Ijumaa, 27 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Uingereza ni Nchi ya Ajabu ambapo Watu Mabubu Huamini Mambo Yasiyo na Maana na Wenye akili Hutishiwa ili Kukubaliana nayo

Kichwa cha habari cha gazeti la ‘The Guardian’ mnamo tarehe 16 Februari 2024, kilichoandikwa na Gaby Hinsliff, kilisema: "Jifunze hili kutokana na mzozo wa Rochdale: jamii inakabiliwa na hatari pindi watu werevu wanapoamini mambo yasiyo na maana."

Soma zaidi...

Mauaji ya Halaiki ya Kimya nchini Congo: Kimya cha Magharibi na Usaidizi kwa Jina la Faida

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nyumbani kwa usambazaji mkubwa zaidi wa cobalt, chuma muhimu kinachotumika katika utengenezaji wa betri za lithiam-ion kwa ajili ya simu, tablets na magari ya umeme. Mnamo 2022, akiba ya cobalt ya Congo ilikadiriwa kuwa karibu tani milioni nne za metric, ambazo ziko mashariki mwa nchi, huku akiba ya kimataifa ikiwa ni tani milioni 8.3.

Soma zaidi...

Unafiki wa Ulimwengu wa Kimagharibi: Uamuzi wa ICJ juu ya 'Israel' na Madai ya Uhusiano wa UNRWA na Hamas

Uwanja wa kimataifa mara nyingi hushuhudia dhihirisho la unafiki, hasa linapokuja suala la hatua za dola za Magharibi katika kushughulikia mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Matukio mawili ya hivi majuzi, kwa mara nyengine tena, yameleta jambo hili katika mwelekeo mkali: uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu 'Israel' ambao ulianzishwa na Afrika Kusini mnamo Disemba 29, 2023, na madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na 'Israel' kuhusu UNRWA (Shirika la Umoja wa Mataifa la Usaidizi na Kazi kwa Wakimbizi wa Palestina)  kuwa na mafungamano na Hamas.

Soma zaidi...

Katika Nchi Ambayo Inadai Kulinda Haki za Wanawake, Wabebaji Dawah Wanawake wa Hizb ut Tahrir Wanakamatwa kwa sababu Wanafanya Kazi Nje ya Mfumo wa Kisekula!

Mnamo jioni ya Ijumaa, 02/02/2024, mbele ya Msikiti wa Al-Lakhmi katika mji wa Sfax, wanawake wawili kutoka Hizb ut Tahrir walikamatwa katika mazingira ya kusambaza taarifa ya kuinusuru Gaza. Kabla ya hili, kulikuwa na uvamizi katika nyumba ya mmoja wa wanawake mashabaat wa Hizb katika mji wa Hammamet siku ya Ijumaa iliyopita, tarehe 26/01/2024, ambapo jeshi kubwa la polisi liliingia kwa nguvu ndani ya nyumba hiyo bila kibali.

Soma zaidi...

Nini Kinachotofautisha Uteuzi wa bin Mubarak kutoka kwa bin Abdul Malik katika Serikali ya Aden?!

Mnamo tarehe 6/2/2024, uamuzi ulitolewa na Baraza la Rais mjini Aden kumteua Ahmed Awad bin Mubarak kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Aden, akimrithi Maeen Abdul Malik. Uteuzi wa Ahmed bin Mubarak umekuja baada ya Baraza la Rais kufeli katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kuafikiana juu ya idadi ya wagombea wa nafasi ya uwaziri.

Soma zaidi...

Kisimamo cha Familia za Mashababu Wanaozuiliwa wa Hizb ut Tahrir mbele ya Bunge la Wawakilishi

Familia za Mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Jordan, wanaozuiliwa na Mahakama ya Usalama ya Serikali, walifanya walilaani mbele ya Bunge la Wawakilishi, asubuhi ya leo, Jumatano 14/02/2024, ambapo waliitaka Afisi ya Mkuu wa Bunge la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhuru wa Umma na Haki za Kibinadamu kufanya kazi na kuwasiliana na wale wanaohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru mara moja kwa watoto wao waliowekwa kizuizini kwa sababu ya kutoa maoni yao ambapo hawakufanya kitendo chochote cha kigaidi, au uhalifu wowote kwa sheria za usalama wa serikali.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu