Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watawala wa Banu Saud, ni Walaji Njama wa Mwanzo na wa Mwisho!
(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika makala ya gazeti la New York Times, yenye kichwa, "Utawala wa Biden Washiriki Jaribio la Muda Mrefu kwa Makubaliano ya Saudi-'Israel’" inaripotiwa kuwa, "Rais na wasaidizi wake wanasisitiza juhudi za kidiplomasia huku Riyadh ikitoa matakwa makubwa kwa badali ya uhalalishaji mahusiano, pamoja na makubaliano ya nyuklia na makubaliano thabiti ya usalama ya Marekani.”

Makala hayo yaliongeza, "Kwa upande wake, Mwanamfalme Mohammed anatafuta kuimarishwa kwa uhusiano wa usalama na Marekani, ufikiaji wa silaha zaidi za Marekani na ridhaa ya Marekani kwa ufalme huo kurutubisha uranium kama sehemu ya mpango wa nyuklia wa kiraia - jambo ambalo Washington imepinga kwa muda mrefu.”

Iliripoti pia, kwamba Martin Indyk, balozi wa zamani wa Marekani katika umbile la Kiyahudi alisema, "Biden ameamua kuyafuata makubaliano hayo, na kila mtu katika utawala sasa anaelewa kuwa rais anataka hili... Unapozungumzia amani ya Mashariki ya Kati, ni jukumu la pande zote tatu."

Maoni:

Bani Saud na familia ya al-Sheikh huko Hijaz kwanza walishirikiana na nyoka Uingereza kupindua Dola ya Khilafah na kulazimisha kutawaliwa na ukoloni wa Waingereza katika Bara Arabia, ash-Sham na Iraq. Kisha wakala njama, wakiwaongoza watawala wote wa Kiarabu, kuunda na kuliimarisha umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu, Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.

Usaliti wao haukuishia hapo. Walifanya kazi na watawala wengine wa Kiarabu, vibaraka wa wakoloni, kuunda Shirika la Ukombozi wa Palestina (PLO). PLO ilitia saini rasmi Makubaliano ya Oslo ya 1993, kwa jina la watu wa Palestina, kuwapa Mayahudi mamlaka juu ya Ardhi Iliyobarikiwa. Wakati wa mwendo huo wa khiyana, watawala wa Kiarabu, wakiwemo watawala wa nchi zinazoitwa Ua la Waarabu (دول الطوق العربي) walijitwika jukumu la kulilinda umbile dhaifu la Kiyahudi kutokana na Ummah, ikiwemo harakati yoyote inayotaka kwa dhati kuikomboa ardhi hiyo, kutoka ndani na nje ya Palestina.

Watawala  wa Kiarabu waliharakisha kuhalalisha uhusiano na umbile la Kiyahudi, kwa amri na maelekezo ya Marekani na Uingereza. Hakuna hata mmoja wao aliyejizuia kutokana na uhalalishaji mahusiano hayo, isipokuwa kwa muonekano wa nje. Dola ya Al-Saud ni lango pana la Ulimwengu wa Kiislamu, kupitia kwalo Mayahudi wanaweza kuzifikia nchi nyenginezo za Ulimwengu wa Kiislamu, ili waweze kuhalilisha mahusiano na Ulimwengu wa Kiislamu, na kuchochea ufisadi ndani yake.

Kupitia uhalalishaji huu wa mahusiano, Marekani ilitaka kulazimisha kwa Mayahudi suluhisho la mwisho lililowakilishwa na mpango unaouita "suluhisho la dola mbili." Inatafuta kutumia suala la uhalalishaji mahusiano na Saudi Arabia kama nukta ya maridhiano na umbile la Kiyahudi, na serikali yake ya kiburi, ambayo inajiona kama mtoto wa kiongozi wa genge aliyeharibiwa.

Mahitaji "ya kupitiliza" ya bin Salman mzembe sio matakwa makubwa, kwa kweli. Badala yake, hayazingatiwi kuwa ni matakwa hata kidogo. Si chochote ila ni kurusha vumbi machoni, huku yakitengeneza njia kwa ajili ya tangazo la uhaini wa uhalalishaji mahusiano na Mayahudi.

Kwa hivyo ni usalama gani anaozungumzia Bin Salman? Ni Tishio gani? Kutoka kwa nani? Je, kwani silaha zote za hali ya juu za ufalme wake hazitoki Marekani, ikiwa zimetolewa kweli na sasa ziko katika milki kamili?! Ni ipi haja ya serikali yake mbovu, fisadi, iliyoanzishwa kwenye ardhi tohara ya Hijaz, kwa ajili ya uranium na urutubishaji wake?! Je munamuona akitaka kutengeneza silaha za nyuklia? Silaha hizi zitatumika dhidi ya nani? Dhidi ya adui hadaifu wa Iran, ambaye hivi karibuni alijenga upya uhusiano? Au dhidi ya dola ya Kiyahudi ambayo anataka kuitangaza kutangaza uhalalishaji mahusiano nayo, na ambayo kwa ajili yake atamtelekeza kila Muislamu katika ardhi ya Hijaz, kama alivyowatelekeza watu wa Palestina?

Imesemwa, إن التذاكي على الأذكياء ضربٌ من الغباء kwamba “Kucheza na wenye akili ni aina fulani ya upumbavu.” Hii ndiyo hali Ibn Salman.

​Kushitadi matukio katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na kuongezeka kwa jinai za Mayahudi na kumwaga kwao damu tukufu, kunapaswa kutoa hamasa kwa majeshi ya Kiislamu huko Hijaz, Pakistan, Misri, Bangladesh, Uturuki na kwengineko. Inapaswa kuwa motisha kwao kuwapindua watawala hawa wasaliti, huku wakisimamisha tena Dola ya Khilafah kwa Njia ya Utume kwenye magofu yao. Hakika Khilafah ndio dola itakayonyanyua majeshi kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na najisi ya Mayahudi.

Itafanya hivyo kwa kuitikia amri ya Mwenyezi Mungu (swt)

[انفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” [Surah At-Tawba 9:41].

Itafanya hivyo, kwa kuthibitisha kauli ya Mtume (saw), «تُقَاتِلُكُمُ اليَهُودُ فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ، ثُمَّ يَقُولُ الحَجَرُ يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ وَرَائِي، فَاقْتُلْهُ» “Mpigana na Mayahudi na mtawashinda, kisha jiwe litasema ewe Muislamu huyu hapa Yahudi nyuma yangu; basi njoo umuuwe!’” [Bukhari] Ni lazima fursa kwa watawala wa Bani Saud, pamoja na walaji njama wengine, kutumia matukio yanayotokea katika Ardhi Iliyobarikiwa kutangaza uhalalishaji wao mahusiano na Mayahudi, kwa kisingizio cha kusimamisha umwagaji damu, lazima izuiliwe.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bilal Al-Muhajir – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu