Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 9 Rabi' I 1439 | Na: 1439/005 |
M. Jumatatu, 27 Novemba 2017 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katili I. Karimov Amekufa, lakini Serikali Yake Bado Ingalipo!
Kuanzia asubuhi na mapema mnamo 14 Novemba kulianza misako mikali katika jiji kuu la Uzbekistan, Tashkent, katika majumba ya Waislamu walio nasibishwa kwa njia moja au nyengine na chama cha kisiasa cha Hizb ut Tahrir. Misako hii ilifanywa kwa muda wa siku kadhaa matokeo yake ni kukamatwa kwa zaidi ya Waislamu 80. Baada ya kuhojiwa kwa muda mrefu, Waislamu 7 walitiwa nguvuni. Wakati wa kuhojiwa huko waliulizwa kuhusu kujihusisha kwao na Hizb ut Tahrir.
Waliotiwa nguvuni ni jamaa za mmoja wa mashuhadaa wa kwanza wa Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan Farhad Usmanov, Allah amuwiye radhi. Hususan, mkewe Musharraf Khudoiberdiyeva alitiwa nguvuni. Vile vile jamaa yake Farhad, Uzakova Nasiba, bintiye Umida, mumewe Umida na mtoto wao Muhammadamin pia walitiwa nguvuni. Wote hawa wamewekwa chini ya mvungu wa jumba la Kitengo cha Mambo ya Ndani jijini Tashkent, na hawaruhusiwi kukutana kwa zaidi ya muda wa wiki moja, na pia hawaruhusiwi kuletewa chakula wala nguo na kupigwa marufuku kutembelewa na wakili.
Mnamo 16 Novemba, polisi kwa niaba ya maafisa wa Ashonguzar ROVD (Kitengo cha Mambo ya Ndani ya Wilaya) cha Tashkent Nuriddinov Ibrokhim, pamoja na mchunguzi Sukhrob Bakhromovich, walipekuwa nyumba ya familia ya Dildora Agzamova, ambapo baadaye mwanawe Nasrulloch alikamatwa. Tangu kukamatwa kwa mwanawe, mpaka leo hana taarifa yoyote aliko mwanawe, ingawa, kabla ya kupelekwa katika kitengo cha ROVD, mchunguzi Sukhrob Bakhromovich alimuahidi mamake Nasrulloch kwamba mwanawe angerudi baada ya muda wa saa moja. Pia, hakuna taarifa yoyote kuhusu Rashodov Muhammad Abdukarimovich aliyekamatwa na Kitengo cha Uchtepa ROVD cha Tashkent kwa zaidi ya wiki moja.
Misako hii na kushikwa huku, pamoja na ukweli kuwa mashabab wa Hizb ut Tahrir wamekuwa ndani ya magereza ya Uzbekistan kwa muda wa miaka 20 na bado wangali hawaja achiliwa huru, ladhihirisha wazi kuwa kwa kufariki katili I. Karimov, hakuna mabadiliko yoyote nchini humu, bali serikali ya kitwaghut inaendelea na uhalifu wake.
Raisi mpya wa Uzbekistan, Shaykat Mirziyoyev, ili kupata afueni kutokana na vikwazo vilivyo ekewa Uzbekistan na jamii ya kiulimwengu wakati wa utawala wa I. Karimov, anajaribu kuwahadaa watu na jamii ya kiulimwengu kwa kudai kuleta mabadiliko katika mueleko wa kisiasa nchini humo. Mashirika yanayodaiwa kutetea haki za kibinadamu, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za kibinadamu, maafisa wakuu kutoka kwa Muungano wa Ulaya wametembelea nchi hiyo, makongamano ya kimataifa yanafanywa na mambo mengine mengi, lakini yote haya ni usanii!
Katika magereza ya kitwaghut ya Uzbekistan, kwa ridhaa ya mashirika haya na dola hizi kwa njia ya kunyamazia kimya, yanaendelea kuwatesa na kuwaua Waislamu, kuwanyanyasa wanawake wa Kiislamu, ambapo kwa sasa hawawezi hata kutoka nje wakiwa wamevalia hijab, kwa kuhofia kukamatwa na kuvuliwa nguo hadharani. Mama za wale walio hukumiwa walisema wazi wazi kuwa watoto wao walioko magerezani wanateswa kwa kumwagiwa maji moto yanayo chemka katika sehemu zao nyeti kwa kosa tu la kuswali, kama ilivyo tokea hivi majuzi katika gereza Nambari 64/46 katika mji wa Navoi.
Enyi Waislamu wa Uzbekistan! Mola wetu ni Allah (swt)! Mtume wetu ni Muhammad (saw)! Dini yetu ni Uislamu! Ufanisi na uokovu wetu uko katika Uislamu pekee! Musimuogope twaghut na watumwa wake. Allah (swt) yu pamoja nasi! Harakisheni katika kuiangamiza serikali ya kikatili! Jiungeni na Hizb ut Tahrir na mufanye kazi ya kusimamisha tena dola ya Khilafah Rashida katika Njia ya Utume kwani ndiyo inayo miliki uokovu wenu na ndani yake ndiyo izza yenu na mwamko wenu!
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.domainnomeaning.com |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) domainnomeaning.com |