Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Pindi Waokozi wanapofanywa kuwa Wahanga

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kiongozi wa BSP Imran Masood alisema mnamo Jumamosi katika tweet iliyotumwa kwa Kihindi, "Dola inageuka kuwa isiyo salama kwa mabinti chini ya utawala wa CM Yogi Adityanath. Huko Meerut, mwanafunzi wa BDS Vania Shaikh alijiua kwa kuruka kutoka kwenye mtaro, mwanafunzi mwenzake alimnyanyasa kimapenzi hadharani na kumpiga kofi kwa kupinga hilo.” (Free Press Journal)

Maoni:

Ripoti zinaonyesha kuwa Waislamu milioni 200 wa India wanakabiliwa na vitisho vilivyopangwa na vilivyolengwa, kushambuliwa, unyanyasaji wa kingono na mauaji. Tukio hili la hivi majuzi la kuhuzunisha la Vania Shaikh, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sayansi ya meno ambaye alikabiliwa na dhulma na udhalilishaji na kuyakatiza maisha yake hadharani. Kitendo chake hakikuwa tu cha kukata tamaa, hasira na kukosa matumaini, bali kilikuwa ni tangazo la wazi la hali duni ya Waislamu nchini India. Alama za mikwaruzo ya kucha zilizopatikana kwenye uso wa mtuhumiwa zinaweza kuonekana kwenye nyuso za watu wenye nguvu ambao wangeweza kumlinda. Kwa Serikali za Pakistan na India zinaweza kuwa majirani tu lakini kwa watu wa Pakistan, Waislamu wa India ni kaka na dada zao waliowaacha nyuma.

Pakistan ni natija ya matakwa ya watu kuishi chini ya Uislamu. Maisha yaliyopotea, yaliyotolewa kafara na kunyakuliwa yalikubaliwa kwa nyoyo nzito. Familia ziligawanywa, mali kupotea, mabinti kushambuliwa na madonda ndugu yalipatikana kwa raia. Sote tumesikia hadithi za kutisha za wanawake kuruka juu ya mapaa ya nyumba zao au kwenye visima ili kuokoa heshima yao. Watoto waliuawa mbele ya macho ya mama zao. Wanaume walikufa wakiwalinda wanawake na watoto na walidhani wanalinda vizazi vya Waislamu. Lakini hata baada ya mistari kuchorwa, ubaguzi uliendelea. Waislamu kila walipopatikana katika mazingira magumu walisakwa. Kwa hakika, ilipanuka na kuwa vuguvugu la kimataifa la kuwalaumu Waislamu kwa kila kosa, hata kwa wao kuwa Waislamu.

Hili linaweka wazi kuwa vita si dhidi ya Waislamu bali imani yao. Wanapodai kuwa Waislamu ni tishio kwao, kwa hakika wanatoa maneno kutokana na hofu yao ya kina ya nguvu ya Uislamu. Vania hakuwa msichana wa kwanza kuteseka na hatakuwa wa mwisho ikiwa tutaendelea kuishi chini ya mfumo huu wa kishetani. Mwandishi wa habari wa India Dhirendra K Jha alisema, "Ikiwa Hindu Rashtra inamaanisha kupeana hadhi ya daraja la pili kwa Waislamu, basi India tayari kivitendo imekuwa mojawapo. Sasa ni swali kuhusu kuifanya rasmi. Hata kama hawatafanya hivyo, mabadiliko yameshafanyika”

Kwa hakika, ndoto ya BJP ni kupunguza uwepo wa Waislamu nchini India, na hawakukwepa kuieleza vilevile. Hawa ni Waislamu walewale waliopigana sambamba na kuwafukuza Waingereza kutoka Bara dogo na ambao wameishi nao pamoja kwa mamia ya miaka. Harakati ilianza kwa ajili ya uhuru bila ya kuwa na mpango wowote wa na nchi ya kando kwa sababu Waislamu walichukulia Bara zima kama nyumbani kwao. Wazo hili la kujitenga lilianzishwa na kukuzwa na Waingereza ili kuwa na udhibiti mzuri zaidi juu ya watu, na kuwafanya wahasimu wao kwa wao itafanya iwe rahisi kwa Waingereza kuwa na udhibiti juu ya wote wawili.

Tukiangalia tu wanawake wa Kiislamu waliofanya kazi ya uhuru wa Bara dogo wakati wanaume walipokuwa wamefungwa, tutakuta wengi ambao walifanya kazi ya kuwaondoa Waingereza. Abadi Bano Begum aliyeitwa na Gandhi kama Bi Amma, licha ya hali yake mbaya ya kifedha, kuanzia 1917-1921, alichangia Rupia 10 kila mwezi kupinga Sheria ya Ulinzi ya Uingereza, baada ya kukamatwa kwa Sarojini Naidu. Bibi Amtus Salaam alifanya kazi na Gandhi na mnamo Februari 9, 1947, ripoti ilitokea kwenye ‘The Tribune’ ikieleza kufunga saumu kwake kwa siku 25 kwa ajili ya kupinga kama uingiliaji kati mashuhuri zaidi. Begum Hazrat Mahal, mke wa Nawab Wajid Ali Shah, mtawala wa Awadh, alikataa kukubali fadhila zozote au posho kutoka kwa Waingereza. Begum, kwa msaada wa kamanda wake Raja Jailal Singh, aliipiga vita kwa ushujaa Kampuni ya British East India. Muhammadi Khanum, pamoja na ufahamu wake wa fasihi alionyesha uharibifu wa Kampuni ya East India wa misikiti na mahekalu ili kutoa nafasi kwa barabara kuu, ambazo zilitumika kama kichocheo cha uasi huo. Syeda FakrulHajiyan Hassan alishiriki katika vita vya uhuru wa India na kuwataka watoto wake kufanya hivyo pia. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto wa wahamiaji wa Iraq na aliwalea wanawe wa kiume kuwa wapiganiaji uhuru ambao baadaye walipata sifa mbaya kama "Ndugu wa Hyderabad Hassan."                     

Hii ni mifano michache tu ya wanawake wajasiri wa Kiislamu na dori yao dhidi ya uvamizi wa Waingereza. Je, tunawezaje kukubali udhalilifu na ukatili huu dhidi ya mabinti wa wanawake hawa wa ajabu na je tunawezaje kuwaacha wateseke peke yao? Je, miaka hii 75 ya utaifa imetufanyia nini? Kutoka kwa kupigana na wanaume na wanawake wanaoandamana tumegeuka kuwa mashini za kuchuma na kutumia pesa. Urasilimali umetugeuza kuwa viumbe wenye mwelekeo wa faida na umezifunga shughuli zetu kwa mafanikio ya kibinafsi, maendeleo na burudani. Tunaweza kujisikiaje tunapowaona binti zetu kama Vania? Kwa nini tusifuate nyayo za mama zetu na kufanyia kazi jambo ambalo kweli ni muhimu? Tunatoa wito kwa ndugu zetu wenye nguvu na silaha wainuke na kujithibitisha kuwa wao ni Waislamu wa kweli wanapoishi tu kwa ajili ya kutii maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Taabu yoyote wanayokumbana nayo katika njia hii hatimaye itawapeleka kwenye Jannah ambayo ni ndoto ya kila Muislamu. Kwa kusimamisha Khilafah pekee ndiko kutakako tatua matatizo ya Umma wa Kiislamu.

Hadi wakati huo tuna machaguo mawili, kuteseka na kusubiri mateso zaidi, au kupambana na tuwe watu wanaopendwa na Mwenyezi Mungu (swt). Kuchelewa na kuzembea kwa Waislamu wenye nguvu kusaidia kutasababisha hasara zaidi kwa Ummah huu na watahisabiwa na Mwenyezi Mungu (swt).

Imesimuliwa kutoka kwa Abdullah bin Umar kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ، وَمَنْ كَانَ فِي حَاجَةِ أَخِيهِ كَانَ اللَّهُ فِي حَاجَتِهِ، وَمَنْ فَرَّجَ عَنْ مُسْلِمٍ كُرْبَةً فَرَّجَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرُبَاتِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِمًا سَتَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ»‏

“Muislamu ni ndugu yake Muislamu, hamdhulumu, wala hamsalimishi kwa dhalimu. Na anayemtimizia nduguye haja zake, Mwenyezi Mungu atamtimizia haja zake; anayemtoa ndugu yake (Muislamu) kutokana na usumbufu, Mwenyezi Mungu atamtoa katika masumbuko ya Siku ya Kiyama, na mwenye kumsitiri Muislamu mwenzake, Mwenyezi Mungu atamsitiri Siku ya Kiyama.” (Sahih al-Bukhari)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu