Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  14 Jumada II 1442 Na: 1442 H / 021
M.  Jumatano, 27 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Komesheni Upatilizaji Wenu wa Vidonda vya Ummah wa Uislamu
(Imetafsiriwa)

Ulinzi wa Raia wa Syria ulisema kwamba idadi ya kambi za wasio na makao ambazo zimeharibiwa na mvua na theluji katika Gatuzi la Idlib (kaskazini magharibi mwa Syria) zimeongezeka hadi kambi 225, ikiashiria kwamba idadi ya familia ambazo sasa hazina makao imefikia familia 3,200. Ulinzi wa Raia ulielezea kuwa idadi hii inatarajiwa kuongezeka kutokana na maumbile ya eneo hilo na ukosefu wa njia za kuzuia mafuriko, kama vilima na mitaro ya maji.

Watoto wawili walifariki katika kambi kaskazini mwa Idlib Jumatano iliyopita, kutokana na baridi kali, hali mbaya ya hewa na theluji iliyoenea kaskazini mwa Syria. Mtoto mwingine alikufa siku moja kabla, na watoto watatu walijeruhiwa kutokana na kuporomoka kwa hema lao la matofali, kufuatia mvua kubwa.

Mateso ya maelfu ya wakimbizi katika kambi za Gatuzi la Idlib huzidi kila msimu wa baridi, kwani kambi zisizo rasmi huenea kwa kushirikiana na kampeni ya kijeshi iliyozinduliwa na serikali katili ya Siria. Mateso haya, ambayo yamekuwa yakirudiwa kwa miaka 9 katika kambi ambazo hazina miundombinu, na zilizo katika ardhi ya kilimo ambapo wakimbizi wameweka mahema yao na hawana msaada wowote baada ya kukosa mahali pengine pa kwenda, baada ya umiminaji mabomu ya kinyama ulio walilazimisha mamilioni ya raia kukimbilia maeneo karibu na mpaka wa Uturuki na Syria huko Idlib, ambapo wanahisi kukwama, hawawezi kuingia Uturuki, hawawezi kurudi majumbani mwao, na hawawezi kupata misaada ya kutosha huku hali ikizidi kuwa mbaya, kwani mamia ya maelfu ya familia wamelazimika kuishi katika mahema baada ya kushindwa kulinda nyumba zao.

Waliohamishwa katika kambi hizi wanaishi katika hali duni ya maisha kwa hofu ya siku zijazo, kwa kuzingatia udhaifu mkubwa wa majibu ya mashirika ya kimataifa na jumuia za misaada, kwani wanakosa chakula, dawa, joto na mahitaji yote ya maisha, haswa kwa ujio wa wimbi la baridi, wakati joto linapofika chini ya sifuri usiku, ambapo haya yalijiri kabla ya siku za Mvua, wakati maji ya mvua yalipovamia mahema ya wakimbizi walipokuwa wamelala, mali zao za kawaida za nguo na blanketi zikafurika, na kambi zao zikawa mabwawa ya maji na matope kama inavyo kuwa kila msimu wa baridi.

Mwanzoni mwa janga la ukosefu wao wa makao, taasisi za misaada na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yalishindana katika kufanya mikutano mfululizo kukusanya michango na misaada kutoka nchi za kirafiki ili kupata suluhisho la haraka kumaliza janga hili na kupunguza mateso ya wakimbizi wanaokimbia ukatili wa serikali dhalimu ya Syria na washirika wake.

Na hii hapa miaka mingi, yenye uchungu ambayo inapita bila masuluhisho msingi, na bila hata masuluhisho bandia, ambayo hutuanika tena na tena:

- Kwamba mashirika haya sio ya kibinadamu, bali ni mashirika ya upatilizaji wa hali hii ya kibinadamu, kwani sasa imebadilika kuwa faili ya faida ya kila mwaka, ambayo haizidi katika ukusanyaji wake wa michango na ruzuku isipokuwa kiuhalisia ni makombo ili kutia majivu machoni.

Ama ambazo zimewafelisha wanawake walio na huzuni na watoto wanaodhulumiwa ambao hukosa hitaji hata dogo kabisa la joto; watoto ambao umri wao ni umri wa janga. Kwa hivyo ni mustakbali gani unaowasubiri katika kambi zilizo na hali hizi duni ambazo havifai hata kwa maisha ya wanyama, Mwenyezi Mungu awalinde kutokana na haya, na kwa kipindi cha miaka yote hii migumu ambapo msiba wa kihakika uko hata bila dhoruba za theluji?!

- Hakika kupuuzwa kabisa kwa hali ya watu wa makambi na wengineo ni sehemu ya msururu wa udanganyifu na shinikizo ili kukubali masuluhisho yoyote yaliyoundwa na Amerika chini ya madai "hakuna wokovu kwenu isipokuwa kwa kurudi katika gereza la wanyongaji." Serikali ya kihalifu ya Kibaathi na washirika wake sio sababu pekee ya mateso ya watu wetu kwenye kambi, kwani washirika wao katika hili pia ni wale wote ambao wameshindwa au wamepuuzia utafutaji suluhisho la kimsingi la kumaliza mateso ya watu wote wa Ash-Sham, sio tu mateso ya wakaazi wa kambi.

Basi jueni enyi Waislamu:

- Kwamba kuwanusuru Waislamu madhaifu nchini Syria na kupunguza mateso yao sio neema au hisani, bali ni jukumu linalohitajika na udugu wa itikadi ya Kiislamu, na ayah na hadith tukufu zinalingania hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]. Na Mtume (saw) amesema:

«مَا مِنِ امْرِئٍ يَخْذُلُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ، وَيُنْتَقَصُ فِيهِ عِرْضُهُ إِلا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنِ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْطِنٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَتُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ إِلا نَصَرَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ».

“Hakuna Muislamu ambaye atamtelekeza Muislamu mwengine katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa, na heshika yake inachafuliwa isipokuwa Mwenyezi Mungu naye atamtelekeza katika sehemu ambayo angependa kupata nusra yake; na hakuna Muislamu ambaye atamnusuru Muislamu mwengine katika sehemu ambayo heshima yake inachafuliwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu naye atamnusuru katika sehemu ambayo angependa kupata nusra yake.”

- Hakika wakati umewadia wa kufanya kazi ya kuhamasisha waokozi wa Ummah karibu na mradi wa wokovu ambao ndio msingi wa itikadi yetu, mradi wa Khilafah pekee, ambao unahakikishia juhudi unganishi za kuing'oa serikali katika nyumba yake wenyewe, ili mateso ya watu wetu yaishe nayo, na kwa mradi kama huo na wafanye kazi wenye kufanya kazi.

Ee Mwenyezi Mungu, tuchukue kwa mikono yetu, na utufariji dhiki zetu, na kuharakisha kusimama kwa Dola ya Kiislamu. Ee Mwenyezi Mungu, wapunguzie baridi ya msimu wa baridi wale wasio na makaazi, na uwahurumie maskini kutokana na ukali wa baridi wanayotateseka kwayo.

]وَلَا تَحْسَبَنَّ اللَّهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim: 42]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.domainnomeaning.com
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) domainnomeaning.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu