Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Dola za Kikoloni Zinatafuta Kuinasa Taliban Ndani ya Wavu wa Mfumo wa Kilimwengu wa Kimataifa
Na: Musab Umair – Wilayah Pakistan

(Imetafsiriwa)

Dola kuu sasa zinaamiliana kikamilifu na Taliban ya Afghanistan, ndani ya mfumo wa sasa wa kilimwengu. Kuongezeka kwa muamala kunaashiria hatari mpya kwa Umma wa Kiislamu, kuhusiana na ardhi yake ya mpaka inayoheshimika ya Ribaat, na makaburi ya himaya, Afghanistan.

Ama kuhusu Marekani, Sauti ya Amerika iliripoti mnamo tarehe 1 Februari 2024 (Chanzo 1) kwamba, "Marekani inachunguza kwa uangalifu uwezekano wa kuingia kibalozi kuifikia Afghanistan inayodhibitiwa na Taliban, kulingana na hati mpya ya mkakati iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje.” Hati hiyo ya mkakati iliyonukuliwa inaitwa, "Mkakati Jumuishi wa Nchi: Afghanistan," na inasema kwamba, "lazima tujenge mahusiano ya kiutendaji ambayo yanaendeleza malengo yetu." (Chanzo 2)

Ama kuhusu China, mdau mkubwa nchini Afghanistan ndani ya eneo lake, imeanzisha mahusiano rasmi na ya kidiplomasia. Ni dola kuu ya kwanza kufanya hivyo. Wizara ya Mambo ya Nje wa Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan iliripoti mnamo tarehe 8 Februari 2024, "Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Xi Jinping, alikubali barua ya utambulisho wa Mawlawi Asadullah (BilalKarimi) kama Balozi wa kipekee wa Imirati ya Kiislamu ya Afghanistan nchini China." (Chanzo 3)

Kuhusu wadau wengine wakuu wa eneo hilo, shirika la habari la Urusi TASS lilisema mnamo tarehe 28 Septemba 2023, "Urusi inaweza kuitambua serikali ya mpito ya Taliban (iliyoharamishwa nchini Urusi) katika mustakbali, lakini wawakilishi wake lazima wapate hili kupitia kutimiza majukumu yao, Mwakilishi Maalum wa Rais wa Urusi kwa Afghanistan Zamir Kabulov alisema katika mahojiano na RTVI. (Chanzo 4)

Wasiwasi mkubwa wa Urusi ni ule wa serikali ya inayojumuisha makabila tofauti tofauti ambayo haijafungika kwa kabila la Pushtun, lakini inajumuisha jamii zinazopatikana katika uliokuwa Usovieti, dola za Asia ya Kati, Watajiki na Wauzbeki.

Kwa kweli hakuna jipya katika mkakati kuelekea Afghanistan, ikilinganishwa na mkakati wa jumla kuelekea Mashariki ya Kati. Ni mkakati huu ambao umehakikisha kutawala kwa ukoloni juu ya Ulimwengu wa Kiislamu tangu kuvunjwa kwa Khilafah mnamo tarehe 3 Machi 1924, sawia na 28 Rajab 1342 H. Ama kuhusu Afghanistan yenyewe, dola kubwa za wakoloni zinaimezea mate ikiwa kama "Saudi Arabia ya lithium" miongoni mwa utajiri mwingine mwingi ilionao ndani ya ardhi yake ya majabali.

Utabikishaji wa mkakati huo unategemea mfumo wa adhabu na motisha ili kuhakikisha uzingatiaji. Vivutio vyake muhimu zaidi ni pamoja na kusukuma kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa cha usaidizi wa kibinadamu, kukuza biashara ya kiuchumi, kuongeza ufadhili na kuwashawishi Taliban kutabanni kanuni za kiuchumi za kimataifa. Kuhusu adhabu ndani ya eneo hilo, watawala vibaraka wa Pakistan walisababisha migogoro mikubwa ya wakimbizi ndani ya Afghanistan. Baada ya mikutano na maafisa wa Marekani, watawala wa Pakistan waliwafurusha ghafla mamia kwa maelfu ya Waislamu wa Afghanistan waliokuwa wakiishi ndani ya Pakistan kwa miongo kadhaa, huku wengi wa vijana wao wakiwa hawajui lolote kuhusu maisha nje ya Pakistan. Kwa kuongeza, kuna mapigano makali kati ya Jeshi la Pakistan na wapiganaji wa kikabila, ambayo ni adhabu zaidi, ya umwagaji damu. Ama kuhusu dola za Magharibi zinaibua kelele na kilio juu ya haki za wanawake na watoto ili kuleta shinikizo, ingawa haki hizo hazina thamani yoyote kwa dola za Magharibi, kama inavyodhihirika wazi katika kadhia ya Gaza.

Makundi fulani ndani ya Taliban yanaonyesha nia ya kukuza mahusiano chanya na nchi za Magharibi, msimamo unaotangaza hatari. Makundi kama hayo yanafanya kosa lile lile baya lililofanywa na viongozi wengine katika nchi za Kiislamu. Wanaungana na dola za wakoloni, hivyo wanaingia kwenye mtego wa wavu wao wa sheria na mikataba. Uongozi wa Taliban lazima uelewe kwamba ukoloni uliondoka Afghanistan kutoka mlango wa mbele, baada ya Jihad, na sasa unajaribu kuingia tena kupitia mlango wa nyuma, kwa kutumia taasisi za kimataifa.

Sera ya kigeni ya dola kubwa inazunguka pambizoni mwa ukoloni. Marekani ilimaliza ukoloni wake wa kijeshi nchini Afghanistan. Inajaribu kuwezesha tena njia zake kupitia mbinu za kiuchumi na kijasusi nchini Afghanistan, haswa njia za kijasusi ambazo ziliporomoka baada ya 2021.

Katikati ya ushindani mkubwa baina ya dola kubwa, Mujahid wa Taliban lazima watengeneze njia huru kwa Umma wa Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah. Kufungamana na dola kubwa ni njia iliyotabanniwa hapo awali na makundi ya Kiislamu, ambayo daima imekuwa ikishindwa, na kusababisha unyonyaji wa rasilimali za Waislamu kwa malengo ya wakoloni. Kwa hivyo, Taliban lazima ikatishe mawasiliano na maadui wa Waislamu na vibaraka wao katika Ulimwengu wa Kiislamu kabisa. Ni lazima ishiriki kikamilifu katika mradi mmoja ambao utachukua nafasi ya mfumo wa sasa wa kilimwengu. Mradi huo ni Khilafah kwa Njia ya Utume. Itaziunganisha dola za Kiislamu kuwa Khilafah moja yenye nguvu. Khilafah itazikomboa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na kufungua ardhi mpya kwa Uislamu kupitia Dawah na Jihad. Itageuza kujisalimisha kuwa utawala, na kushindwa kuwa ushindi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ما ترك قوم الجهاد إلاّ ذُلّوا» “Watu hawataiacha Jihad isipokuwa watadhalilika. [Ahmad].

 

Maregeleo

1.https://www.voanews.com/a/us-exploring-consular-return-to-afghanistan-without-recognizing-taliban-rule/7467103.html

2.https://www.state.gov/wp-content/uploads/2023/12/ICS_SCA_Afghanistan_31OCT2023_PUBLIC.pdf

3https://mfa.gov.af/en/16271

4 https://tass.com/politics/1681639

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu