Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 1 Rajab 1442 | Na: 1442/023 |
M. Jumamosi, 13 Februari 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miaka 100 ya Kiza, Utovu wa Heshima na Kukata Tamaa kwa Mwanamke wa Kiislamu kwa Kukosekana kwa Ngao na Mlinzi wake – Khilafah
(Imetafsiriwa)
Rajab hii inaashiria hatua nyingine mbaya katika historia ya Umma wa Kiislamu - miaka 100 katika kalenda ya Hijria tangu kuvunjwa kwa dola yake tukufu na uongozi wa Kiislamu: Khilafah mikononi mwa adui wa Uislamu, Mustafa Kemal, na serikali za kikoloni za Kimagharibi. Tukio hili baya lilikuwa na athari mbaya kwa maisha ya wanawake wa Kiislamu na watoto wao na familia zao, kwani walipoteza dola ambayo kila wakati ilisimama kama mlezi na mlinzi juu ya haki zao, ustawi na hali nzuri maishani, kwani Mtume (saw) amesema,
« الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ »
"Imam (Khalifah) ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake". Katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, kwa kukosekana kwa Khilafah, maisha ya wanawake wa Kiislamu yamekumbwa na kifo, uharibifu, utovu wa heshima, umasikini na kukata tamaa. Wao na watoto wao wamekuwa wahanga wakuu wa vita vya kikoloni visivyo na huruma, utawala dhalimu wa kidikteta wa kisekula unaosaidiwa na Magharibi katika nchi za Waislamu, na pia uvamizi wa kikatili na mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu. Kutoka kwa dola iliyotawaliwa na Uislamu ambayo chini yake mwanamke wa Kiislamu alikuwa kitovu cha umakini katika upande wa utunzwaji na ulinzi, na ambapo viongozi wake walihamasisha majeshi yote kuhami heshima yake… leo tuna ulimwengu uliopoteza Khilafah ambapo wanawake wa Kiislamu wananyanyaswa, kufa na njaa, kufungwa gerezani, kuteswa, kubakwa na kuchinjwa na maadui wa Uislamu bila ya kujali sheria, na ambapo hakuna jeshi lolote linalohamasishwa kuwasaidia. Wala dola yoyote kuwapa hifadhi ya heshima.
Kwa kuongezea, kwa kukosekana kwa utawala wa Kiislamu, ardhi za Waislamu zimekumbwa na ghasia kubwa dhidi ya wanawake na ukiukaji dhidi ya heshima yao. Hii ni pamoja na kusibiwa na ongezeko la maovu, upendaji mali na ufisadi kwa sababu ya kuenea kwa maadili huria ya Kimagharibi ambayo yametia sumu ladha ya vijana na kuwapotosha kutoka kwa Dini yao na kuingilia mitindo ya haribifu ya kimaisha. Kuingizwa kwa maadili haya ya kiliberali, pamoja na kutengwa kwa sheria za Kiislamu za kijamii na familia maishani ambazo zilifuata kutoweka kwa Khilafah, pia kulisababisha janga la kuvunjika kwa familia, na kusababisha mlima wa shida kwa wanawake, wanaume na watoto vilevile. Kwa kuongezea, kwa kukosekana kwa mfumo wa Kiislamu, wanawake walinyimwa haki zao walizopewa na Mwenyezi Mungu za kupata elimu ya hali ya juu na huduma ya matibabu kwa sababu ya kuporomoka kwa mifumo ya elimu na afya chini ya serikali tepetevu na fisadi mtawalia ambazo hazijali chochote kuhusu mahitaji yao watu. Zaidi ya hayo, kwa kutoweka Khilafah, wanawake walinyimwa dola ambayo ilihakikisha matunzo yao ya kifedha na usalama. Kwa hivyo, waliachwa wajitafutie wenyewe, mara nyingi wakifanya kazi ya unyanyasaji, au kuombaomba barabarani au kuchakura rundo la takataka ili kuishi. Yote haya ni mbali na marupurupu mengi ambayo wanawake walifurahiya ndani ya dola ambayo ilifurika utajiri, na ambayo ilitokomeza umasikini kutoka katika ardhi, ikawaletea ufanisi watu wengi na ikajenga taasisi za elimu ya daraja la kwanza na vituo vya huduma za afya ambavyo viliwanufaisha wanaume na wanawake sawia. Hakika, kwa kukosekana kwa ngao yao na mlinzi wao, Khilafah, mateso, machungu na hasara ambazo wanawake wamepata ni kubwa na zisizo na kikomo.
Hivyo basi, kampeni hii ni sehemu ya kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Hizb ut Tahrir kwa mwongozo wa Amiri wa Hizb, mwanachuoni mkubwa, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, yenye kichwa, "Juu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah … Enyi Waislamu, Isimamisheni!" Kitengo cha Wanawake katika Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni yake ya kimataifa Rajab hii kuangazia athari chungu, mbaya ya kupoteza Khilafah juu ya maisha ya wanawake wa Kiislamu ulimwenguni, na pia kutoa maono ya kile haki za kweli, majukumu na hadhi ya wanawake itakuwa chini ya utawala wa Kiislamu na kutoa wito wa kusimamishwa kwa dharura kwa dola hii ya Kiislamu, Khilafah Rashidah. Pia itasambaratisha fahamu nyingi potofu na uwongo kuhusu ukandamizaji wa wanawake chini ya utawala wa Khilafah. Katika kampeni hii, sisi wanawake wa Hizb ut Tahrir, tunasema miaka 100 ya mateso yasiyo vumilika, udhalilifu na hasara imetosha! Tunahitaji kuileta sura hii yenye kiza zaidi katika historia ya Umma wa Kiislamu mwisho wa haraka! Enyi Waislamu! Tunakuita muunge mkono kampeni hii muhimu, na muwe miongoni mwa wale wanaopata heshima kubwa Bi'idhnillah ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili!
Fuatilia kampeni hii katika:
http://www.domainnomeaning.com/en/index.php/hizbuttahrir/20797.html
na Ukurasa wa Facebook:
https://www.facebook.com/womenscmoht/
#أقيموا_الخلافة
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
#خلافت_کو_قائم_کرو
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@domainnomeaning.com |