Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Taifa Imara huzaliwa kutokana na Fikra Imara

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ajenda katika Jumba la Rais, Rais Erdoğan alisema, “Mataifa imara yanajumuisha familia imara. Kama sharti la hadhara yetu ya zamani, sisi ni taifa linaloundwa kutokana na familia imara. Sio mahali pa mtu yeyote kuharibu muundo wa familia ya taifa hili. Tutalinda muundo wa familia yetu dhidi ya kila aina ya upotovu.” (Haber7, 03/11/2022)

Maoni:

Nguvu kubwa zaidi ya taifa ni mfumo wake. Nguvu ya kiroho (kimfumo) ina nguvu zaidi kuliko nguvu za kimada. Ni fikra (nguvu ya kiroho) ya familia ndiyo inayo pelekea maendeleo au kuporomoka kwa familia. Leo, nchini Uturuki, mbali na baadhi ya fikra na hisia, mawazo yanayotawala familia au watu binafsi ni imani na mifumo ya kirasilimali ambayo ni kinyume na maumbile ya mwanadamu na haikujengwa juu ya akili. Kwa mujibu wa hili, mataifa imara na familia imara huzaliwa kutokana na fikra wanazoziamini. Ikiwa mawazo na fikra zinazotawala familia ni fikra na hisia za kirasilimali, kama ilivyo Uturuki na nchi nyingine nyingi za Kiislamu leo, taifa lenye imara haliwezi kupatikana. Ushahidi bora wa hili ni hali ya watu na dola katika nchi za Kiislamu.

Tumesema mataifa imara hayawezi kupatikana kwa fikra za kibepari. Hapa, swali linaweza kuja akilini; Naam, je, watu wa Marekani na Magharibi au mataifa yanayoamini mfumo wa urasilimali si taifa au dola yenye nguvu? Nguvu ya nchi hizi haitokani na mifumo wanayoiamini, bali kutokana na nguvu ya kimada waliyo nayo. Kwa sababu mifumo yao imepitwa na wakati, mawazo yao yameoza, na tabia zao ni potovu. Mawazo na tabia hizo dhaifu, potovu, mbovu haziwezi kuzalisha mataifa yenye nguvu. Muundo na hali ya watu dhaifu na familia zilizosambaratika barani Ulaya na Amerika ni uthibitisho bora wa hili. Kwa hiyo, nguvu ya Marekani na Ulaya haitokamani na uimara wa miundo ya familia zao au utimamu na usahihi wa mifumo yao, bali kutokana na nguvu ya kimada walio nayo na kukosekana kwa mataifa yenye nguvu dhidi yao. Ambapo kuna madhaifu, wale ambao ni madhaifu kimuundo lakini kwa kiasi fulani huibuka kuwa mataifa yenye nguvu. Nguvu ya Marekani na Ulaya leo hii inatokana na ukweli kwamba hawana Ummah (Dola) wenye nguvu dhidi yao.

Ingawa Erdogan anahusika, alidai kuwa baadhi ya makundi yaliyopotoka yamevuruga muundo wa familia ya taifa la Uturuki. Huu ni mfano wa kulaumu mtu mwingine wakati wa kutapatapa na kufilisika. Au kuwalaumu wengine ili kuficha hatia yako mwenyewe. Ikibidi kumtafuta mhalifu na mtu anayehusika, ni muhimu kuwatafuta wale ambao kwa kujua wanazitawala familia na watu binafsi kwa fikra na mifumo iliyooza, fisadi na kinyume na imani zao. Kwa kifupi, sio vikundi potovu kama vile LGBT, lakini mfumo unawaruhusu kuchipuza kama uyoga kwa jina la uhuru, na mtawala ambaye kwa hiari anatabikisha mfumo huu uliopitwa na wakati unaovunjia heshima muundo wa familia wa taifa la Uturuki. Kwa sababu ikiwa kuna uasherati, uovu, ufisadi, taabu, njaa, ukosefu wa ajira, umaskini, nk katika nchi, tabia yoyote na jambo lolote lisilofaa ustawi wa binadamu na maisha ya heshima, Erdogan anawajibika. Kwa sababu kila kiongozi anawajibika kwa raia wake.

«فَالإِمَام رَاعٍ وهو مَسْؤولٌ عن رَعِيَّتِهِ»

“Imam ni mchungaji na yenye ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake.”

Kama mtu anayewajibika kwa raia wake, Erdoğan hawezi kulinda muundo wa familia yetu kwa fikra ya ubepari, ambao huangamiza, kusambaratisha, kubomoka na kutawanya muundo wa familia yetu. Mtu hajaponywi kwa sumu, kinyume chake, anakufa. Kwa fikra za kibepari zenye sumu na watawala wenye sumu wanaotabikisha fikra hizi za sumu, muundo wa familia yetu hauwezi kuhifadhiwa, kinyume chake, itatiwa sumu. Kuona mara kwa mara mauaji na maangamivu ya familia kwenye habari ni dalili na uthibitisho wa hili. Zimwi la familia huzaliwa tu kutoka kwa fikra za kizimwi. Erdogan anapaswa kuelewa hili vizuri na ikiwa anataka kulinda familia, atabikishe mfumo wa Kiislamu itakaolinda familia. Chochote chengine ni kejeli.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu