Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 8 Safar 1442 | Na: 1442/04 |
M. Ijumaa, 25 Septemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Makubaliano ya Imarati na Bahrain Pamoja na Umbile la Kiyahudi ni Khiyana Kubwa dhidi ya Palestina
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh iliandaa Visimamo vya Kulaani dhidi ya Makubaliano Haya
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh leo (Ijumaa, 25/09/2020) baada ya swala ya Ijumaa iliandaa maandamano katika misikiti tofauti tofauti jijini Dhaka na Chittagong dhidi ya makubaliano ya khiyana ya Imarati na Bahrain pamoja na umbile la Kiyahudi. Wazungumzaji walisema: Jumanne iliyopita (15/09/2020) katika mji ule mkuu mweusi Washington, Imarati na Bahrain zilitia saini makubaliano ya khiyana kubwa kwa eneo la safari ya Isra' na Mi'raj ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) bila ya kumcha Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waumini! Katika kuwafichua watawala wengine wa Kiislamu, wazungumzaji pia walisema: Wale ambao bado hawajatia saini makubaliano haya yaliyotangazwa sio duni kidaraja na waliotia saini, kwani Oman ni mwenyeji na ni mgeni wa umbile la Kiyahudi, na Qatar ni mpatanishi asiye na upendeleo kati ya Mayahudi na Gaza! Serikali ya Saudia umefungua nafasi ya anga kwa ndege za kivita za umbile hilo kikatili, na serikali ya Uturuki bado ingali inalitambua umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu Palestina!
Wazungumzaji pia walisema: Palestina ni nchi iliyobarikiwa, ardhi ya Al-Quds, ardhi ya Isra 'na Mi'raj, iko katika nyoyo za Waislamu, Palestina na Al-Quds yake ni Palestina ya Waislamu, na sio ya watawala hao wasaliti. Usawazishaji mahusiano yao na umbile la Kiyahudi, mnyakuzi wa Palestina, kutawavisha taji na fedheha na udhalilifu.
Wakiwahutubia Waislamu, wazungumzaji walisema: Kuling'oa Umbile la Kiyahudi na kuirudisha Palestina kwa watu wake wenyewe kunaweza tu kufanywa kupitia kuhukumu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu na kupitia majeshi yanayotikisa maadui wa Mwenyezi Mungu (swt). Na hili laweza kupatikana pekee kupitia kurudi kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt) hili litatokea hivi karibuni, limethibitishwa na dalili zilizokatikiwa kupitia mambo manne:
Kwanza: (كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ) “Nyinyi mmekuwa bora ya umma ulio tolewa watu” [Al-i-Imran: 110]. Na taifa la Dola hii halitavumilia dhulma, hivyo basi halitaisahau Al-Quds yake, bila ya kujali kila ambacho madhalimu wanakifanya, bali litawakanyaga juu yao kwa miguu yake …
Pili: Ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ukhalifa katika ardhi:
(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ)
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi Allah” [An-Nur: 55].
Na bidhara njema kutoka kwa Mtume (saw) ya kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume.
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” (Imepokewa na Ahmad).
Tatu: Hadith ya kupigana na kuwauwa Mayahudi,
«لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ، حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ»
“Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na mtawauwa, mpaka jiwe litasema: Ewe Muislamu, huyu hapa Yahudi (amejificha nyuma yangu); basi njoo umuue.” (Imesimuliwa na Muslim).
Nne: Chama chenye ikhlasi, uaminifu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kinachofanya kazi kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na bishara njema ya Mtume Wake (saw). Kilicho na maono na upeo, kinauongoza Ummah katika kheri inayouamsha kwa utukufu na ushindi.
(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاء وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)
“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
Mkusanyiko wa Picha
https://domainnomeaning.com/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/bangladesh/1129.html#sigProId1400f406e8
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |