Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  19 Safar 1444 Na: 1444 / 07
M.  Alhamisi, 15 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

“Blackberry Wakati wa Uvamizi Haina Maana!”

Utayari wa Dola ya Khilafah katika Kukabiliana na Maafa na Ajali  
(Imetafsiriwa)

Kuporomoka kwa jengo la makaazi katika eneo la Al-Weibdeh katikati mwa mji mkuu, Amman, siku ya Jumanne, kumesababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine 10, katika hali isiyokwisha, huku msako wa kuwatafuta manusura ukiendelea kwenye vifusi. Kuna habari ambazo hazijathibitishwa juu ya uwepo wa zaidi ya watu 10 chini ya vifusi, ambao kati yao wako hai, na Manispaa ya Amman imeondoa watu kwenye majengo 4 karibu na jengo lililoporomoka.

Awali ya yote, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwarehemu wale waliofariki katika ajali hii mbaya, na uponyaji kwa majeruhi, na awatie moyo wa subira familia zao zote na kuwafariji misiba yao. Muislamu hana ila kujisalimisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na subira kwa yale Mwenyezi Mungu (swt) anayompa, huenda Mwenyezi Mungu akambadilishia hapa duniani na akhera kwa kilicho bora zaidi kuliko alichokikosa au kukipoteza.

Hata hivyo, kuna kipengee chengine cha suala hili ambacho hakihusiani na qadhaa na qadar. Badala yake, ni kiini cha uchungaji wa mtawala kwa zizi lake. Ajali na maafa yamekuwa yakirudiwa kwa marefu na mapana ya nchi na tofauti tofauti, kwa miongo kadhaa; ya ajali na maafa ambayo hufuata mvua kubwa na theluji na kuporomoka kwa miundombinu, hadi tukio la kuvuja kwa gesi, ukosefu wa oksijeni, ajali za barabarani, ajali za kuporomoka kwa majengo na kuta, yawe ni ya zamani au machakavu, kama inavyosemwa; au hata mapya ambayo yanajengwa, ambayo mengi yalisababisha kupoteza maisha na hasara za majeraha ya kimwili na ya kimali.

Licha ya ajali na maafa haya na kujirudia rudia kwake, wananchi hawaoni chochote kutoka kwa serikali, vyombo vyake, na utayari wake wanaousifu, bali ni mkanganyiko na hofu ya papo hapo katika kukabiliana na athari za maafa hayo. Watu wa Jordan hulipa ushuru wa juu zaidi ulimwenguni, na serikali inadaiwa mabilioni hadi deni kuzidi dolari bilioni 51. Hawaoni hata chembe ya uchungaji maslahi yao, kwani miundombinu imechakaa chini ya shinikizo la serikali zinakwenda kwa kasi. Na hakuna maji wala kawi ila kwa bei ya juu, ikiwa ipo yoyote, na maslahi ya elimu na elimu ya juu yapo katika kiwango kibaya zaidi, na huduma ya afya hupatikana tu kwa baadhi ya watu wenye matatizo makubwa, na pindi ajali zinapotokea, hatuoni mikakati, taratibu, au mipango ya ushirikiano baina ya sekta husika ili kupunguza athari za ajali hizi, ingawa kwenye vyombo vya habari tuko mstari wa mbele katika nchi ambazo ziko katika hali ya hofu kutoa msaada wa kiufundi, nyenzo na matibabu kwa maafa yanayotokea katika nchi zingine za kiulimwengu.

Msingi wa tatizo katika uchungaji halisi na sahihi wa watu, na dhiki wanayoishi ndani yake, iwe ni wakati wa ufanisi au wakati wa shida, majanga na ajali, ni kuuweka mbali Uislamu na medani ya vita vya kimaisha, na kuubadilisha mfumo wa Uislamu kwa kirasilimali kwani mfumo wa kirasilimali wa kidemokrasia hauangalii mambo isipokuwa kwa mtazamo wa kimada.

Ni wa kinyama, hivyo unazingatia tu uwezekano wa kimada katika kukabiliana na majanga, na haujali kuhusu uchungaji na maslahi ya mwanadamu na kuhifadhi nafsi ya mwanadamu isipokuwa kwa kadiri ya maslahi ya kimada anayoyapata.

Lakini Dola ya Kiislamu, yaani Dola ya Khilafah (Ukhalifa), ina jukumu la kulinda maisha ya raia wake wakati wote. Anasema Mtume (saw): «كُلُّكُمْ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Hakika! Kila mmoja wenu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu anaowachunga: Imam (mtawala) wa watu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake.” (Imepokewa na Al-Bukhari).

Kwa mtazamo wa uchungaji mambo ambayo Khalifa anapaswa kuwa nao kwa raia wake, na ili kuzuia au kuondoa madhara yatokanayo na maafa kama haya, Dola ya Kiislamu inawajibika kwa maandalizi ya kuzuia maafa haya, kwa ajili ya kutayarisha mapema kukabiliana nayo wakati yanapotokea, na kwa ajili ya kujenga upya na kuyasaidia maeneo ya maafa.        

Ajali na majanga yanahitaji maandalizi kamili kwa sababu nyakati za kutokea kwayo hazijulikani. Mwitikio wa haraka wakati na baada ya majanga kama vile kuporomoka kwa majengo kwa wakaazi wake ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya watu. Dola ya Kiislamu huteua kamati ya wataalamu katika kila jimbo linalohusika na kitengo kikuu cha usimamizi wa maafa na ajali ambao kazi yao ni kujiandaa mapema ili kupunguza hatari ya ajali, maafa na matokeo yake, na kuandaa mipango ya kukabiliana nayo kwa mujibu wa umbile la eneo, na kisha kushughulikia tukio hilo kwa mbinu bora za kisayansi na kiufundi na njia zinazopatikana ulimwenguni, na kisha kamati hiyo hutatua matokeo ya maafa, na wakati huo huo, hutoa huduma kwa suala la chakula, mavazi na makaazi kwa kila mtu ambaye alilazimika kuhama na kwa muda unaohitajika.

Hata hivyo, ukweli kwamba Dola ya Kiislamu ndiyo yenye jukumu kubwa la kutibu athari za maafa kama hayo haimaanishi kwamba Waislamu, kama watu binafsi, wameepushwa katika kusaidia na kuchangia katika juhudi za kukabiliana na maafa, kwa sababu dalili ya kuondoa madhara na dalili ya kwamba ni wajibu kutoa msaada kwa wenye dhiki na wenye shida ni dalili za kijumla, ikiwemo serikali na watu binafsi, kama Mtume (saw) alivyosema na kuunganisha vidole vyake: «الْمُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِ كَالْبُنْيَانِ يَشُدُّ بَعْضُهُ بَعْضاً» “Uhusiano wa muumini kwa muumini mwengine ni kama (matofali ya jingo), kila moja hutilia nguvu jengine.”

Mtazamo unaowavutia watu katika nchi yetu kuhusu jinsi baadhi ya nchi nyingine zinavyokabiliana na ajali na majanga mbalimbali kwa utoshelevu, utayari, na njia na mbinu za hali ya juu, si ndoto ya mbali. Bali, ililazimishwa na kuishi kwao ndani ya dola duni ambazo mkoloni kafiri alizigawanya na kuwawekea mifumo inayoyafanya maisha ya watu wao kuwa magumu, duni na ya dhiki, licha ya akili na mali ambayo Mwenyezi Mungu amewajaalia. Lakini itafikiwa mara moja na kwa ubora zaidi kuliko hivyo mara tu Khilafah Rashida itakaposimamishwa, kwa kasi ya kufaulu, utoshelevu na uzoefu katika kushughulika, na kuwajali waliosibiwa na walioathirika na ajali hizi, ambao viungo vyao viko makini kufikia muundo bora wa kuishi duniani uliowekwa na Uislamu na kuamrishwa na Mola Mtukufu, hivyo kufanya kazi kuelekea kusimamishwa kwake, tunakulinganieni enyi Waislamu.

[إنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً]

Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.[ At-Talaq:3]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu