Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Matarajio ya Wakoloni Nchini Tanzania
(Imetafsiriwa)

Swali:

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye utulivu zaidi wa kisiasa barani Afrika. Tanzania inacheza dori katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Uhusiano wake na mkoloni wake wa zamani Uingereza ni imara. Lakini tunaona harakati za Marekani na China ndani yake. Je, ni kipi kiwango cha ushawishi wa Marekani na China katika nchi hii? Je, kuna mzozo wa kimataifa ndani yake? Na kwa nini kundi la SADC lilianzishwa?

Jibu:

Ili kupata jibu wazi kwa maswali hayo hapo juu, tunahakiki mambo yafuatayo:

Kwanza: Tanzania ni nchi ya Kiislamu, asilimia ya Waislamu ndani yake inazidi 60%. Uislamu uliingia humo mwishoni mwa karne ya kwanza ya Hijri, lakini ulikabiliwa na mashambulizi ya wakoloni, maadui wa Uislamu, kuanzia ukoloni wa Wareno hadi ukoloni wa Wajerumani na Waingereza, na Marekani sasa iko kwenye njia ya kuingilia kati... Eneo lake la kimkakati linaifanya kuwa muhimu kwa nchi za kikoloni, iko kwenye Bahari Hindi kutoka kwenye mipaka yake ya mashariki, na iko ndani ya eneo la Maziwa Makuu ya Afrika. Kwa sababu hiyo, ulikuwa ni mlango mmojawapo wa wakoloni kupenya kwenye kina kirefu cha Afrika na kuikoloni. Tanzania ilipata uhuru wake rasmi mwishoni mwa 1961, lakini ushawishi wa Waingereza uliendelea kuitawala.

Pili: Uingereza ilimteua Julius Nyerere kama rais wa Tanganyika, ambaye alionekana kuongoza harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni! Hapo awali aliteuliwa kuwa waziri katika serikali ya Uingereza iliyoendesha eneo hilo kabla ya uhuru. Zanzibar ilitwaliwa na Tanganyika mwaka 1964, ili kuunda Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa mpango wake, iliouandaa kusimama dhidi ya Marekani, ambayo ilianza kufanya kazi ya kuchukua nafasi ya ukoloni mkongwe barani Afrika. Nyerere alitawala Tanzania kwa chuma na moto hadi 1985, akiunganisha ushawishi wa Waingereza na kupiga vita Uislamu. Alikuwa akijificha nyuma ya kauli mbiu ya mapinduzi na ujamaa katika wakati ambapo alikuwa akitabikisha mfumo wa kirasilimali kama ilivyo desturi ya mawakala wengi wa nchi za Magharibi.

Tatu: Kwa sababu Waislamu ndio wengi (zaidi ya 60%), na ili rais asitokee kwao, iwapo kungekuwa na uchaguzi wa rais, waliweka katiba inayotamka katika ibara ya tatu ya Kifungu cha 47 kwamba “Ni lazima mgombea urais awe anatoka sehemu fulani ya muungano (Tanganyika au Zanzibar). Wakati huo huo, naibu anapaswa kutoka upande mwingine ". Kuna ufahamu na sio utaratibu wa kikatiba kwamba marais wakristo na waislamu wapishane. Baada ya kifo cha Rais Mkristo Julius Nyerere, aliyetawala kwa muda mrefu zaidi, kuanzia mwisho wa 1961 hadi 1985, Hassan Mwinyi mwenye asili ya Kiislamu alichukua madaraka (1985-1995), kisha Mkristo Benjamin William (1995-2005). na ndipo Rais Mrisho Kikwete mwenye asili ya Kiislamu akashika madaraka (2005-2015), kisha Mkristo akaingia madarakani, John Magufuli na akafariki mwaka jana. Baada ya hapo, naibu wake, Samia Hassan, mwenye asili ya Kiislamu, alichukua kiti cha urais tarehe 19/3/2021.

Samia Hassan alikuwa waziri katika serikali ya Zanzibar ndani ya Muungano. Mnamo 2014, aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi kwa Masuala ya Muungano. Mwaka 2015, Rais John Magufuli alimchagua kuwa Makamu wa Rais, akiwapiku wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama tawala cha Nyerere, kilichokuwa madarakani pekee, mara zote kilishinda kwa asilimia kubwa. Katika uchaguzi uliopita wa urais uliofanyika mwaka 2020, chama cha Nyerere kilishinda kwa 84.39%, na kisha mgombea wake Magufuli na makamu wake, Samia Hassan akashinda awamu ya pili, na hii inaashiria kuwa watawala wa Tanzania bado wanaifuata Uingereza, kwa sababu chama hicho tiifu kwake, chama cha Nyerere, bado kinatawala serikalini. ... Ili kuendeleza utamaduni uliokubalika wa kisiasa wa kupokezana madaraka, Samia Hassan alimteuwa aliyekuwa rais msaidizi wa zamani wa masuala ya uchumi, Philip Mbango, kuwa naibu wake ambaye ni Mkristo. Kumbuka kwamba rais Samia Hassan alizaliwa Januari 1960 nchini Zanzibar, ambayo inafurahia uhuru nusu wa utawala, na idadi ya Waislamu ndani yake ni karibu 99%. Baadaye niliendelea na masomo ya Utawala wa Umma kwanza nchini Tanzania kisha nikahitimu Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza. Alikula kiapo cha kikatiba akiwa amevaa hijabu na Qur’an mkononi mwake wa kulia, hivyo akajipatia sifa njema miongoni mwa watu wa nchi yake ya Waislamu, hasa kwa vile alifuata njia isiyo ya kugombana na upinzani.

Nne: Uingereza inaitazama Tanzania kwa kiasi fulani cha umuhimu kutokana na nyanja ya kisiasa na kiuchumi.

Ama kipengele cha kisiasa, eneo lake kama moja ya milango ya kuingia kwenye kina kirefu cha Afrika na ukoloni wake kunaifanya kuwa muhimu kwao. Uingereza imefanya kazi ya kusimama dhidi ya kuenea kwa Uislamu na kuupiga vita na watu wake wanaomkataa mkoloni na kukabiliana naye. Uingereza kuipoteza Tanzania kulisababisha ipoteze baadhi ya nchi jirani, ambazo Uingereza bado ina ushawishi ndani yake kama Kenya, Malawi, Zambia na nchi nyingine katika eneo hilo.

Kwa upande wa kiuchumi, ni mwekezaji mkubwa wa kigeni wa moja kwa moja nchini Tanzania katika sekta za madini, viwanda na uzalishaji wa kilimo, na mwekezaji mkubwa wa chai ya Tanzania, na mauzo yake ya nje ndiyo yanatawala soko la Tanzania, hasa magari na vifaa vya kielektroniki.

Tano: Kadhalika, Marekani inaitazama Tanzania kwa kiwango fulani cha umuhimu na inajaribu kupata mwanya wa kuifikia kwa njia zote, na kubadilisha ukoloni mkongwe. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi chache za kiafrika ambazo marais wa Marekani walizizuru kwa ajili ya kuonesha nia yake na kujaribu kuivutia Marekani... Hivyo Bush Mwana alizuru Tanzania mnamo tarehe 17/2/2008. Vilevile Obama mnamo tarehe 1/7/2013, alipoweka jiwe la msingi la kumbukumbu mbele ya ubalozi wa nchi yake kwa heshima ya Wamarekani kumi na moja waliouawa katika shambulizi la bomu la mwaka 1998 katika ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam.

Sita: Kwa hivyo, inaweza kusemwa kwamba mzozo wa kisiasa unaendelea kati ya Uingereza, mkoloni mkongwe anaye endelea, na Amerika, ambayo inajaribu kupenya ndani ya Tanzania ili kufanikiwa ushawishi wa Kiingereza, na nchi zote mbili zinatumia njia zao mbaya za kikoloni kufikia malengo yao.

1- Kwa upande wa Amerika, imetangaza kupinga matokeo ya uchaguzi wa 2020. Morgan Ortagus, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, aliandika mnamo tarehe 30/10/2020 baada ya kutangazwa kwa ushindi wa Rais Magufuli. Aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter, akisema kwamba "alikuwa na wasiwasi kuhusu ripoti za kuaminika za dosari katika uchaguzi na matumizi ya nguvu dhidi ya raia wasio na ulinzi." Alisema, "Tutawajibisha watu binafsi kwa hili." Pia, Amerika inatabanni matakwa ya upinzani, haswa Chama cha Chadema. Huku ni kuleta machafuko ya kisiasa ili kuweza kuvunja utawala wa chama tawala, Chama cha Uingereza... Kumbuka kuwa upinzani bado ni dhaifu. Mgombea wa chama kikubwa cha upinzani cha Democratic and Progress Party (Chadema) hakupata asilimia kubwa katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka 2020. Mgombea wake Tundu Lissu alipata 13.03%. Mgombea wa Chama cha Chadema aliyakataa matokeo hayo na kusema “kilishuhudia udanganyifu usio na kifani katika historia yetu...” Kadhalika, Marekani inapatiliza wito wa kujitenga, hasa wito wa kujitenga kwa Zanzibar na Tanganyika... Inatumia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kama njia ya kuishawishi serikali nchini Tanzania!

2- Kwa upande wa Uingereza, inafanya kazi kwa mujibu wa mbinu yake chafu ya kisiasa kufunga milango ambayo Marekani inajaribu kuipatiliza nchini Tanzania, kwa upande mmoja inaonekana kukubaliana na Marekani, na kwa upande mwingine inafuata sera tofauti.

a- Kuhusu uchaguzi, Uingereza ilitoa tamko kuhusu hilo. Waziri wa Uingereza wa Masuala ya Afrika, James Doddridge, alisema kwenye akaunti yake ya Twitter mnamo tarehe 30/10/2020, ("Uingereza ina wasiwasi kuhusu habari kuhusu dosari" na kutoa wito wa "uchunguzi wa wazi" na kuhimiza vyama vya kisiasa "kutafuta suluhisho la amani”), Amerika iliridhika, lakini haikupinga matokeo ya uchaguzi, wala haikusema yale ambayo Amerika ilisema: (kwamba kuna ripoti za kuaminika za ukiukaji wa uchaguzi) au wito wa (uwajibikaji kwa wale waliohusika)!

b- Kwa upande wa upinzani, viongozi wa kundi la Kiislamu lililotaka uhuru kamili wa eneo lenye uhuru nusu wa kujitawala la Zanzibar nchini Tanzania walifutiwa mashtaka ya ugaidi: [Viongozi mashuhuri wa jumuiya ya kiraia, Jumuiya ya Uhamasishaji na Ulinganizi wa Kiislamu, au UAMSHO, waliachiwa huru baada ya kukaa kizuizini kwa miaka minane, Farid Hadi na Mselem Ali Mselem waliachiliwa Jumanne usiku, na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Sylvester Mwakitalu, aliwathibitishia waandishi wa habari kwamba mashtaka yote dhidi yao yamefutwa...” (https://apnews.com/)] na pia katika wiki za hivi karibuni iliruhusiwa kwa baadhi ya magazeti ya Kiswahili yaliyopigwa marufuku kuregelea uchapishaji, na Rais Samia Suluhu Hassan amewasamehe wafungwa wengi wa dhamiri, wakiwemo wanachama wa Chadema.

c- Kuhusu suala la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, licha ya ukweli kwamba IMF ilifukuzwa Tanzania enzi za Rais Hassan Mwinyi, kwa sababu ilitaka kumwekea masharti kama vile kushusha thamani ya sarafu, kupandisha bei na kufungia mishahara, ambayo huongeza mateso ya watu, kama IMF inavyofanya katika kila nchi inayoomba mkopo. Hata hivyo, IMF ilichukua fursa ya athari za janga la virusi vya Korona kutoa mkopo kwa Tanzania wenye thamani ya dolari milioni 567, ikisema kuwa "mkurupuko wa virusi vya Korona ulisababisha kuporomoka kwa sekta ya utalii na kuzidisha haja ya ufadhili mkubwa." (Bloomberg 8/9/2021), hivyo serikali ya Tanzania ilikubali kuchukua mkopo huo, huku ikijua kuwa Tanzania haiutambui mkurupuko huo wa Korona na haikuweka hatua za kuzuia, lakini ilikubali kuboresha uhusiano na IMF na sio kugongana na Amerika, sambamba na mtazamo wa Uingereza inayoifuata!

d- La muhimu zaidi ni kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo ilianzishwa mnamo tarehe 17/8/1992 badala ya Kongamano la Uratibu wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, iliyoanzishwa nchini Botswana mnamo tarehe 1/4/1980 kutoka nchi wanachama tisa (Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Msumbiji na Eswatini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe) na sasa ni 15 baada ya kujiunga Afrika Kusini, Namibia, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Madagascar, na Ushelisheli na ilianzishwa na Uingereza ili kudumisha ushawishi wake katika eneo hilo, na kuzuia kuingilia katika kwa ushawishi wa Marekani katika nchi za kikundi hilo. Hivyo basi, pindi kampuni ya mafuta ya Marekani, Anadarko, ilipogundua hifadhi kubwa ya gesi asilia iliyoko katika Bonde la Rovuma, lililoko karibu na pwani ya mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji mwaka 2010, ambako Waislamu wanaishi nchini humo.

Kisha hifadhi hii ilithibitishwa mnamo mwaka wa 2017, kwa mujibu wa makala yaliyochapishwa na Financial Times mwaka 2017. "Gesi iligunduliwa katika vitaru viwili vya karibu, na kila moja yao kimethibitisha hifadhi ya futi za ujazo trilioni 75, ambayo ni ya kutosha - kulingana na wataalamu - kuisambazia Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia kwa zaidi ya miaka 20." Kwa hivyo, gesi ilipogunduliwa na kuthibitishwa mnamo 2017, Uingereza iligundua tabia ya Amerika ya kuingilia Msumbiji, haswa kwamba hii iliambatana na vuguvugu la uasi katika nchi hii lililozidi kuongozwa na kikundi cha ndani kiitwacho Ansar al-Sunna wal Jama'a, na kisha Rwanda, ambayo ina uhusiano na Amerika, ilijitolea kuisaidia Msumbiji dhidi ya (uasi) na kuijaribu kwa hili, Msumbiji ilikubali... Manmo tarehe 9/7/2021, Rwanda ilipeleka kikosi cha wanajeshi 1,000 kwa ombi la Msumbiji kusaidia kuzima waasi wa muda mrefu wa Kiislamu katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado... Ingawa Rwanda inashirikiana na Amerika, Msumbiji ilipendelea kuomba msaada kutoka Rwanda!

Saba: Uingereza ilipoona hili, ililisukuma kundi la SADC kurekebisha hali ya Msumbiji, ambayo ni mwanachama wake:

1- Viongozi wa SADC wakati wa mkutano walizipongeza nchi wanachama kwa kujitolea kwao kupeleka Kikosi cha Kudumu cha SADC na kutoa msaada wa kifedha katika Mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, kwa ajili ya kutumwa nchini humo. (https://africa.sis.gov.eg 21/8/2021)

2- Pindi Rwanda mfuasi wa Marekani ilipopeleka wanajeshi 1,000 kaskazini mwa Msumbiji, ambayo si mwanachama wa SADC, idadi kadhaa ya wanachama wa SADC walipinga: ["Kutumwa kwa vikosi vya Rwanda kuliwakasirisha baadhi ya wanachama wa SADC, kwa kuwa ushiriki wa Rwanda hauko chini ya udhibiti wa SADC..." Walisema kwamba hoja ya uhalalisha ya Rwanda ambayo si mwanachama wa SADC, kwa msaada wa Msumbiji, ni kuhalalisha "kichocheo cha maafa" (https://www.defense-network.com 22/7/ 2021)].

Hivyo Uingereza, kwa kutambua majaribio ya Amerika kuingilia kati kupitia msaada wa Rwanda kwa Msumbiji, ilipotambua hilo mara moja ilituma msaada wa kijeshi kwa Msumbiji kupitia shirika lake la SADC ili Rwanda isibaki peke yake huko.

3- Kulingana na ripoti ya tovuti ya Bloomberg, [Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alisema katika mkutano wa Kundi la nchi saba zilizoendelea kiviwanda: “Nilipata fursa ya kukutana na Ufaransa, Muungano wa Ulaya na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na kuwaeleza kuwa maoni yetu ni kwamba Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika inapaswa kuongoza katika suala hili” (https://www.bloomberg.com/news/newsletters/13/8/2021)].

4- Hivi majuzi, kundi hilo lilifanya mkutano mnamo tarehe 18/1/2022 nchini Malawi kusaidia ujenzi wa kiuchumi na kijamii wa Cabo Delgado, ambayo ina utajiri mkubwa wa gesi asilia nchini Msumbiji, yenye wakaazi wapatao milioni 30, na idadi ya Waislamu karibu 20%. Kiasi cha gesi ndani ya mkoa huu inakadiriwa kuwa mita za ujazo trilioni 75. Mkutano huo uliidhinisha uungwaji mkono wa Msumbiji na hatua za kuimarisha amani, usalama na ufufuaji wa kijamii na kiuchumi katika mkoa huu ambako vuguvugu la kisilaha linafanya kazi. Kundi hilo liliapa kuendelea kupambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali nchini Msumbiji. Rais Lazarus wa Malawi, ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya SADC, alisema: ["Kujitolea kwa kundi hili ni kuhakikisha kuwa eneo la Cabo Delgado nchini Msumbiji linaendelea kuwa sawa, shwari na salama, na kwamba mkutano huu unatoa fursa ya kupitia kuhakiki misheni ya SADC nchini Msumbiji katika mapambano dhidi ya ugaidi." (SPA 18/1/2022)].

Nane: Kuhusu juhudi za China, hadi sasa imetawaliwa na ushawishi wa kiuchumi zaidi kuliko kufikia ushawishi wa kisiasa, na kuridhiana nayo kiuchumi ni kuiudhi Marekani. Kwa kuzingatia jambo hili inabainika kuwa Tanzania inajitahidi kuimarisha mahusiano yake ya kiuchumi na China ili kuokoa hali ya kiuchumi na hata kuepukana na utawala wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa juu yake, yaani utawala wa Marekani juu yake, yote ni kwa maelekezo ya Uingereza. Kwa sababu hii, Tanzania ilitia saini mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi na China ili kufadhili miradi ya China nchini Tanzania. Kuna mazungumzo ya kufadhili miradi yenye thamani ya mabilioni ya dolari, ima ni kujenga bandari mpya kwa thamani ya dolari bilioni 10, au kujenga kituo cha gesi iliyoyeyuka chenye thamani ya dolari bilioni 30, na mradi wa mgodi wa chuma na makaa ya mawe wenye thamani ya dolari bilioni 3.

Katika mazungumzo ya simu kati ya Xi Ping na Samia Hassan mnamo tarehe 22/6/2021, Xi alisema, "China iko tayari kutekeleza mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kwa kuzingatia mikakati ya maendeleo ya Tanzania na kupanua ushirikiano katika maeneo kama kilimo, uchukuzi, mawasiliano, utalii na nishati,” Samia Hassan alisema, “Tanzania iko tayari kushirikiana na China kuendeleza kikamilifu ujenzi wa pamoja wa Ukanda na Barabara, na itatekeleza kwa dhati matokeo ya Mkutano wa Beijing wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika, na kukuza maendeleo mapya ya uhusiano kati ya China na Afrika. (Uchina CGTN 22/6/2021)

Tisa: Kutokana na hili inaeleweka kwamba Uingereza bado inadhibiti kundi la SADC, kwani maamuzi yanafanywa kwa upendeleo wa kuimarisha ushawishi wa Uingereza kwa kuunga mkono tawala zake tanzu. Kutokana na hayo, inaweza kusemwa kwamba Uingereza inaidhibiti Tanzania na vile vile SADC, na kwamba majaribio ya Marekani ya kupenya ndani ya Msumbiji yanasitasita kati ya mafanikio na kushindwa, na hayana utulivu hadi sasa.

Kwa sababu hizi, Tanzania na Msumbiji ni wagombezi wa mzozo wa kimataifa, yaani baina ya Uingereza, ambayo ina ushawishi katika SADC na wanachama wake, na Amerika, ambayo ina nia ya kupanua ushawishi wake mahali pa Uingereza, hasa Msumbiji. Nchi hizi za Kiafrika zitaokolewa tu kutokana na migogoro yake na makucha ya ukoloni kupitia utawala wa Uislamu ambao ni rehma kwa walimwengu wote.

 [وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ]

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote” [Al-Anbiya: 107]

1 Ramadan 1443 H

2/4/2022 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu