maeneo tofauti Ulimwenguni leo yanazidi kuunganisha na kuimarisha ushikiliaji wa Mataifa Makubwa juu ya masuala ya dunia. Zaidi ya hayo, inasaidia kuunganisha mgawanyo wa nguvu za kilimwengu baina ya Mataifa Makubwa, kitu ambacho mkataba wa Westphalia kiasili umeuzingatia.

Mtizamo wa haraka kwa masuala ya kiulimwengu hivi leo na Mataifa Makubwa yaliyoyaunda umefichua kuwa ufanisi na ushawishi muhimu wa Mataifa Makubwa ya leo umekuwa kihistoria ni jamii binafsi kwa kipindi kirefu. Na pia hii idadi ndogo ya mataifa yenye ushawishi ambayo yanaunda masuala ya kiulimwengu. Sehemu kubwa ya masuali ya leo ya siasa zinazoathiriwa na mambo ya kijiografia ambayo ni muhimu kwa usimamizi wa kiulimwengu wa masuala ya kimataifa na ambayo ni kitovu cha mashindano ya Mataifa Makubwa kwa hakika ni masuala yaliochimbuka katika historia na tamaa ya jamii hizi kongwe. Amerika inataka kuhifadhi ukubwa wake wa kiulimwengu kulingana na kwamba hakuna nguvu inayoweza kumiliki ulimwengu, bila kumiliki maeneo mawili pacha na yalioungana kijiografia ya Ulaya na Asia, yanayoitwa Eurasia. Hivyo, Amerika imetaka kuelezea masuala ya zamani ya siasa zinazoathiriwa na ushawishi wa kijiografia katika maeneo tofauti ya ulimwengu na kupitia suluhisho maalum kwa changamoto za siasa za kijiografia Amerika imejihakikishia ukubwa wake kiulimwengu. Katika Ulaya, Amerika imetaka kuepuka vita na mashindano ya siasa za kijiografia baina ya Mataifa tofauti ya Ulaya, ya mwanzo yao ni Ujerumani na Ufaransa, kwa kutoa ulinzi wake kupitia NATO, hivyo kupunguza hitajio lao kwa matumizi ya ulinzi na kukandamiza tamaa za masuala ya kijeshi ya nchi hizi. Amerika kwa makusudi ilitaka kuelekeza nguvu ya hizi jamii za kihistoria na za zamani kuelekea maendeleo ya kiuchumi kupitia uanzishwaji wa Muungano wa Ulaya, hivyo kuziondoa kutoka katika kuwa na tamaa ya siasa za kijiografia zao wenyewe. Hivyo hivyo, Amerika inataka kuidhibiti Urusi ambayo imeendelea kujipanua kwa karne nne na kihistoria imetaka kuwa na hadhi na utambulisho kuwa ni Taifa Kubwa kupitia ushindi wa kijeshi na kujipanua. Hivyo, uundwaji wa NATO na Muungano wa Ulaya zimeipatia Amerika malengo pacha ya kudhibiti nguvu za Ulaya na kuzuia tamaa za utanuzi wa Urusi kwa kudhibiti Mizani ya Nguvu katika Ulaya. Katika eneo la Mashariki ya Mbali ukingoni mwa Eurasia, historia ya changamoto ya siasa za kijiografia imekuwa ni taifa chokozi la Japan na mahusiano yake na majirani zake na jamii ya zamani ya Kichina ambayo inataka ukubwa na hadhi kwa ustaarabu wake. Amerika inataka kuisimamia Mashariki ya Mbali kupitia mkataba wa kijeshi na Japan, ambao unafanya kazi zote mbili, kudhibiti uchokozi wa Japan na kuelekeza nguvu za Japan kwenye maendeleo ya kiuchumi. Pamoja na uwepo wake wa kijeshi katika Japan na Korea, Amerika inahitaji kuweka Mizani ya Nguvu katika Mashariki ya Mbali kudhibiti ukuaji wa China na kuizuia kuwa na ushawishi mkubwa duniani. Katika eneo la pembeni la kusini mwa Eurasia, katika Ghuba la Uajemi, Amerika inahitaji kudhibiti, kupitia uwepo wake hapo, kudhibiti rasilimali ya nishati za eneo na kuzuia kuibuka kwa Dola ya Kiislamu juu ya eneo kubwa la siasa za kijiografia lililoenea katika ardhi za Waislamu. Katika kufanya hivyo, kama ilivyo katika maeneo mengine ya dunia, Amerika inafahamu fika juu ya historia ya eneo hili na changamoto za historia ya siasa ya kijiografia ilizozileta. Na pia katika eneo hili, ambapo jamii kongwe ya karne nyingi, iliotawaliwa na Dola ya Kiislamu kuvunjwa na kuwekwa dola mpya kadhaa za kitaifa za Westphalia zilizoelezewa kabla. Ni kutokana na hofu hii ya historia, ya ujasiri na hali ya uzito wa jamii binafsi kongwe, zilizoasisiwa, ambazo zinaendelea kuilazimisha Amerika na Magharibi kuichukulia Mashariki ya Kati na Ulimwengu mpana wa Waislamu kama changamoto ya siasa ya kijiografia, ambayo ina uwezo wa kubiruwa au kuleta mageuzi ya kimsingi ya Mfumo wa Kiulimwengu.

Historia ya jamii ina jukumu kubwa katika kuamua ushawishi wake wa kiulimwengu. Hadi pale itakapovutiwa na fikra yenye nguvu ambayo huweza kugeuza sura yake ya jamii kimsingi, kwa ukamilifu na kwa kina na ambayo hugeuza taasisi ya mahusiano ya kudumu yanayopatikana katika jamii, jamii za wanaadamu kwa kawaida huelekea kuegemea juu ya mizizi ya kihistoria kutafuta ujasiri na kuandaa uwezo wa kuongoza nguvu zao za ubunifu na tamaa katika kuelekea kutaka hadhi ya kiulimwengu na ushawishi. Kwa hakika inaweza kudaiwa kwamba ilikuwa ni maandiko ya kidini tu ambayo awali yaliubadilisha Ulimwengu wa Ulaya kwa kiasi kikubwa na sehemu ya Mashariki ya kati, na baadaye Uislamu ambao ulilazimisha jamii kuacha imani zao zilizopita na kuchukua imani mpya moja kwa moja na misheni ya maisha. Japokuwa Umoja wa Kisovieti ulichukua itikadi mpya iliobuniwa na akili ya mwanaadamu ambayo iliigeuza moja kwa moja jamii ya Urusi, Ukomunisti ikiwa ni fikra ya mageuzi ya kimsingi ni kweli tu imeivutia jamii ya Wasovieti katika zama za Lenin na Stalin. Mapema zaidi katika zama za Nikita Khrushchev, anaye chukuliwa kumiliki Umoja wa Sovieti kuwa ni kiongozi mwenye nguvu baada ya kifo cha Stalin mwaka 1953, sera za nje za Usovieti zilianza kuelezea malengo ya sera za Urusi za kigeni zilizochipuka zaidi kihistoria, kutaka kuwa na hadhi na ushawishi kwa jamii ya Warusi kuliko kueneza fikra za Kikomunisti, ambazo watangulizi wake wawili wenye nguvu walifanya.

Ama kwa vipi historia inacheza dori yake muhimu kwa takwa la jamii la ushawishi wa kiulimwengu, sababu ya mwanzo ni kuwa umashuhuri wa jamii kihistoria katika kiwango cha ulimwengu unaipatia jamii hisia ya ubwana na kujiamini katika uwezo wake wenyewe na nguvu, ambayo inaelezea tamaa ya jamii kwa ajili ya nguvu za kiulimwengu. Nguvu za kiulimwengu hutakiwa na mataifa kuthibitiisha hisia zao dhidi ya wengine, kutaka mali na unyonyaji wa rasilimali nje au katika huduma ya ujumbe unaoelezewa na mfumo. Kuwa kwake kihistoria kuwa ni mchezaji muhimu aliye na ushawishi kunaweza kusisimua vyote vitatu, au japo moja ya hizi tamaa. Pili, jamii zenye historia ndefu za uwepo kama jamii binafsi zisizovunjika huwa zinaunda taasisi zisizotegemea sana juu ya umahiri wa mtu na uwezo wa watu binafsi kutenda mambo, kuimarisha uwezo unaohitajika kwa ajili ya nguvu za kiulimwengu na ushawishi. Uwezo huu kama nguvu za kijeshi na kiuchumi, uvumbuzi wa teknolojia na utamaduni wa kipekee ambao unazalisha hisia za ujumbe na dhumuni katika jamii hizo. Historia ndefu ya ushiriki wa kijeshi mara nyingi huleta vizazi vya wapiganaji na utamaduni wa kutukuza uwezo wa kupigana na ambao unathamini na kuheshimu wapiganaji kuwa ni watu wa daraja kubwa. Pia jamii kama hizo huwa zenye bidii kubwa katika uzalishaji wa vifaa vya kijeshi. Kipindi kirefu cha neema na historia ya uvumbuzi huleta hisia ya uwezeshwaji wa kisiasa na shauku, ambapo utajiri huweza kuleta katika jamii pamoja na imani juu ya ubora wa juhudi katika kazi na utamaduni wa kuwa na bidii, ambayo huimarisha nguvu za uzalishaji katika jamii hiyo. Muendelezo wa ushiriki katika masuala ya kilimwengu hujenga taasisi ya viongozi wa kisiasa na wana fikra wanaoweza kuzingatia juu ya urithi unaoendelea wa uzoefu wa kisiasa na utaalamu, ulioenea kwa karne nyingi nyuma, katika juhudi zao za kusimamia masuala ya ulimwengu hivi leo. Hata hivyo, huenda suala muhimu zaidi la hisia ya kihistoria ya ujumbe ambao jamii huweza kuwa nao, ni kwa sababu ya vizuizi vya kiutamaduni. Kwa upande wa kikabila jamii ya kiasili na ya zamani, yenye utamaduni unaothaminisha mashujaa wa vita na ambao huadhimisha utawala msonge ambao wafalme wa Japan huonekana kuwa wanamiliki nguvu za Kiungu, hisia ya Japan ya ubwana wake imeifungulia nguvu za kuwa ni taifa kubwa kijeshi na kiuchumi. Hata hivyo, kutokana na kutoweza kwake kuuwakilisha utamaduni wake kwa ulimwengu kuubeba na kutowezekana kwa dunia kuukubali, ushawishi msingi wa siasa wa kijiografia wa Japan ulikuwa na ukomo, utamaduni na fikra zinazoelezea ujumbe, thamani yake na utambulisho wa jamii hiyo na sababu za kuwepo kwake. Pia uwezo wake wa asili wa utamaduni huu kuwa ni wa kuenea zaidi kwa watu jumla katika maumbile yake ambapo hatimaye huielezea jamii au ushawishi wa kiulimwengu wa taifa kwa utamaduni na fikra ndio vipengele muhimu zaidi visivyopewa umuhimu na mataifa yenye nguvu. Japokuwa, kuwa kwake kihistoria ni taifa kubwa chokozi la kijeshi na lenye nguvu kubwa za kiuchumi hivi leo na kuwa na uwezo wa kiviwanda kwa ajili ya muendelezo wa haraka na muhimu wa kijeshi, Japan imebakia kutoweza kuelekeza nguvu zake kieneo.

Moja ya himaya kubwa zaidi ya ardhi ilioshikana katika historia ya Ulimwengu ilianzishwa na wapiganaji mahiri zaidi wa Kimongoli chini ya uongozi wa Genghis Khan, ambao iliangamiza mataifa mengi makubwa ya zama zake na ambao baadaye walishindwa na Saif ad-Din Qutuz, mtawala Mamluki wa Misri, baada ya kufanya maangamizi ya kuibomoa Dola ya Kiislamu na kumuua Khalifah wa Abasiyya katika Baghdad. Japokuwa utawala wao ulienea katika ardhi kubwa, ukosefu wa upekee au utamaduni wowote wa maana au fikra zinazoweza kuwajumuisha watu jumla kuwa ni kitu cha kuelezea Himaya ya Mongoli, ilimaanisha kuwa Himaya ya Mongoli na utawala hatimaye ulimezwa na sehemu za nchi ambazo ziliishinda na ambayo ilikaliwa na watu walio na utamaduni wa juu Zaidi. Hivyo himaya ya Mongoli imejibagua kuwa Khanate ndogo ndogo, ambapo Khanate za Magharibi wamefuata Uislamu na kuimiliki Asia ya Kati. Moja ya vitu vyenye kuelezea ukuaji wa Uislamu kuwa na ushawishi wa kiulimwengu na karne nyingi za utawala wa kiulimwengu ulikuwa ni utamaduni wenye hadhi iliokuwa nao, ambao umeipeleka katika Dunia na ambao umeisaidia kuiunganisha utawala wake katika maeneo mapya yaliokombolewa. Ilikuwa ni kuenea kwa utamaduni wa Kimagharibi na mvuto wake katika bara la Ulaya ambayo imesaidia Amerika kuzuia ushawishi wa Urusi katika Ulaya na hatimaye kuishinda katika ushindani wao wa ushawishi dhidi ya Ulaya. Ilikuwa ni ueneaji wa utamaduni wa Kimagharibi ambao iliunganisha ukoloni wa Ulaya kote duniani, ikiwemo ardhi za Kiislamu. Ni kama ilivyo tu athari ya utamaduni huu katika ardhi za Kiislamu kupungua na utamaduni wa Kiislamu ulio mkubwa zaidi kujiimarisha wenyewe ndani ya jamii ya Waislamu katika ardhi za Kiislamu ambao Wamagharibi imewaongezea hofu yao ya kuiregesha Khilafah kwenye ardhi za Waislamu.

Uoni wa Uislamu kuelekea mahusiano ya kimataifa unalingana na maumbile na uhalisia wa mahusiano ya kimataifa. Uislamu hautaki kuingiza Mfumo wa Kiulimwengu duniani ambao unaweza kujengwa tu juu ya muundo wa kudumu wa mahusiano ya kimataifa. Katika muktadha huo Uislamu unapinga dhana yoyote ya Mfumo wa Kiulimwengu, ambao umeegemea juu ya taasisi ya muundo rasmi wa mahusiano ya kimataifa, hatimaye kupelekea kusimamisha taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa. Badala yake, Uislamu unaangalia mahusiano ya kimataifa kupitia uoni ulio hai zaidi wa namna jamii inavyojiangalia yenyewe. Hivyo Uislamu unaigawa Dunia katika Dar ul Islam (ardhi ya Uislamu) na Dar ul Harb (ardhi ya Kivita). Mtazamo huu kuelekea mahusiano ya kimataifa unaiangalia Dunia kutokana na imani yake yenyewe ya kuwa ni jamii ya Kiislamu. Ummah wa Kiislamu umebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa jukumu la kuwa ni wabebaji Da’wah. Da’wah hii hupelekwa kivitendo kote ulimwenguni, kupitia kusimamishwa kwa utawala wa Uislamu juu ya jamii mpya, ambazo si tu hupokea wito wa Uislamu kwa mdomo na maandishi tu, kuvutia vipawa vyao vya fikra, bali wito wa Uislamu unaoonekana na wa kivitendo, wanapochunguza sheria za Uislamu zikitawala kwa vitendo na kusimamia mambo yao, ambao wanashuhudia kuwa ni bora kuliko mifumo ya utawala iliopita ambayo huishi chini yake. Kwa namna hii, Uislamu huitangaza Da’wah kwa uzima wake kwa watu kwa nafasi yao ya kama watu binafsi, pamoja na watu kwa nafasi yao kama wanachama wa jamii. Hivyo, Uislamu unatumia sera ya ushawishi mpana, mvuto kwa hisia za watu binafsi na kuelezea uwezo wake kifikra pamoja na kuelezea hisia za jamii na fikra zake zinazotawala. Uislamu unahukumu kuwa katika uwasilishaji huu wa Da’wah ya Kiislam, mpokeaji wa Da’wah kama ni mtu binafsi, bado anabakisha matakwa yake na chaguo katika kukubali Dini mpya kwa hiyari yake mwenyewe. Hivyo uoni wa Uislamu kwa Ulimwengu unaigawa dunia katika maeneo, ambayo yanatawaliwa na Uislamu na maeneo ambayo yanatawaliwa na sheria zisizo za Kiislamu. Kupitia Jihad, Uislamu unataka kutanua mipaka ya Dola ya Kiislamu na hivyo sheria za Uislamu kiukamilifu, unapinga udumishaji wowote katika mahusiano ya kimataifa. Uislamu hautaki kusambaza nguvu za kiulimwengu miongoni mwa Mataifa Makubwa Duniani, wala kuweka Mizani ya Nguvu katika mahusiano ya kimataifa. Inapinga taasisi za kimataifa kwa sababu unakataa udumishaji wowote katika mahusiano ya kimataifa na mamlaka yoyote ya Dola nyengine juu ya kutekeleza mambo ya Dola ya Uislamu katika utekelezaji wake wa sera zake za nje. Sera ya Uislamu kuelekea dunia ni ile sera inayoegemea vita. Hadi hapo Dola ya Kiislamu itapokuwa tayari kwa makabiliano ya kijeshi na baadaye kutanua utawala wa Kiislamu kwenye jamii nyengine, Uislamu unayaangalia mahusiano ya kimataifa kuwa ni matendo ya hiyari ya kisiasa na kijeshi kwa Mataifa, ambapo serikali zinaruhusika kuchukua tendo lolote au matendo yote, bila kulazimishwa au kutumia nguvu. Yako huru kujiunga kwa hiyari na kuwa na hiyari ya kutojiunga katika mikataba ya pande mbili na ya pande nyingi na jamii zote za kigeni, ima zenye nguvu au dhaifu, muda wa kuwa ni jamii huru, huzingatiwa kuwa ni sawa katika muktadha wa haki zao kutenda katika mawanda ya kimataifa, kulingana na imani zao wenyewe na maslahi. Hivyo Uislamu unaangalia mahusiano ya kimataifa kuwa ni ya muda, yanayoweza kubadilika na katika hali ya kutotabirika na utekelezaji wa imani za dola yenyewe. Bila ya sheria za kulazimisha za kimataifa, au utamaduni wa kimataifa, au hisia ya uwajibikaji wa lazima kupitia kuwa ni sehemu ya jumuiya kubwa ya kimataifa.

Uislamu hata hivyo unakubali kujifunga kwa Serikali ya Kiislam katika upeo mdogo zaidi wa kanuni za kimataifa, kama haki ya kinga ya kidiplomasia kwa mabalozi au haki inayohusiana na baadhi ya sheria za vita. Hata hivyo kanuni kama hizo zinazingatiwa na Serikali ya Kiislamu na serikali nyengine kwa sababu ya kujifunga kimaadili na hofu ya rai jumla na kujitweza, na sio kwa kutwezwa nguvu yoyote. Dola ya Kiislamu iko huru kufunga mikataba pamoja na Mataifa mbali mbali, ambayo huilazimisha Dola ya Kiislamu kwenye amani na suluhu pamoja na dola nyengine yoyote kwa kipindi maalum, ili mradi mkataba huo wa amani unahudumia maslahi ya Uislamu na Waislamu. Hairuhusiki kwa Dola ya Kiislamu kuweka miungano ya kijeshi pamoja na Mataifa ya kikafiri, kwa kuwa hairuhusiwi kwa Waislamu kupigana kuilinda taasisi ya kikafiri. Kupigana katika Uislamu ni kwa ajili ya kusimamisha utawala wa Kiislamu tu. Inaruhusika kwa Dola ya Kiislamu kutekeleza matendo ya kisiasa na kufunga mikataba ya ujirani mwema pamoja na dola nyengine, kutumia nguvu zake na ushawishi kufungua fursa katika dola hizi kuunda rai jumla chanya kwa ajili ya Da’wah ya Uislamu. Hivyo, uoni wa Uislamu wa mahusiano ya kimataifa umejengwa juu ya uenezaji wa Da’wah ya Uislamu kwa jamii nyengine, ambapo jamii kama hizo zimeunganishwa chini ya mamlaka na utawala wa Dola ya Kiislamu kupitia Jihad. Endapo kwa sababu yoyote ya busara au kulazimisha, Dola ya Kiislamu haitoweza kuunganisha jamii hizi chini ya utawala wake, jamii kama hizo huzingatiwa kuwa ni jamii huru ambazo zinaruhusiwa kwa hiyari kufanya mahusiano ya kimataifa, bila ya kutezwa nguvu. Dola ya Kiislamu inaweza kuingia katika mikataba na jamii kama hizo zote, hadi inapokuwa tayari kuziunganisha chini ya mamlaka yake.

Ummah wa Kiislamu hivi leo uko katika nafasi ya kipekee kuhuisha hadhara ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (saw). Una faida ya kumiliki mfumo wa Kiislamu, pamoja na ufahamu sahihi hivyo unakuwa na mjumuiko wa fikra za mabadiliko ya kimsingi, ambayo ndio pekee yaliyotumika kihistoria kubadilisha njia ya historia. Nayo pia yana faida ya historia imara na ilio na nguvu ya historia ya utawala wa Kiislamu, ulioenea kwa zaidi ya miaka elfu moja, wenye urithi wa taasisi kutoka zama hizo, ambao unatumika kuimarisha kujiamini kwake katika uwezo wake kurudisha nafasi yake katika Ulimwengu kuwa ni mshiriki muhimu wa kumiliki masuala ya dunia. Taasisi kama zile za kithaqafa za Fiqhi ya Kiislamu na thaqafa pana ya Kiislamu, ambazo kutiliwa nguvu kwake na kuhuishwa kumetumikia katika kuhudumia kuuweka wazi ufahamu wa Ummah wa fikra, taasisi ya Jihad na utayari wa kupigana na adui hata kwa namna za uchache, hisia yenye nguvu ya umoja iliyoundwa na utambulisho wa Kiislamu wa kuwa ni Ummah mmoja na hisia ya ukubwa wa kuwa na thaqafa ya kidini ilioletwa kupitia Mtume wa mwisho, Bwana wetu Muhammad (saw), yote hayo yanauweka Ummah wa Kiislamu juu ya mataifa mengine kuwa ni mrithi wa ujumbe wa Mitume (as), unaozalisha kujiamini katika uwezo wake kukabili shida kubwa unaotokana na historia yake na ushindi wa karibuni zaidi dhidi ya maadui zake.

Kutoendelea kwa utawala wa Kiislamu kwa zaidi ya karne moja hata hivyo, kumevunja kabisa taasisi nyeti iliyo muhimu kwa utawala wa ulimwengu. Uwepo wa tabaka la kisiasa na kifikra ambalo limechukua uzoefu, mijadala na fikra zinazohusiana na umiliki wa historia ya Uislamu na ambayo linaweza kuisoma, kuitafakari na kuweka maoni juu ya umuhimu wa masuala ya kieneo na kiulimwengu kupitia nuru na huduma ya ujumbe wa Dola ya Uislamu katika masuala ya Dunia. Ilikuwa kudhoofika huku kwa chombo cha kisiasa cha Kiislamu ambacho kimepelekea kudhoofika kwa Khilafah ya Uthmani na hatimaye kuvunjika kwake. Baada ya ukoloni kujikita katika ardhi za Waislamu, kwa makusudi ililenga chombo hichi cha kisiasa cha zamani na kifikra katika ardhi za Waislamu na ikakiondoa kabisa, ikakiwekea tabaka la watawala, ambao wameleleka katika tamaduni na historia za Kimagharibi. Tabaka tawala hili lilitaka kuielezea na kuitafsiri historia ya Muislamu kwa maslahi ya muendelezo wa ukoloni katika ardhi za Waislamu, hivyo kuinyima jamii ya Waislamu uzoefu wa kihistoria na kujiamini kutokana na kipindi kirefu cha utawala wa kiulimwengu. Hii imetutenga kutokana na asili ya historia yetu na thaqafa yetu kuwa ni dola kiongozi wa Ulimwengu huenda imekuwa ni ushindi mkubwa zaidi dhidi ya ardhi za Kiislamu. Ni baada tu ya Ummah kukabiliana na mtengano huu na kuungana tena na shina lake ndipo sasa utakuwa umemakinika katika njia ya kuhuika. Hata hivyo, Ummah unabaki umenyimwa chombo cha kisiasa cha Kiislamu na manufaa ya urithi wa kuendelea wa wanasiasa, wanaopitisha maarifa yao na uzoefu wa siasa ya kijiografia, kwa kuzingatia changamoto ngumu zaidi za siasa za kijiografia za Ulimwengu. Pengo hili lilieleweka, kwani baada ya kuangushwa kwa Dola ya Khilafah, Ummah ulipoteza lengo lake, dhumuni na matarajio ya kuwa ndio dola kiongozi katika masuala ya Kiulimwengu. Ikatawaliwa baadaye na watawala waliokuwa watiifu kwa maslahi ya Wamagharibi. Zaidi ya hayo Wamagharibi waliwauwa au kuwabadilisha watawala mahiri wa Kiislamu wa zamani. Ilikuwa ni katika Uturuki na Iran tu, ambapo baadhi ya wakongwe hao walibakia kwa kiasi fulani. Hata hivyo, tabaka la viongozi wa Kiislamu hata katika nchi hizi, chini ya ushawishi wa tamaduni za Kimagharibi, jukumu lao la kusimamia na kushawishi masuala ya kiulimwengu limezuiwa moja kwa moja, hivyo kufuta moja kwa moja chombo cha kisiasa cha Kiislamu kutoka katika Ulimwengu wa Kiislamu. Tunataraji na kuomba kuwa katika juhudi za kufafanua na kubainisha kwa upana kufahamu matukio ya kisiasa katika Ulimwengu, katika mtazamo wa maslahi ya Uislamu na Waislamu, Hizb ut Tahrir na Mashabab wake, ambao wana ufahamu madhubuti katika masuala ya kimataifa, kuwa wanahudumia kuhuisha taasisi nyeti, kuunda jukwaa la kisiasa za Kiislamu na kundi (makada) la viongozi wa dola, ambao watahudumu kama nguzo ya Dola ya Kiislamu itakayosimamishwa hivi karibuni, inayolenga kujikita katika masuala ya kimataifa kwa lengo la kuwa ni dola kiongozi na kuwa ni mnara wa mwangaza na uongozi kwa wanaadamu wote,

[وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا]

“Na hivyo hivyo tumekufanyeni muwe Ummah wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe shahidi juu yenu.” [Al-Baqarah-143]

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mhandisi Moez – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 28 Julai 2020 18:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu