Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  3 Safar 1442 Na: 1442 H / 03
M.  Jumapili, 20 Septemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Upigaji Marufuku wa Usafirishaji Nje Vitunguu Nchini India Umefichua Maumbile Halisi ya Watawala wa Kisekula wa Bangladesh Ambao Hawaoni Aibu Kujifanya kama Vinywa vya Washirikina Maadui.

Wakati ambapo India imeweka marufuku ya ghafla kwa usafirishaji wake wa kitunguu kwenda Bangladesh, watawala wetu wa vibaraka wamekuja kuokoa sura ya adui huyu mshirikina kwa kujifanya kama mdomo wake. Badala ya hata kujifanya kuikosoa India, Waziri wa Kigeni asiyejimudu kabisa AK Abdul Momen alikuwa mwepesi kuitetea India, akisema kwamba Wizara ya Kigeni ya India "inatubu" sana kwa kutoiarifu Bangladesh kabla ya marufuku hii! Na kinaya iliyoje kwamba siku ambayo India ilisimamisha ghafla mamia ya malori yake yaliyo na vitunguu kuingia Bangladesh, serikali ya Hasina ilituma tani 1,450 za Hilsha kwenda India siku hiyo hiyo kama zawadi ya Durga Puja kwa kuondoa marufuku ya usafirishaji wa Hilsha! Hakika, Hasina yuko tayari kuuza maisha ya Ummah kwa fadhila kutoka kwa dola hii a kiadui Kishirikina. Kwa hivyo, haishangazi kwamba Hasina anapeana maji ya Mto Feni kwa India, wakati India inalemaza kilimo, upanzi wa mimea, uvuvi na riziki yetu kwa kuzuia maji kupitia ugaidi wake wa maji ya mto. Mwaka jana wakati marufuku ya vitunguu ya India ilisababisha mateso makubwa nchini Bangladesh, badala ya kuchukua msimamo mkali, Sheikh Hasina asiye na haya alizungumza kwa ujinga katika ziara yake ya India kwa kufanya mzaha ambao alimwagiza mpishi wake kuandaa chakula bila kitunguu. Hata baada ya 'diplomasia ya kitunguu' mbaya ya India inayoendelea, serikali ya Hasina imeiweka sekta hii muhimu katika huruma ya adui kwa kuagiza kwa makusudi asilimia 75 ya vitunguu kutoka India.

Sasa watawala wetu watumwa wa kisekula wamekuwa duni zaidi hata hawaoni aibu kuuokoa uso wa Mshirikina adui wetu wa dhati. Wakati raia wetu wasio na silaha wanauawa na mamluki wa India wa BSF katika maeneo ya mpakani, badala yake watawala wetu wasaliti wanamtetea adui kwa kuwatuhumu wahasiriwa kama walanguzi ("Siwezi kulaumu wengine kwa mauaji ya mpakani wakati wanapotekeleza ulanguzi wa ng'ombe: Waziri", www. theindependentbd.com, Januari 25, 2020).

Enyi Waislamu, hakuna heshima, hadhi wala ustawi chini ya uongozi wa khiyana wa watawala hawa wa kisekula. Utumwa wao hautaacha uchumi wetu ujitegemee. Wanahatarisha uhuru wetu wa chakula kwa makusudi kwa kuifanya sekta muhimu ya kilimo kutegemea dola ya Kishirikina. Kwa kuongezea, kwa kukabidhi rasimali zetu za kistratejia kama bandari za bahari na sekta za kawi, na miundombinu ya reli na barabara kwa Washirikina Makafiri, watawala hawa wasaliti wanauvunja uti wetu wa mgongo ili tusiweze kusimama imara wakati Khilafah Rashidah aliyoahidiwa kwa njia ya Utume itakaporudi hivi punde kutoka Bangladesh bi idhnillah. Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inawaomba muongeze bidii yenu maradufu na mushirikiane mkono kwa mkono na chama hiki chenye ukweli kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili, ambayo ndicho chanzo pekee cha heshima na utukufu wetu. Umar ibn al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alisema,

"إِنَّا كُنَّا أَذَلَّ قَوْمٍ فَأَعَزَّنَا اللَّهُ بِالْإِسْلَامِ فَمَهْمَا نَطْلُبُ الْعِزَّةَ بِغَيْرِ مَا أَعَزَّنَا اللَّهُ بِهِ أَذَلَّنَا اللَّهُ"

“Hakika, sisi tulikuwa watu wadhalilifu mno na Mwenyezi Mungu akatupa utukufu kwa Uislamu. Na pindi tutakapotafuta utukufu kwengine kusikokuwa kwa kile alichotutukuza kwacho Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.” [al-Mustadrak, 214]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu