Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uingereza ni Nchi ya Ajabu ambapo Watu Mabubu Huamini Mambo Yasiyo na Maana na Wenye akili Hutishiwa ili Kukubaliana nayo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kichwa cha habari cha gazeti la ‘The Guardian’ mnamo tarehe 16 Februari 2024, kilichoandikwa na Gaby Hinsliff, kilisema: "Jifunze hili kutokana na mzozo wa Rochdale: jamii inakabiliwa na hatari pindi watu werevu wanapoamini mambo yasiyo na maana."

Maoni:

Je, ni ukweli kiasi gani kwamba jamii inakabiliwa na hatari wakati watu werevu wanaamini mambo yasiyo na maana, lakini katika hali kama hizo angalau watu wenye akili wanaweza kuona ukweli na kubadili mawazo yao. Hatari kubwa zaidi ni pale watu mabubu wanapoamini mambo yasiyo na maana na watu werevu wanatishiwa ili wakubaliane nayo, na ndivyo inavyotokea nchini Uingereza ambapo ukosoaji wowote wa uharibifu na mauaji ya raia huko Gaza unakomeshwa kwa kuhojiwa vikali. Kwa siku kadhaa, vyombo vya habari vya Uingereza vimemfuatilia mgombea wa chama cha Muslim Labour, Bw. Azhar Ali, ambaye alisikika katika mazungumzo ya faragha yaliyovuja pamoja na wanachama wenzake wa Chama chake akisema: "Wamisri wanasema kwamba waliionya Israeli siku 10 kabla ... Wamarekani waliwaonya siku moja kabla [hayo] ... kuna kitu kinatendeka. Waliondoa ulinzi kwa makusudi, waliruhusu ... mauaji hayo ambayo yanawapa idhini ya kufanya chochote wanachotaka.”

Bwana Ali alitoa maoni hayo mara tu baada ya tarehe 7 Oktoba, wakati ulimwengu, na hasa ulimwengu wa Kiislamu, uliposhangazwa na ukubwa na kasi ya kuanguka kwa lile linaloitwa Jeshi la Ulinzi la "Israeli" (IDF) karibu na eneo la Gaza. Hadithi ya kutoshindika kwa "Israel" ilivunjwa mara moja na wengi walipata ugumu kuamini kwamba umbile la Kizayuni halikujua juu ya shambulizi linalokuja kutoka Gaza. Kama maelezo ya pembeni, IDF ilihitajika mara mbili tu katika historia yake kutetea umbile la Kizayuni, na mara mbili ilishindwa. Umbile la Kizayuni limekuwa likizitegemea tawala za nchi jirani za Kiarabu kwa ulinzi wake, ili liweze kuzingatia kuwatiisha Wapalestina, na dori yake ya hila ya kuwa kambi kubwa ya mafunzo kwa vijana wake. Katika hali ya mchanganyiko wa kijinsia ya urafiki, unaowatazama 'wengine' waliodhoofishwa, vijana wa Kiyahudi wanaoweza kuguswa wanachukua dhana ya kizushi ya kikoloni ya Uzayuni wa kisiasa wenye ubinafsi na kuwa na tukio la kushiriki katika uvamizi ghasia wa kikoloni kwa maisha ya Wapalestina, ili kwamba baada ya hapo, kukataliwa kwa Uzayuni wa kisiasa kungekuwa kujikataa wenyewe kwa uchungu. Wachache ambao hushindwa kuelewa mafundisho hayo huachwa na aibu na kuharibiwa kihisia kutokana na uzoefu, kulingana na ushuhuda kutoka kwa askari wa zamani wa IDF. Wengi wameukosoa utamaduni huu wa kikoloni bila ya kuwatakia madhara Mayahudi.

Jambo la kushangaza kuhusu vyombo vya habari vya Uingereza na taasisi zake za kisiasa ni jinsi zinavyochukua sio tu msimamo huo dhalimu na wa upande mmoja lakini bila huruma kuwasafisha wapinzani wote. Chama cha Labour, kwa mfano, kiliwafukuza mamia ya wanachama wake kwa chuki dhidi ya Mayahudi na hata kiongozi wake wa zamani, Jeremy Corbyn, aliathiriwa na ufukuzwaji huo, na maelfu zaidi walitumwa kwa kulazimishwa kuelimishwa upya katika miezi iliyofuata. Pamoja na haya yote ya ‘kuelimishwa upya’, sasa tuna wanachama wengi wanaoadhibiwa kwa kutoa ‘fikra potofu’. Cha kushangaza, Mayahudi walikuwa na uwezekano mara tano zaidi wa kushtakiwa kwa chuki dhidi ya Mayahudi kuliko wasiokuwa Mayahudi, kulingana na ripoti ya shirika la Kiyahudi la Voice of Labour (JVL) kwa Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu (EHRC) mnamo 2021, ambayo inapaswa kumfanya mtu yeyote mwenye akili kuhoji fundisho lililopo. Kwa vitendo vya mauaji ya halaiki vya IDF huko Gaza, ukosoaji wa umbile la Kiyahudi umeongezeka, na ufukuzaji kwa chuki ya mayahudi umeanza tena. Wanasiasa wameadhibiwa, madaktari na wataalamu wengine wanalengwa kufukuzwa makazini, watu waliovalia vitu vya kitamaduni vya Palestina au wanaotaka Palestina iwe huru wametishiwa. Yote haya kwa sababu, kwanza, chuki dhidi ya Mayahudi imefafanuliwa upya kwa upotovu kumaanisha ukosoaji wa umbile la Kiyahudi na pili, Uingereza imekuwa dola ya polisi ambapo washawishi na wamiliki wa vyombo vya habari mabilionea wanaamua nini watu wanapaswa kufikiria, na majeshi ya kasuku huandika makala kulalamika juu ya wale wanaokengeuka kutokana na mafundisho mapya.

Gaby Hinsliff anatoa nukta ya kufurahisha katika kipande chake cha maoni katika gazeti la ‘The Guardian’ kwamba "alama ya fikra za njama ni imani ya kidini kwamba hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, kwa kubuni tu, na kwamba ni watu tu wasio na akili kujua jinsi ulimwengu ulivyo wanaweza kufikiria vyenginevyo. Wanapopingwa, waumini hurudi kwa hasira kwenye jambo hilo moja la asili, kabla ya kusisitiza kwamba wana haki ya kutoa maamuzi yoyote wanayopenda kutoka kwayo.” Anawatetea watu "wanaopambana na uchafu hatari wanapousikia na hivyo kuweka desturi ya kawaida ya kijamii", lakini hakuna mtu anayeweza kupinga chochote tena nchini Uingereza kwa sababu 'desturi za kijamii' zimewekwa nguvu na ingawa kwa huzuni Bw. Ali alitishiwa kukana maoni yake, aliadhibiwa hata hivyo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu