Chini ya sera ovu ya uhamiaji ya ‘kutokuwa na hata chembe ya uvumilivu’ ya Raisi wa Amerika, takriban watoto 2000, wengine wao wakiwa na umri mdogo wa miaka 4 au 5, ni miongoni mwa wale walioorodheshwa kama ‘wahamiaji haramu’, wametenganishwa kwa nguvu kutoka kwa wazazi wao katika mpaka wa Amerika na Mexico katika kipindi cha wiki sita pekee. Wametiwa ndani ya vibanda vya seng’enge katika vituo vya vizuizi, ambavyo hali zake zimesifiwa kuwa ‘mithili ya gereza’. Mojawapo ya vituo hivi vya wahamiaji katika jimbo la Texas kimepewa lakabu ya La Perrera, “kibanda cha mbwa”, ambamo watoto wanalala chini sakafuni juu ya magodoro membamba na makaratasi ndio blanketi zao. Kanda ya sauti ya watoto walioathirika kimawazo na kulia imepatikana, wakililia wazazi wao. Idara zimetangaza mipango ya kujenga mahema yatakayobeba mamia zaidi ya watoto katika jangwa la Texas ambako viwango vya joto kawaida hufikia nyuzi 40.