Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Makosa Mawili Hayafanyi jambo kuwa Sawa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Rais Recep Tayyip Erdoğan, kuhusiana na sera za kiuchumi zilizojadiliwa baada ya kauli ya Waziri wa Hazina na Fedha Mehmet Şimşek "Tutarudi kwenye msingi wa busara", alisema, "Tulikubali kwamba Waziri wetu wa Hazina na Fedha anachukua hatua zake na Benki Kuu haraka na kirahisi. Tulitangaza dhamira yetu ya kupunguza mfumko wa bei hadi tarakimu moja. Unajua tulipopunguza (mfumko wa bei) hadi tarakimu moja wakati wa uwaziri mkuu wangu, riba ilikuwa 4.6 na mfumko wa bei 6.2. Tulifanya mambo haya pamoja wakati huo na tumesema  vivyo hivyo kwa Bw. Waziri sasa inabidi tufanye kwa pamoja kwa namna hiyohiyo. Tulifanya kazi kwa nadharia ya ‘riba ya chini, mfumko wa bei wa chini’ wakati huo. Nafanya kazi kwa uelewa huo huo sasa, nina wazo hilo hilo na ninaamini kwamba tunaweza kufikia hili kwa njia hii." (Mashirika 15.06.2023)

Maoni:

Maadamu pembetatu ovu za mfumo wa uchumi wa kibepari - benki, kiwango cha riba, soko la hisa - zinafuatwa, matokeo yayo hayo ni yakini kutokea. Je, matokeo haya ni yapi? Mfumko wa bei, yaani, gharama ya maisha, kuanguka kwa uwezo wa ununuzi. Migogoro imekuwa ndio maumbile ya mfumo wa kibepari. Kipote cha mabepari wachache wanazidi kutajirika kila siku huku watu wakizidi kuwa masikini. Tunaweza pia kuuita huu mkono wa matajiri usioiachi kamwe mifuko ya watu. Riba inaweza kuonekana kama ufukarishaji na unyonyaji jamii. Haya ndio madhara yasiyoepukika ya utabikishwaji mfumo wa uchumi wa kibepari.

"Mafanikio" ya sera za kiuchumi za Rais Erdoğan wakati wa uwaziri mkuu wake, ambayo anayazungumzia sana, kwa kweli ndio sababu ya migogoro ya leo. Ima yeye hajui ukweli huu, au anaufunika ingawa anaujua. Kiasi kilicholipwa kwa riba katika miaka 11 ya uwaziri mkuu wake kilikuwa dolari bilioni 389. Hususan kuhusiana na miaka iliyosemwa sana; Mnamo 2008, kwa mfano, kiasi kilicholipwa kwa riba kilifikia dolari bilioni 40. Mnamo 2022, pamoja na viwango vya riba vya Amana Inayolindwa ya Sarafu (KKM), bili ya riba inayolemezwa watu ni dolari bilioni 24.4. Maadamu hupingi riba lakini unapinga riba kubwa, hakuna kitakachobadilika. Ulisema kuna ‘Nas’, lakini hata hukutilia maana ‘Nas’ kuhusu mada hiyo. Ulizitumia tu hisia za watu kwa msingi wa imani yao. Leo, utajaribu kurekebisha uchumi kwa kuongeza kiwango cha juu cha riba ukitumia mkono wa Mehmet Şimşek, uliyemteua tena kuwa Waziri wa Fedha. Wewe, ambaye ulifanya makosa makubwa zaidi huko nyuma kwa kutoa mamia ya mabilioni ya dolari kwa magenge ya kimataifa kwa sura ya riba, unasisitiza juu ya kosa baada ya kosa kwa kuendelea na ufahamu ule ule leo. Ingawa unajua kuwa makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sawa.

Kwa kuwa ustawi na amani ya watu haiwezekani kwa mfumo fisadi, wokovu hautawezekana kwa kufuata njia ya makosa. Kiwango cha riba ambacho umewafanya watu hawa walipe wakati wa utawala wako kimezidi dolari bilioni 600. Wananchi hawajalipia tu gharama ya mfumo katili wa kibepari ulioutabikisha kiuchumi. Pia wamelazimika kulipia gharama kubwa katika masuala ya kijamii, kisiasa, kijeshi, imani, akhlaqi na maadili. Achana na makosa yaliyojaribiwa, maovu yanayojulikana, masuluhisho ambayo hayatasaidia, na mfumo wa Kibepari unaofisidi jamii. Unaweza kumaliza vurugu hizi, dhulma hii, ulaghai na ufisadi huu kwa kurudi kwenye Mfumo safi wa Kiislamu. Umefika mwisho wa uhai wako na mwisho wa utawala wako. Kama vile hapo awali, tunaendelea kukwambia ukweli, ingawa unauzibia masikio. Kwa matumaini kwamba utauepuka batili hii.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu