Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Miaka 97 ya Kuomboleza na Kutaabika Chini ya Idhilali ya Ukoloni wa Urasilimali

Kwa takriban miaka 1300 ya kuishi chini ya usimamizi wa Khilafah, Ummah huu ulifurahia amani, utulivu na ufanisi katika muda wote huo. Lakini, kila kitu kilikoma mnamo 28 Rajab 1342 H sawia na 3 Machi 1924 pindi wanafiki na wapatilizaji fursa walipotongozwa na thaqafa ya kikafiri na kuvutiwa na mfumo wake wa kimaisha wakiongozwa na Mustafa Kamal. Walitekeleza njama za Wamagharibi, waliotaka kuvunjwa kwa Khilafah wala kutosazwa chochote katika ukumbusho wake kwani huenda kikawa kichocheo cha Mwamko wa Kiislamu. Walifaulu katika kuiondoa Khilafah lakini, Imani ya Waislamu na Dini yao haikuondolewa badala yake ilichochea wimbi la uchukivu kwani ni kinyume na Uislamu kuishi pasi na Khilafah kwa kuwa ndio ngao ya Ummah huu na hivyo mambo yake husimamiwa na kupelekwa kwa mfumo huu wa Kiislamu. Kama ilivyo simuliwa kuwa Rasulullah (saw) asema:

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

Hakika, Imam ni ngao, watu hupigana nyuma yake na kujihami nayoIndeed. [Muslim]

Wamagharibi kupitia mfumo wao muovu wa kirasilimali mpaka leo wanaendelea kusababisha ghasia katika ardhi zote za Waislamu na kuugawanya Ummah ambao mwazoni uliungana pamoja kuwa vijidola vidogo vidogo kila mojawapo kikitawaliwa na mtawala kibaraka wa wakoloni anaye zungukwa na duara la wasaidizi wake ambaye Qibla chake ima kiko London au Washington. Watawala hawa vibaraka wa wakoloni kwa usaidizi kutoka kwa mabwana zao wameleta maafa baada ya maafa. Maafa haya yanajumuisha miongoni mwa mengine kuupa Uislamu sura mpya ya kileo ili ukubaliane na maadili ya mabwana zao wa Kimagharibi, wakiwabandika majina na kuwafunga gerezani Waislamu wanaolingania mwamko wa Kiislamu kuwa magaidi au waliovuka mipaka. Wakitabikisha kila aina ya sera zinazo ashiria ushawishi wa Wamagharibi kwa vidola hivyo katika sekta zote kuanzia biashara – zinazo endeshwa kwa misingi ya riba, jamii inayo endeshwa kwa misingi ya uhuru, na siasa bandia – zisokuwa na sera ya kigeni na viwanda – vinavyo endeshwa kwa misingi ya ubinafsishaji nk.

Watawala vibaraka hawa walisonga mbele zaidi katika kuwaabudu mabwana zao kufikia kiwango cha kutoa nafasi kwa amali za majeshi ya Kimagharibi zilizo lengwa ndugu zao huku wakijitia upofu wanapo elekezwa kuangalia uharibifu wanaoutekeleza. Maisha yamekuwa magumu mno chini ya idhilali ya watawala vibaraka wa wakoloni ambao wako katika hali ya wazimu na kutapatapa kuokoa viti vyao mamlakani kupitia kumaliza tishio lolote la hali halisi yao. Huku ulinganizi wa mwamko wa Kiislamu ukifikia kilele chake, imepelekea watawala vibaraka na mabwana zao wakoloni kuwahadaa watu kwa kuuonesha Uislamu kama mfumo katili, ambao hauwezi kuwa badili ya mfumo batili wa kirasilimali. Wamefaulu katika kujidanganya wenyewe na wale walioko pambizoni mwao ama kwa wengi wa watu wakiwemo wale walioko eneo la Magharibi na ulimwengu mzima wa Kiislamu kamwe hawaja kubali ujanja wao na kwa hivyo njama zinafichuka mbele ya macho yao huku watu wakisilimu na ulinganizi wa mwamko ukizidi kufikia kileleni kila uchao kwa fadhila na rehma za Allah (swt):

  كَتَبَ اللَّـهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي ۚ إِنَّ اللَّـهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴿

“Allah ameandika: Hapana shaka! Mimi na Mitume yangu tutashinda. Hakika Allah ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” [Al-Mujaadalah: 21]

Hakika, kwa miaka tisiini na saba, tumekuwa tukiomboleza na kutaabika chini ya idhilali ya ukoloni wa urasilimali; kuanzia Mashariki ya Kati, Afrika, Asia, Latin Amerika nk. Watu wametabanni mwito wa maisha uchungu unaosema: ‘jana ilikuwa bora kuliko leo’ huku majambazi wa kirasilimali na makampuni yao ya kimataifa wakiwatafuna kila uchao kwa sera za kinyama zinazo lenga kuwatapeli rasilimali zao nyingi. Kila dakika inasonga kwa kufichuka kwa majaribio tasa ya kujaribu kuuokoa uhalisia wa kuporomoka kwa mfumo muovu wa kisekula wa kirasilimali unaosubiri mazishi wakati wowote hivi kuanzia sasa. Nyoyo zetu zinapiga kwa macheo mapya, ambayo dalili zote zinaashiri kukaribia kwake kwa kasi. Macheo haya mapya chini ya uongozi wa Khilafah itakayo simamishwa katika njia ya Mtume (saw) hayana shaka kama ilivyo bashiriwa na Mtume Muhammad (saw) katika hadith maarufu:

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً ، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ»

…kutakuwepo na tawala za kiimla kwa muda apendao Allah kuwepo kwake.” [Ahmad]

Zaidi ya hayo, Allah (swt) ameahidi ushindi:

﴿وَعَدَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴾

“Allah amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na wakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu”.  [Nur: 55]

Na Yeye (swt) pia anasema:

 ﴾وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿  

“Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu (washindi) ikiwa nyinyi ni waumini (wa kweli)”. [Al-Imran: 139]

Kwa bishara ya Rasulullah (saw) na ahadi kutoka kwa Allah (swt) Ummah wa Kiislamu ni lazima kutokaa na kungoja tu mambo yajitokeze, badala yake, ni lazima tubakie imara na wakakamavu katika ulinganizi wetu wa mwamko wa kweli wa Kiislamu unaolenga kurudisha mfumo kamili wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah kwani ni kupitia kwayo pekee ndio hadhi ya Ummah huu na heshima yake itakapo patikana. Khilafah itawakomboa sio tu Waislamu pekee bali pia Wasiokuwa Waislamu na wanadamu wote kwa jumla kutokana na njama za mfumo batili wa kikoloni wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazo nuka zitokamanazo nao ikiwemo nidhamu ya kiutawala ya kijambazi ya Kidemokrasia. Allah (swt) asema:

  وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ﴿

“Na hatukukutuma (Ewe Muhammad), isipokuwa uwe ni rehma kwa walimwengu wote”. [Al-Anbya: 107]

Wakati umewadia sasa mujiunge ikiwa bado hamujafanya hivyo na kazi ya kulingania ukombozi wa kweli unaoongozwa na Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislamu ambacho hakiogopi wala kuficha maneno yake dhidi ya watawala vibaraka wa wakoloni na mabwana zao wakoloni inapo kuja katika kuamrisha mema (kheri) na kukataza maovu (munkar) huku macho yake yakiangazia na kulenga kusimamisha tena Khilafah Rashidah katika njia ya Mtume (saw).

Enyi Vijana wenye ikhlasi wa Ummah wa Kiislamu,

Ambao kwa sasa muko katika kambi za kijeshi, ndugu zenu na dada zenu nchini Kashmir, Palestina, Syria, Somalia nk, wanawalingania kuipa Nusra (usaidizi wa kijeshi) Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah ambayo itawakomboa kutokana na mateso yao na kwayo itaunganisha Ummah huu, majeshi yake na ardhi zake na kuanza kulingania Da’wah ya Kiislamu ulimwengu mzima. Je, hamupendi kutambuliwa kama Saad ibn Mu’adh (ra) alivyo kuwa pindi alipo fariki arshi ya Allah ilitingishika na ambaye milango ya pepo ilifunguliwa kwa ajili yake na mazishi yake kushuhudiwa na malaika ambao hawaja wahi kushuka ardhini isipokuwa siku hiyo na kwenda haraka kwa ajili ya kushindana katika kushiriki katika mazishi yake na kupata daraja yake kwa heshima na unyenyekevu kwake? Au mumechagua kutumiwa kama vikaragosi katika vita vya wakala vya kiulimwengu ambavyo matunda yake ni fedheha duniani na Jahannam kesho Akhera? Macheo yamewasili baada ya miaka 97 Allah (swt) angali amewapa fursa muandikwe katika historia kama alivyo kuwa Khalid bin Walid (ra). Zikomboeni nafsi zenu kutokana na utiifu kwa watawala vibaraka wa wakoloni na kumbatieni mwito wa Allah (swt) na Mtume wake (saw):   

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿

“Enyi mulio amini! Muitikieni Allah na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Allah huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa”. [An-Anfal: 24]

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 28 Juni 2020 07:12

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu