Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  25 Safar 1444 Na: 1444 / 08
M.  Jumatano, 21 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mkataba wa Maelewano na Usaidizi wa Kifedha kwa Jordan

Udhibiti Hatari wa Kikoloni wa Marekani  
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa tarehe 16/9/2022, Naibu Waziri Mkuu wa Jordan na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni Ayman Safadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken walitia saini, jijini Washington, mkataba mpya wa maelewano kuhusu uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuhusu misaada ya kifedha ambayo Amerika inakusudia kutoa kwa Jordan kwa miaka saba ijayo, ukihakikisha kujitolea kwa Amerika kwa usalama na utulivu wa Ufalme huu. Kwa mujibu wa taarifa moja iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan, mawaziri hao wawili walitia saini mkataba huo, ambao ni wa nne kati ya nchi hizo mbili, ambapo Marekani itatoa msaada wenye thamani ya dolari bilioni 1.45 kila mwaka, kwa miaka saba, kuanzia fedha mwaka 2023 na kumalizika 2029, ambacho ni kipindi kikubwa na kirefu zaidi cha misaada iliyotolewa na Amerika kwa Jordan.

Baada ya kuibuka nchi tajiri na yenye nguvu mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, Amerika, pamoja na nguvu yake ya kijanja ya kikoloni, imeifanya misaada ya kigeni kuwa kipaumbele cha kwanza, na hili limejumuishwa katika bajeti ya Amerika kwa jina la kudumisha usalama wa kitaifa. Tangu ilipoingia Mashariki ya Kati kama dola mpya ya kikoloni, misaada na usaidizi wa kifedha, ambao hauzidi 1% ya bajeti yake, ni mojawapo ya mbinu za kisasa za kikoloni ambazo Amerika inafuata katika kukoloni mataifa na kupanua udhibiti na ushawishi, na ni muhimu na yenye madhara kama ukoloni wa moja kwa moja wa kijeshi. Mbinu hizi zinazofanywa na nchi za kikoloni ni njia za kupata utiifu wa kisiasa na kujenga utegemezi katika nyanja zote zikiwemo kisiasa, kijeshi, kiuchumi na kiusalama.

Mkataba wa maelewano uliotiwa saini na utawala wa Jordan na Amerika sio maelewano juu ya usaidizi wa kifedha ambao Amerika itatoa kwa Jordan, lakini ni mkataba wa maelewano wa pande mbili juu ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Amerika na Jordan. Mikataba hii itawasilishwa kwa Bunge la Jordan, na hailazimiki kisheria au kimataifa kama makubaliano ya nia, na la muhimu zaidi ni kwamba una vifungu vingi vya siri, ambavyo havijafichuliwa na pande hizo mbili lakini kwa kawaida huipendele nchi mfadhili yenye nguvu, huku nchi dhaifu na yenye haja ikitii maagizo yake yote ambayo hayajatangazwa, na kwa hakika ni tofauti na kile ambacho Safadi ametangaza katika mahojiano ya faragha na Ufalme, kwamba "msaada huo hauna masharti na unaweza kuongezeka."

Taarifa ya pande zote mbili, kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa maelewano wa pande mbili za ushirikiano wa kimkakati kati ya Marekani na Jordan, ambayo ilitangazwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilisema kuwa “dhamira ya Marekani kwa usalama na ustawi wa Jordan ni thabiti, na mkataba huu wa maelewano utashughulikia changamoto zisizo za kawaida zinazoikabili Jordan, kwani inapunguza athari kubwa ya changamoto za kikanda, na kuunga mkono mpango wa mageuzi wa kiuchumi wa Mfalme Abdullah II, na kuthibitisha uimarishaji wa muda mrefu wa ushirikiano kati ya Marekani na Jordan.”

Ama kuhusu masharti ya misaada hiyo, ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan alikanusha kuwepo kwake, maelezo ya mkataba wa maelewano kama tulivyotaja ni ya siri, inaonekana ni wenye kutusi, lakini watu wa Jordan wamezoea kutoamini kauli za serikali, linapokuja suala la uhusiano na makubaliano, kati ya serikali, Amerika na umbile la Kiyahudi, na ambayo vyombo rasmi vya habari vya ndani haviyataji. Ulisia ambao Wajordan wanauona na kuishi katika upotovu wa mikataba hii, ambayo Amerika inailipa Jordan misaada hii na kuonyesha uungaji mkono, badala ya kile inachopata na kufikia kutokana na kuimarisha usalama wake wa kitaifa ili kufikia maslahi yake nchini Jordan.

Aaron David Miller, mwanachama wa Taasisi ya Carnegie, alisema kuhusu Mkataba huu wa Maelewano: “Ongezeko la usaidizi wa pande mbili, katika muktadha wa mkataba wa maelewano, litakuwa ni uwekezaji mdogo, huku Marekani ikihamisha vipaumbele vyake kwenda Asia.” (Axios)

Amerika imepata manufaa makubwa, kutokana na makubaliano ya pamoja ya ulinzi na Jordan mwaka jana, na iliimarisha uwepo wake wa kijeshi katika kambi na maeneo zaidi ya 14, na kuifanya Jordan kuwa kituo kikuu cha kuweka majeshi yake katika Mashariki ya Kati. Vikosi hivi haviko chini ya sheria za nchi au ufuatiliaji na vina uhuru wa kutembea. Bila shaka, dori za kijeshi zinazohitajika na vikosi vya Jordan ni ufahamu muhimu zaidi ambao haujatangazwa, na Amerika, kupitia mashirika yake ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, inalazimisha maadili na sheria fisadi za kimataifa kupitia masharti ya kutoa msaada kwa jamii, kielimu, taasisi za afya na kiuchumi, na sheria za kuwawezesha wanawake, na Sheria ya Mtoto ambayo imepitishwa kijanja, na kwa uhadaifu bila hatua yoyote kutoka kwa Wawakilishi wa Baraza la Jordan ni mfano mmoja tu.

Kwa sababu ya msaada huu, na ule unaoitwa ushirikiano na uhusiano wa kimkakati, kama mkataba wa maelewano unavyoita, balozi wa Marekani anatembelea taasisi za mitaa na manispaa na kutoa maagizo yake yenye sumu bila uwajibikaji au usimamizi wowote, na msaada huu unatiririka ndani ya mfumo wa makubaliano ya Wadi Araba ndani ya mkakati wa Amerika wa kuunga mkono umbile la Kiyahudi na nchi zilizofanya amani nalo, na makubaliano ya pamoja ya kiuchumi na kikanda na wote wawili, kama vile Mkataba wa Nia ya Kawi, Gesi na Maji.

Kuhusu uhalali unaotolewa na pande za Jordan na Marekani kufinika misheni za mikataba mingi ya maelewano, zimefichuliwa kwa rai jumla yenye utambuzi kuhusu hila zao tangu msaada huu uanze katika miaka ya 1950. Msaada huo unajumuisha kuunga mkono nakisi ya bajeti na deni kubwa ambalo lilisababishwa na Amerika, kupitia chombo chake, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Misheni nyingine za mikataba ya maelewano ni pamoja na ubinafsishaji wa miradi iliyofanikiwa, na kusitasita kuvinjari utajiri mkubwa ili kuhalalisha haja ya misaada hii. Umaskini nchini Jordan sio wa kikweli na haihitaji usaidizi wa kifedha au kisiasa wa Marekani. Bali inahitaji hukmu za Uislamu wa kweli na uongozi wa kweli wa Umma wa Kiislamu ili kuzuia kuporwa mali yake na kuondoa athari za mkoloni kafiri na ala zake.

Enyi Waislamu, enyi Watu wetu wa Jordan:

Ili kuikomboa nchi kutokana na ukoloni wa Marekani na Ulaya, katika mifumo yake yote ya kijeshi, kisiasa, kiuchumi na kithaqafa, ukoloni huu lazima ufurushwe. Misaada ya kifedha iliyounda haja yake wakati nchi za Kiislamu zimebarikiwa kuwa na mali, na ambayo tawala tegemezi zimekubali na kutekeleza upigiaji debe wake ili kudumisha utulivu wa utawala wao, tawala hizi pasi na budi zitatoweka kwa sababu zinategemea nguvu za ukafiri na ukoloni, ambazo hazitadhurika kwa kuzitelekeza kama zilivyowatelekeza walio kuwa kabla yao, na hapo ndipo mkoloni wa Kimagharibi atakapokuwa kwenye makabiliano ya kweli na Umma huu hivi karibuni. Umma huu uko katika juhudi za kuendelea kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kuregea kwa Dola ya Khilafah Rashida.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu