Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  15 Safar 1444 Na: 1444 / 06
M.  Jumapili, 11 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rasimu ya Sheria ya Haki za Mtoto katika Baraza la Wawakilishi la Jordan ni Aina ya Vita Dhidi ya Uislamu na Lazima Ikataliwe
(Imetafsiriwa)

Haibishaniwi kwamba Sheria ya Haki za Mtoto iliyoagizwa kutoka UNICEF, moja ya mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa, ni sheria ambayo haina uhusiano wowote na haki za watoto katika Uislamu, na ni aina ya vita dhidi ya Uislamu kama mifano yake iliyotangulia ya sheria za haki za binadamu na CEDAW inayo husiana na wanawake, ambapo Magharibi inajaribu kuanzisha maadili ya urasilimali uliooza, ambayo ni kinyume na maumbile ya kibinadamu, na uhuru fisadi na madhihirisho yake ya kiharibifu yanayoonekana katika jamii za Magharibi ya: kuvunjika kwa familia, kuoza kwa maadili, ushoga, kujiua, na kupoteza nasaba, kiasi kwamba asilimia 50 ya watoto katika jamii za Magharibi ni watoto nje ya ndoa!

Mgogoro uliopo ndani na nje ya Baraza la Wawakilishi ni ule wa wahusika kutaka kupitisha sheria hii kwa gharama yoyote kwa sababu ni “maelekezo ya mamlaka za juu,” katika maregeleo ya Spika wa Bunge kwa Baraza la Wawakilishi. Wanaofanya kazi chini ya majina ya wazi na ya aibu ni Kamati ya Kisheria ya Baraza la Wawakilishi, Wanawake na Masuala ya Familia, Waziri wa Sheria na baadhi ya majaji wa Shariah walishiriki ndani yake. Wanajificha nyuma ya msemo "kwamba majadiliano na lengo lake yanaendeshwa na dira ya maslahi ya juu ya kitaifa na maslahi ya jamii," kwa mujibu wa mkuu wa Kamati ya Sheria, akisisitiza juu ya kile kinachoitwa uboreshaji wa sheria na kuondolewa kwa vifungu vinavyokinzana na Shariah ya Kiislamu, iwe vinahusiana na kubadilisha Dini au umri wa kisheria wa ndoa, na kukinzana na Sheria ya Hali ya Kibinafsi, au uhuru wa mtoto kutoa maoni yake, na kuwakataza wasichana walio chini ya umri wa miaka kumi na minane kuolewa. Wote huo ni uhalali wa kiulaghai katika jaribio baya na la kupotosha la kupitisha sheria hiyo kwa gharama yoyote ile, kwa kurekebisha baadhi ya vifungu vyake na kuvipamba vyengine, kwani imekataliwa kabisa kwa sababu imeagizwa kutoka kwa imani na maadili fisadi ya kikafiri ya kirasilimali.

Haki za mtoto zinalindwa na Uislamu kupitia ukamilifu wa hukmu zake, uadilifu wake na kuafikiana kwake na umbile la mwanadamu ambayo yanatoa utulivu na ukinaifu wa kiakili, ambayo hujenga shakhsia bora za Kiislamu katika nyanja zote za maisha kupitia nidhamu ya familia. Familia ina dori muhimu ambayo haiwezi kupuuzwa au kudharauliwa. Mtume (saw) amesema: «كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» Nyote ni wachungaji nan yote mutaulizwa kuhusu mulivyovichunga.” Na yeye (saw) amesema: «كَفَى بِالْمَرْءِ إِثْماً أَنْ يُضَيِّعَ مَنْ يَعُولُ» Inatosha kuwa ni uovu kwa mtu, kuwapuuza wale ambao ni jukumu lake kuwaangalia.” [Imepokewa na an-Nasa'i].

Uislamu ulizingatia kuwalinda watoto na kuwaona kuwa ni pambo la maisha ya dunia. Ulimhakikishia mtoto haki nyingi na mbalimbali, kuanzia na nasaba iliyoanzishwa na kunakiliwa; yaani kupitia kuifanya ndoa kuwa ndio njia pekee halali ya kupata watoto. Ulichunga usimamizi wake na unyonyeshwaji wake wa kiasili, hivyo ulihakikisha kwamba ataishi chini ya uangalizi wa wazazi wake ili kumtunza kiafya, kisaikolojia na kielimu, na anadhaminiwa haki ya matibabu na huduma za afya anapokuwa mgonjwa, na kutompuuza mpaka apone. Uislamu umelinganisha baina ya watoto wote, unakataa kutofautisha baina ya mwanamume na mwanamke, na ukafaradhisha elimu ya mtoto na thaqafa, na hii ni haki kuu ya watoto katika Uislamu na wajibu wa wazazi kujishughulisha na kuwasomesha watoto wao na kuwafunza katika yote ambayo yatawafaa katika mambo ya Dini na dunia hii na kuinua vizazi kuwa viongozi na watawala wa baadaye. Kumlea mtoto katika itikadi ya Kiislamu ni haki ambayo ni sifa ya Shariah ya Kiislamu.

Kwa hivyo kwa nini kulazimisha sheria dhalimu ya watoto ya kimataifa? Kwa nini kuna utetezi mkubwa wa kuingizwa kwake kwenye katiba iliyotungwa na mwanadamu na kupitishwa na manaibu wake?! Wakati Uislamu, pamoja na hukmu zake za kiwahyi, umedhamini matunzo bora kwa mtoto katika Uislamu.

[أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]

Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Al-Mulk: 14]?! Jibu liko wazi na liko pande mbili, ya kwanza ni; hukmu za Uislamu hazitekelezwi katika nchi yoyote duniani ili tuweze kufurahia uadilifu na rehma, sio kwa watoto tu bali kwa Ummah mzima, tangu kuondolewa Uislamu katika medani ya vita vya kimaisha kupitia kuibomoa dola ya Khilafah zaidi ya karne moja iliyopita. Ama sababu ya pili, ni tawala za vibaraka zinazofanya kazi ili kufikia maslahi ya mkoloni kafiri Magharibi katika vita vyake dhidi ya Uislamu, na kuhujumu sheria zilizobaki za Uislamu zinazohusiana na hadhi ya kibinafsi, wanawake na watoto katika jaribio la kushambulia familia na malezi ya Kiislamu, ambayo ndiyo yanayotumiwa kwa ajili yake manaibu, mawaziri, waandishi wa kisekula na wanazuoni wa masultani (watawala); ili kulazimisha sheria zake za kishetani na kuupamba ubaya wake machoni pa watu.

Ni matamanio yao, kwa sababu itikadi ya Kiislamu bado imekita ndani ya nafsi za Umma, na kwa ujumla wake, unakataa sheria hizi za kikafiri za kimataifa. Unafahamu njama za wasaidizi hawa wafisadi wa madhalimu, kwa utamu wa maneno ya uhalali wao wa wazi. Utawaandika katika kumbukumbu yake wale wanaokubali kuzipitisha sheria hizi na kumsaliti Mwenyezi Mungu (swt) na Dini yake kwa ajili ya starehe zisizo na maana za kidunia. Kwa hivyo, kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu (swt) na simameni pamoja na Ummah wenu mnaodai kuuwakilisha, kwani wote unakataa kata kata sheria hii fisadi ya mtoto.

Ama suluhisho msingi litakaloona mwanga hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, ni kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, mradi wa mwamko wa Umma ambao utakomesha sheria zote za kikafiri ambazo zilipitishwa kinyume na matakwa yake, na kwa nchi za makafiri  za kirasilimali ambazo zinafanya kazi ya kulazimisha maadili yao yaliyooza na fisadi badala ya hukmu za Uislamu, ambao wanahisi ukaribu wa kuanzishwa kwao na kwa hiyo huchochea vita vyake dhidi ya Uislamu. Hivyo basi, tunawalinganieni kwa ajili ya kazi ya kusimamisha Khilafah, Enyi Waislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالاً بَعِيداً]

Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali [An-Nisa: 60].

 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu