Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Minyororo ya Taratibu za Biashara Huria katika Mipaka ya Ardhi za Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mapema Oktoba, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtakatifu Burhanuddin alitembelea mkoa wa Visiwa vya Riau, ambao ni eneo la mpakani nchini Indonesia. Aliomba kwamba upande wa mashtaka kwa kesi za Ulanguzi wa Dawa za Kulevya na Binadamu katika Visiwa vya Riau utoe athari ya kuzuia wahalifu katika eneo la Visiwa vya Riau (Kepri). Alitaka vifungu viweze kuongezwa. Haya yaliwasilishwa na Mtakatifu Burhanuddin wakati wa ziara yake ya kikazi katika Visiwa vya Riau mnamo 7 Oktoba. Burhanuddin anataka hatua za kisheria zichukuliwe kuhusiana na kuibuka kwa uhalifu wa kimataifa, kama vile uvuvi haramu, ulanguzi wa binadamu, magendo ya bidhaa na mihadarati, hadi masuala ya mahuruji na maduhuli.

Wakati huohuo Septemba iliyopita, iliripotiwa kuwa Polisi wa Riau (bara) pamoja na Polisi wa Dumai walifanikiwa kukamata magenge 16 yanayoshukiwa kuwa na zaidi ya kilo 203 ya dawa za kulevya aina ya crystal methamphetamine na tembe 404,491 za ecstasy zilizo chukuliwa ndani ya siku 4 tu (11-14 Septemba 2022). Haya ndiyo mafanikio makubwa zaidi yaliyofikiwa na Polisi wa Riau katika kufichua visa vya dawa za kulevya.

Maoni:

Idadi ya kesi za uhalifu wa dawa za kulevya, magendo na ulanguzi wa binadamu katika maeneo ya mpakani mwa Indonesia inaonyesha udhaifu wa ulinzi wa mpaka katika nchi hiyo kubwa zaidi ya Kiislamu. Ongezeko la wahusika na makundi ya uhalifu katika maeneo ya mipakani ni kiashirio cha udhaifu wa ulinzi wa serikali katika maeneo ya mpaka wa nje, ambapo pwani ya mashariki ya Sumatra iko katika hatari kubwa ya kukabiliwa na msururu wa biashara ya dawa za kulevya kutoka eneo la Indo-China huku silsila yake ya usambazaji ikitoka Mto Mekong hadi Mkondo wa Malacca. Bila kusahau kuwepo kwa mashirika ya ulanguzi kutoka Cambodia na Vietnam.

Uwepo wa mafia wa chinichini wa madawa ya kulevya na makundi ya magendo ya ulanguzi wa binadamu - pia unanufaika kutokana na kuanzishwa kwa FTZ (Eneo Huria la Biashara kwenye Visiwa vya Batam, Bintan na Karimun), ambayo inahitaji uingizaji wa bidhaa zinazotoka nje bila kutozwa ushuru na hata zile zisizo halali katika ardhi ya Indonesia, pamoja na topografia ya visiwa ambayo inaruhusu bandari nyingi za panya kwa magendo. Haya yote yalianza kwa jina la uwekezaji na biashara tangu 2006, Indonesia na Singapore zina makubaliano ya pamoja ya FTZ huko Batam, Bintan na Karimun, ambapo Singapore - nchi isiyo ya Kiislamu inajulikana kama mshirika wa karibu wa Marekani na umbile la Kiyahudi. na ni shupavu sana katika kutekeleza uvamizi wa kiuchumi na utamaduni kwa eneo jirani.

Kutarajia athari za kuzuia uhalifu mwingi kwenye mpaka ni sawa na kuufyatulia risasi mwezi, ikiwa nchi haina ruwaza na mtazamo thabiti na sahihi katika kulinda mipaka yake kutokana na kujisalimisha kwake kwa mifumo ya biashara ya WTO na GATTS na udhaifu wa msimamo wake wa kujadiliana dhidi ya nchi za makafiri. Athari ya kuzuia hakika haitoshi kupitia hatua za chini za kutibu kupitia vikwazo vya kiutawala tu, lakini hatua za kimkakati zinahitajika pia kutoka juu, yaani, utumiaji wa siasa sahihi za biashara ya Kiislamu na sera ya kigeni ya Kiislamu ambayo itaboresha nafasi ya mazungumzo ya Indonesia machoni pa nchi za kigeni.

[لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِي الْبِلَادِ مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمِهَادُ]

“Kabisa kusikudanganye kubakia kutangatanga kwa walio kufuru katika nchi. Hiyo ni starehe ndogo. Kisha makaazi yao yatakuwa Jahannamu. Na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia.” [Al-i Imran 196-197].

Hali ya hivi leo inazidishwa na mgawanyiko mkubwa zaidi wa Ummah kupitia fikra ya utaifa na mfumo wa dola ya kitaifa. Picha ya jinsi Sharia ya Kiislamu inavyosimamia mipaka kiuchumi na kiulinzi inafifia. Thaqafa kuhusu mipaka na ardhi ya Ribat imemomonyoka. Kwa kawaida, hali ya kijografia ya Ummah iko katika kilele chake cha chini kabisa katika historia ya hadhara ya Kiislamu. Uislamu una sheria maalum kuhusu maeneo ya mipakani na jinsi sifa za kibinadamu zinapaswa kuyalinda.

Mtazamo wa Kiislamu ni tofauti sana na Magharibi katika suala la kuweka mipaka ya dola. Ubwana wa nchi hautegemei tu eneo la nchi, bali unatokana na utekelezaji sheria na dhamana za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya usalama wa nchi, matokeo yake, mijadala ya kimaeneo inakuwa yenye nguvu na kunyumbulika sana; hata inasemekana kwamba damu ya Mujahid ndiyo inayo amua mipaka ya ardhi za Kiislamu.

Tunahitaji dola inayo tabanni dira imara ya mpaka na mtazamo inayotokana na Uislamu pekee, na inaweza tu kutekelezwa na Khilafah - dola iliyo kwa mujibu wa mwongozo wa Kiislamu na manhaj (njia ya utume). Kwa njia hiyo, Khilafah itawaweka watu wake bora zaidi kwenye mipaka kwa sababu Uislamu pia unataka sifa bora zaidi kwa walinzi wa mipaka watakaoweza kukabiliana na kumtia hofu adui, kwa sababu maeneo ya mpakani ni maeneo yenye msuguano na nje ambayo hufanya kazi kama msingi wa kueneza hadhara pindi inapokuwa kwenye kilele cha nguvu na vivuko kwa askari wa adui wanapokuwa dhaifu. Uislamu unataka sifa bora za kibinadamu kwa imani yao, utambuzi wa nafasi, ukali wa macho ya mwewe ambaye yuko kwenye ulinzi mpakani.

[يَا أَيُّهَا الَّذِيْنَ آمَنُوا اصْبِرُوْا وَصَابِرُوْا وَرَابِطُوْا وَاتَّقُوا اللّٰهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُوْنَ]

“Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.” [Al-i Imran: 200]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu