Jumanne, 12 Sha'aban 1446 | 2025/02/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Mabadiliko Mapya ya Kisiasa nchini Lebanon

(Imetafsiriwa)

Swali:

Al-Araby Al-Jadeed ilichapisha kwenye tovuti yake tarehe 21/1/2025: “... Nawaf Salam aliondoka baada ya kukutana na Rais Joseph Aoun jioni ya leo, Jumanne, kwenye Kasri la Baabda, akiwa amebeba faili jeusi mkononi mwake bila kufichua iwapo aliwasilisha rasimu ya majina yoyote au muundo wa baraza la waziri...”, ikibainisha kuwa: Baada ya nafasi ya urais kuwepo kwa zaidi miaka miwili kutokana na tofauti za kisiasa, bunge la Lebanon lilimchagua Aoun kama rais wa Lebanon mnamo 9/1/2025. Siku nne baada ya kuchaguliwa kwake, Aoun alimpa Nawaf Salam jukumu la kuunda serikali mpya ya Lebanon. (Al-Jazeera 20/1/2025).

Ni yapi yanayojiri nchini Lebanon kuhusu wepesi wa makubaliano juu ya uteuzi wa Kamanda wa Jeshi Joseph Aoun kama rais mnamo 9 Januari 2025 baada ya nafasi hiyo kudumu kuwepo kwa zaidi ya miaka miwili, kisha siku chache baadaye makubaliano kwa Salam Nawaf kuwa kama waziri mkuu mnamo 13 Januari 2025? Haya yote yalitokeaje haraka hivyo? Je, kasi hii ina maana kwamba kazi ilikuwa na bado ingali inatayarishwa kubadilisha uso wa Lebanon ndani na nje, au ni mabadiliko ya kawaida, kama inavyotokea katika kanda hiyo?

Jibu:

Ili kufafanua majibu ya maswali ya hapo juu, lazima tupitie yafuatayo:

Kwanza: Maendeleo makubwa ya kisiasa katika kanda na dunia ndiyo yaliyosababisha mabadiliko haya ya haraka nchini Lebanon. Kisha Aoun akachaguliwa kuwa Rais wa Lebanon, na Nawaf Salam akateuliwa kuwa waziri mkuu. Ili kufafanua hili, tunasema:

1- Muda mfupi baada ya kuuawa kwa viongozi wa chama cha Iran na umbile la Kiyahudi na kabla ya kusitishwa kwa mapigano, wito uliibuka nchini Lebanon kumchagua rais na kusitisha uwazi katika nafasi hiyo. Wito huu uliongozwa na wapinzani wa chama cha Iran, kama vile kikundi cha Samir Geagea, ambacho kilikataa waziwazi kuunga mkono Gaza katika vita. Huu ulikuwa upatilizaji wa hali iliyotokana na vita, na ilikuwa ni kwa ushauri kutoka kwa wajumbe wa Ulaya waliokuwa wakizuru Lebanon sambamba na ziara za mjumbe wa Marekani Hochstein, ambazo zilizingatia usitishaji wa mapigano. Chama cha Iran kilikuwa kikishutumu wito huu kutoka kwa upinzani wa Lebanon.

2- Baada ya vikao 12 kushindwa kumchagua rais nchini Lebanon katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, vikosi mbalimbali vya kisiasa nchini Lebanon vilikubali karibu ghafla, Kamanda wa Jeshi Joseph Aoun alichaguliwa kuwa rais mpya ili kumaliza uwazi katika nafasi hiyo. Chama cha Iran kilikuwa kimetangaza kuwa mgombea wake ni Suleiman Franjieh. (Al-Alam Channel, 7/1/2025) Franjieh anahusishwa na mhimili wa Iran na utawala uliokufa wa Bashar, kisha Suleiman Franjieh alitangaza kujiondoa ugombea wake ili kufikia makubaliano.

3- Wafuasi wa mhimili wa Iran (chama chake na vuguvugu la Amal) hawakumchagua Joseph Aoun katika kikao cha kwanza, kumaanisha kuwa kura ilishindwa kutokana na kutopata theluthi mbili (kura 86). Kisha katika kikao cha pili na baada ya mkutano na kambi hizi za wabunge, walimpigia kura na akapata kura 99. Kwa hivyo, kura ya Joseph Aoun katika kikao cha pili ililenga kuonyesha kwamba kama si kura za Chama cha Iran na Harakati ya Amal, Joseph hangeshinda urais. Ingawa hii ina maana fulani kwa kuwa ushawishi wa wafuasi wa Iran bado upo na kwamba wanaathiri kura, kuacha kwao kizuizi, ambacho wana uwezo nacho, kunamaanisha kurudi nyuma.

4- Mnamo tarehe 13/1/2025, Waziri Mkuu mpya aliteuliwa kwa ajili ya Lebanon, Nawaf Salam. Alipandishwa cheo kama mgombea wa maridhiano ya kisiasa, kwani yeye si Najib Mikati, mgombea wa Chama cha Iran na washirika wake, wala Fouad Makhzoumi, mgombea wa kundi la Samir Geagea, yaani wapinzani wa Chama cha Iran. Hivyo, Nawaf Salam aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu nchini Lebanon.

5- Nawaf Salam alikuwa mgombea aliyekataliwa na chama cha Iran na vikosi vinavyoshirikiana nacho nchini Lebanon. Chama cha Iran kilimkataa mnamo 2019 baada ya kujiuzulu kwa Saad Hariri na kumwita “mgombea wa Amerika” wakati huo. Hassan Diab aliteuliwa wakati huo, na chama kilikataa uteuzi wake tena mwaka uliofuata baada ya mlipuko wa bandari ya Beirut mnamo 4/8/2020.

 6- Inaonekana kwamba chaguo hili lilikasirisha chama cha Iran na Harakati ya Amal: Mwandishi wa Al Jazeera aliripoti mnamo tarehe 13/1/2025 kwamba kambi ya bunge ya Hezbollah haikuteua mgombea yeyote wa waziri mkuu wa Lebanon. Kufuatia mkutano wa wawakilishi wa kambi ya Hezbollah na rais wa Lebanon kumteua waziri mkuu, mwakilishi wa chama hicho, Muhammad Hassan Raad, alielezea masikitiko yake na kusema kwamba baadhi wanafanya kazi ya kulitenga na kuliondoa kundi hilo. Aliongeza, katika taarifa kwa waandishi wa habari, “Tulichukua hatua chanya katika mkutano wetu na rais wa jamhuri, lakini hatukunyoshewa mkono,” akisisitiza kuwa kundi hilo litachukua hatua kwa utulivu na busara ili kulinda maslahi ya kitaifa.

Duru iliyo karibu na Hezbollah iliripoti kwamba chama hicho na mshirika wake, Viguvugu la Amal, linaloongozwa na Spika wa Bunge Nabih Berri, wanaunga mkono kuteuliwa tena kwa Mikati kama waziri mkuu. Alieleza kuwa kuteuliwa tena kwa Mikati ni “sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na mjumbe wa Saudia nchini Lebanon, Yazid bin Mohammed bin Fahd Al Farhan, ambayo yalipelekea Hezbollah na Amal kuendelea na uchaguzi wa Aoun kama rais Alhamisi iliyopita.” Katika muktadha huo huo, BBC iliripoti mnamo tarehe 13/1/2025 kutoka kwa mkuu wa kambi ya Chama cha Iran bungeni kwamba kuteuliwa tena kwa Aoun ni “sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na mjumbe wa Saudia nchini Lebanon, ambayo yalipelekea Hezbollah na Amal kuendelea na uchaguzi wa Aoun kama rais.”

Pili: Hii ilikuwa njia ya matukio nchini Lebanon; bunge lilimchagua rais mpya na kumteua waziri mkuu mpya pia. Baada ya uchunguzi wa kina, tunapata yafuatayo:

1- Tunaona kwamba Amerika imeridhika kabisa na maendeleo mapya ya kisiasa nchini Lebanon, au tuseme, ndiyo inayohusika nayo. Rais Biden alisema katika taarifa yake: “Ninampongeza kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Lebanon,” na akaendelea: “Rais Aoun atatoa uongozi muhimu huku Lebanon na ‘Israel’ zikitekeleza kikamilifu usitishaji wa uhasama na huku mamia ya maelfu ya watu wakiregea makwao na Lebanon kupata nafuu na kujijenga upya. Rais Aoun ana imani yangu. Ninaamini kwa dhati kuwa ndiye kiongozi anayefaa kwa wakati huu.” (CNN Arabic, 9/1/2025). Pia, kibaraka wa Amerika Mohammed bin Salman pia alimpongeza huko Saudi Arabia (Al-Hurra, 1/9/2025).

2- Kwa hivyo, maendeleo mapya ya kisiasa nchini Lebanon hayana uhusiano wowote na mzozo wa kimataifa juu yake. Lebanon ilikuwa mikononi mwa Amerika wakati wa urais wa Michel Aoun, ambaye alionekana kama sehemu ya mhimili wa Iran. Rais wa sasa, Joseph Aoun, aliteuliwa kuwa kamanda wa jeshi mnamo 2017 na kibaraka wa Amerika, Michel Aoun. Hii ina maana kwamba rais wa sasa, Joseph Aoun, kiasili anatoka katika kinu cha vibaraka wa Marekani. Kwa kweli, Amerika, kabla na baada ya urais kuwa wazi mnamo 2022, ilitoa msaada wa kijeshi kwa jeshi la Lebanon. Hii ina maana kwamba ina uhusiano wa karibu na Kamanda wa Jeshi Joseph Aoun. Nawaf Salam, ambaye alitumia maisha yake kufundisha na kuelimisha katika vyuo vikuu vya Ufaransa na Amerika na taasisi za kimataifa, hivi karibuni kama rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, hawezi kuwa nje ya mfumo huu pia.

3- Kwa hivyo, Amerika leo inabadilisha sheria za mchezo wake nchini Lebanon. Baada ya kuzoea kuitegemea Iran, mhimili wake, na vikosi vinavyoshirikiana nayo nchini Lebanon kuimarisha ushawishi wake, leo hii inazitenga nguvu hizi kwa kupendelea kuangazia tarakimu mpya za kuendeleza ushawishi wake nchini Lebanon. Lebanon ilikuwa katika mtego wa Amerika na bado iko, lakini Amerika inabadilisha sura na umbo lake.

4- Ama dola zinazofungamana na Wazungu, wanajua kuwa nguvu zao sio muhimu kuliko uwezo wa Amerika. Ufaransa, kupitia ushiriki wake katika kamati ya wajumbe watano, ilikataa jina la Joseph Aoun kama mgombea urais tangu 2023 wakati jina lake lilipotangazwa mapema na Marekani na Saudi Arabia (Al-Araby Al-Jadeed, 22/9/2023), lakini hatimaye ililazimika kumkubali. Kwa upande mwingine, Wazungu wanakosa ushawishi wa kumfanya rais awe chini yao. Samir Geagea, ambaye ana kambi kubwa zaidi ya Wakristo bungeni, hakutangaza hata nia yake ya kuwania kiti cha urais kwa kuzingatia upinzani mkubwa wa kuteuliwa kwake kutoka chama cha Iran. Chama cha Iran kilisema, “Hakuna kura ya turufu kwa jina lolote isipokuwa Samir Geagea; kwa sababu mradi wake ni uharibifu kwa Lebanon.” (Asharq Al-Awsat, 6/1/2025), na pia ilikataa jina la mgombea Fouad Makhzoumi wa uwaziri mkuu, ambalo lilitolewa na vyama vya upinzani (RT, 13/1/2025). Kwa hivyo, mamlaka zinazofungamana na Wazungu haziwezi kuhodhi urais wowote kati ya tatu za Lebanon na nyadhifa hizi zimesalia mikononi mwa wafuasi wa Amerika.

5- Hata hivyo, Wazungu wanakubali maendeleo mapya ya kisiasa nchini Lebanon, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimpongeza Aoun kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Lebanon, katika tweet aliyoweka kwenye akaunti yake kwenye jukwaa la X. Macron aliona kwamba chaguzi hizi “zinafungua njia ya mageuzi na kuregeshwa kwa mamlaka na ustawi wa Lebanon.” (Al-Hurra, 10/1/2025). Kauli ya Rais wa Ufaransa inaakisi hali ya dola za Ulaya na furaha yao na kupungua kwa kivuli cha Iran juu ya Lebanon. Maana yake ni kwamba wameridhika na kufikia sehemu ya matamanio yao, ambayo ni kuiweka Lebanon kwenye njia iliyo mbali na Iran, na wameridhika na kuwepo katika kamati ya watu watano ya kusimamia masuala ya Lebanon ambayo iliundwa baada ya nafasi ya rais kuwa wazi, kwani Ufaransa inakaa humo bega kwa bega na Marekani, Misri na Saudi Arabia, huku Qatar ikiwakilisha maslahi ya Waingereza ndani yake.

Yaani, Marekani ndiyo mdau mkuu wa kimataifa wa Lebanon leo hii, na ndiyo inayobadilisha sura na umbo, huku Wazungu wakiridhika na hayo yote kwa kukiondoa kivuli cha Iran kutoka Lebanon.

Tatu: Ama kuhusu kubadilisha sura ya Lebanon ndani na nje, hili liko wazi kutokana na mambo yafuatayo:

 1- Kwa upande wa kindani nchini Lebanon, kuna uwezekano kwamba vizuizi vya silaha za chama cha Iran vitaongezeka, kwani haja ya “upinzani” ambao hapo awali uliambatana na kauli na matamko ya rais wa Lebanon umetoweka na haukuwepo katika matamshi ya rais mpya:

a- (Tofauti na hotuba za kawaida zilizokuwa na sifa za enzi zilizopita baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Lebanon, hotuba ya Aoun ilikuja imejaa ujumbe wazi, hasa msisitizo wake juu ya umuhimu wa “kuweka haki ya serikali ya kuhodhi silaha” kama nguzo ya msingi ya kuimarisha ubwana wa Lebanon. (Al-Hurra, 10/1/2025). Aoun alisema katika hotuba yake: serikali ya Lebanon - na nauria tena serikali ya Lebanon - itaondoa uvamizi wa ‘Israel’ (CNN Arabic, 10/1/2025).

b- Nawaf Salam alitoa maoni yake kuhusu uvujaji wa vyombo vya habari kuhusu ugawaji wa nyadhifa kwa vyama vya jadi na pia kuendelea kwa mujibu wa masharti ya Hezbollah na Harakati ya Amal, hasa kwa kuwapa Wizara ya Fedha ... Salam aliongeza kuwa “hakujitolea kutoa wizara yoyote kwa chama chochote, ama Wizara ya Fedha, ni kama wizara nyingine zote na sio ukiritimba kwa dhehebu fulani”... akisisitiza kuwa anaegemea kwenye serikali ya mawaziri 24... (Al-Araby Al-Jadeed, Januari 21, 2025).

2- Kwa nje, wakati wa kutafakari yanayotokea, yafuatayo yanabainishwa:

a- Katika hali isiyo ya kawaida, Iran haijaonyesha dori yoyote katika kuchagua rais na waziri mkuu, ingawa dhati ya dori hii ipo nyuma ya misimamo ya chama chake nchini Lebanon, na kwa sababu chama cha Iran na washirika wake wanaweza kuzuia maendeleo haya na hawajafanya hivyo. Kwa hiyo, mabadiliko haya ya Marekani, ambayo yameelezwa kuwa mapinduzi, yanafanyika kwa idhini kamili ya Iran. Ushawishi wa Iran kwa kweli unapungua kutoka kanda ya Arabuni. Amerika imeikabidhi Uturuki suluhisho la kisiasa nchini Syria, na imeiondoa Iran kutoka kwayo, kama ilivyoiondoa Urusi kutoka kwa mlinganyo wa Syria kikamilifu. Hii ni sera mpya ya Amerika katika kanda, na hivi ndivyo ilivyofanya nchini Lebanon. Sio tu sera ya utawala wa Biden, lakini utawala unaofuata una maono sawa, na utafanya kazi ya kuimarisha zaidi nchini Syria na Lebanon na upanuzi wake hadi Iraq. Sera hii ya Marekani inaendana kabisa na kile ambacho umbile la Kiyahudi linataka, na inaweza kuwa moja ya ahadi ambazo utawala wa Biden ulitoa kwa umbile la Kiyahudi wakati ilipolihimiza kukubali kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon.

b- Inaonekana kwamba rais mpya wa Lebanon anatambua kwamba Marekani inamleta katika hatua hii kwa mabadiliko makubwa yatakayoikabili Lebanon, Rais Aoun alisema mwanzoni mwa hotuba yake ya kuapishwa, “Wawakilishi waheshimiwa wameniheshimu kwa kunichagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Lebanon, ambayo ni medali kubwa zaidi ninayobeba na jukumu kubwa zaidi, hivyo nikawa rais wa kwanza baada ya karne ya kwanza ya kuanzishwa kwa dola ya Lebanon kubwa zaidi, katikati ya tetemeko la ardhi la Mashariki ya Kati ambalo kwalo miungano imevunjika, tawala zimeanguka, na mipaka huenda ikabadilika.” (Independent Arabia, 11/1/2025)). Kwa mujibu wa chanzo hicho hicho, ataelekea Saudi Arabia kama eneo lake la kwanza la kigeni, “Rais wa Lebanon Joseph Aoun alisema leo, Jumamosi, kwamba Saudi Arabia itakuwa nchi yake ya kwanza ng’ambo, baada ya kupokea mwaliko wa kuitembelea wakati wa maongezi ya simu aliyofanya na Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman.”

c- Pia ni wazi kutokana na haya yote kwamba Amerika inaipa Saudi Arabia jukumu la kushughulikia suala la Lebanon wakati huu, baada ya kukabidhiwa Iran hapo awali. Ndio maana nafasi ya Saudia itakuwa kubwa katika masuala ya Lebanon, na itakuwa na mkono katika ujenzi upya, hasa kwa vile inatarajiwa kwamba Iran itakuwa chini ya mashinikizo mapya ya kibiashara na kifedha yaliyowekwa juu yake na utawala wa Trump. Kwa hivyo Saudi Arabia itakuwa badali ya Iran nchini Lebanon, kutoka nyanja ya kisiasa na kifedha kwa ajili ya ujenzi upya na kusaidia serikali kuimarisha jeshi lake na kuwezesha kupokonya silaha chama cha Iran. Hii inaweza kuiburuza Lebanon katika kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi, haswa kwa vile Rais ajaye wa Marekani Trump anaharakisha uhalalishaji mahusiano wa Saudia na umbile la Kiyahudi.

Nne: Hali hii ya kuogofya inaelekea kuendelea nchini Lebanon na pambizoni mwa Lebanon hadi Mwenyezi Mungu atakapoleta jambo lililoahidiwa, kisha dola ya Kiislamu, dola ya Khilafah isimamishwe, na nguvu zote hizi za kisiasa zitatoweka kutoka Lebanon na pambizoni mwa Lebanon, na pamoja nazo umbile la Kiyahudi, kama vile utawala wa Assad ulivyoyeyuka kutoka Syria. Kisha ardhi ya Ash-Sham itaregea kama ilivyokuwa siku zote, kuwa moyo unaodunda wa Ummah wote wa Kiislamu. Tuna yakini na kuregea Khilafah kwa mara nyingine tena baada ya utawala huu dhalimu tunaoishi ndani yake. Imepokewa kutoka kwa Ahmad kutoka kwa Hudhayfah ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha utakuwa utawala dhalimu (ملكًا جبرية), na utadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza”.

Popote itakaposimamishwa, itafika Ash-Sham na kukaa hapo. Al-Tabarani amepokea kutoka kwa Salamah bin Nufayl, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «عُقْرُ دَارِ الإِسْلامِ بِالشَّامِ» “Kitovu cha nyumba ya Uislamu kiko Ash-Sham”.

Itapigana na Mayahudi na itaondoa umbile lao linaloikalia kimabavu ardhi iliyobarikiwa na itairegesha Palestina kikamilifu kwenye nyumba ya Uislamu, na kesho iko karibu kwa wanaoiona. Lakini sheria ya Mwenyezi Mungu imetaka kwamba Yeye (swt) asiteremshe Malaika kutoka mbinguni ili kutusimamishia Khilafah inayopigana na adui yetu huku sisi tukiwa tumekaa, bali Yeye (swt) huwateremsha Malaika Wake wawe wasaidizi na bishara ya ushindi wake kwa watu waliomuamini Mola wao Mlezi, na akawazidishia uwongofu, wanajeshi Waislamu, subira katika vita, wenye kulindwa na Imam wao na kupigana na maadui zao nyuma yake. Na kisha tutakuwa miongoni mwa wale wanaostahiki kupata bishara hiyo njema.

[نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“… nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saf: 13].

23 Rajab 1446 H

23/1/2025 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu