Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Sheria ya Kupambana na Upotoshaji wa Habari

(Imetafsiriwa)

Habari:

Sheria ya Kupambana na Upotoshaji wa Habari, pia inaitwa Sheria ya Mitandao ya Kijamii, imepitishwa na Bunge Kuu la Uturuki na kuanza kutekelezwa. Kwa mujibu wa sheria hii, mtu yeyote anayesambaza hadharani taarifa zisizo za kweli kuhusu usalama wa ndani na nje, utangamano wa umma na afya kwa jumla ya nchi kwa njia inayozua wasiwasi, hofu au kuogopa miongoni mwa umma kwenye mitandao ya kijamii kwa njia inayoleta usumbufu kwa amani ya umma ataadhibiwa kwa kifungo kuanzia cha mwaka 1 hadi miaka 3. Endapo mhalifu atafanya uhalifu kwa kuficha kitambulisho chake cha kweli au ndani ya mfumo wa shughuli za shirika, adhabu itaongezeka kwa nusu.

Maoni:

Inawezekana kuzingatia sheria hii, Sheria ya Kupambana na Upotoshaji wa Habari/Sheria ya Mitandao ya Kijamii, katika vipengele kadhaa:

1- Kwa sheria hii, serikali inalenga kudhibiti na kuweka kikomo kwa upashanaji wa habari na taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazoweza kujenga rai jumla dhidi ya serikali na kusababisha kupungua kwa uungaji mkono wa wananchi kwa serikali kabla ya uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi Juni 2023.

Ikiwa serikali ilitaka kweli kuwalinda watu wake kutokana na athari mbaya za mitandao ya kijamii kwa sheria hii, ingekataza ushiriki unaofanywa kwenye mitandao ya kijamii kwa maudhui machafu, yenye maudhui ya ngono na ambayo yanaeneza LGBT na kusababisha ufisadi wa kijamii na kimaadili.

Au ingekataza magazeti, majarida, habari, musalsalati, sinema katika vyombo vya habari vya kuona na maandishi vinavyosifu/kuhimiza ngono, LGBT, uchafu, udanganyifu, usaliti, ghasia, umafia, pombe na dawa za kulevya, dhulma, utamaduni wa kigeni, mtindo wa maisha na maadili yanayosababisha ufisadi wa kijamii na kimaadili.

Kwa hivyo, wakati wa kutunga sheria hii, serikali ilichukua ulinzi wa mamlaka yake yenyewe kama msingi, badala ya watu wake.

2- Fahamu kuu ya sheria hii ni fahamu ya habari zinazopotosha/upotoshaji wa habari. Haijabainishwa katika sheria hii kipi cha kukichukua kama msingi wa habari zinazopotosha. Sheria ya wazi au iliyoko wazi kutoa maoni imeshatungwa.

Je, suala la upotoshaji wa habari, ambalo linaweza kutofautiana kulingana na mtazamo, litaamuliwa vipi. Au itabainikaje iwapo taarifa/habari fulani inahusu usalama wa nchi, inavuruga utulivu/amani ya umma, ikiwa inaleta hofu, wasiwasi miongoni mwa wananchi.

Tashwishi hii imeachwa kwa uamuzi wa mahakama. Ikiwa habari au taarifa ya kweli iko dhidi ya serikali, inawezekana kwa hakimu kuichukulia kama habari ya kupotosha. Serikali imeigeuza sheria hii kuwa upanga mkali kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii unaokata pande zote mbili.

Hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaharamisha uwongo na kueneza habari na taarifa za uwongo. Wakati huohuo, hata mbele ya mtawala dhalimu, Aliamuru, akasifu na kutukuza kusema ukweli.

3- Kilicho muhimu ni kubaini kwa usahihi chanzo kinachozalisha uhalifu na kuzuia uhalifu kwa kuharibu chanzo hiki. Kwenda kwenye adhabu ya wahalifu tu bila kuharibu chanzo cha uhalifu hakutazuia uhalifu, lakini kinyume chake, itasababisha kuongezeka kwa viwango vya uhalifu.

Pindi machapisho ya mitandao ya kijamii yakichunguzwa, inaonekana jinsi watu wetu walivyo katika mporomoko mkubwa, uchakavu, uduni, ufisadi, muozo, na kutokuwa na thamani.

Hali hii imesababishwa na Jamhuri ya Uturuki ambayo imekuwa madarakani na kuwatawala wananchi kwa miaka 99 na ambayo imejengwa juu ya msingi wa mfumo wa kibepari na maadili yake msingi kama vile uhuru, usekula, demokrasia na uchumi wa soko huria.                                                                                                                                                 

Ufahamu wa siku hizi wa siasa, unaopuuza utaratibu halisi wa uharibifu wa jinai kwa kuwalaumu/kuwaadhibu watu katika matatizo na maovu yote yanayoletwa na mfumo fisadi/haribifu wa kirasilimali, pia ni mshiriki katika mfumo huu haribifu.

Kwa sababu hizi, suluhisho sahihi ni kusahihisha kwa sheria kile ambacho kimevunjwa na sheria. Ni Mfumo wa Uislamu pekee, ambao umeegemezwa juu ya Sheria za Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndio unaoweza kuwasahihisha watu wetu, waliofisidishwa na kuharibiwa na mfumo wa Kirasilimali – utabikishaji wa sheria za Kikafiri – na kuwaendeleza na kuwainua tena kwenye hadhi ya Ummah mashuhuri na bora.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Özer

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu