Jumanne, 24 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Uhakiki wa Habari 02/04/2022

Putin Atafuta Kutoka Ukraine lakini Asisitiza juu ya Kusimama Kidete

Vita vinaenda vibaya kwa Putin. Rais wa Urusi amejenga uongozi wake juu ya wazo la ukubwa wa Urusi ilhali udhaifu wa kibinafsi unamlazimisha kujaribu kuuthibitisha kwa kila fursa. Amerika ilitumia majigambo ya awali ya kujivuna kwa Putin ili kumchochea kuivamia Ukraine, na Amerika inatumia haja ya Putin kuonekana kama mshindi ili kumfanya aendeleze vita ambavyo ni wazi haviwezekani kwa Urusi kushinda. Badala ya Ukraine kuporomoka kwa haraka, Urusi imekwama ndani ya matope ya Ukraine na sasa imepunguza malengo yake hadi kuchukua sehemu ndogo ya mashariki mwa Ukraine pekee. Kulingana na Washington Post:

Wakati Urusi ilipoanzisha vita vyake nchini Ukraine mnamo Februari, Rais wa Urusi Vladmir Putin pengine alitarajia vita vya haraka na ushindi wa haraka. Badala yake, sasa tuko katika mwezi wa pili wa mapambano makali na ya kikatili. Maelfu ya raia takriban wameuawa (ingawa hakuna hesabu ya kihakika), miji ya Ukraine imesagwasagwa, na Waukraine milioni 4 wamemiminika Ulaya, na kusababisha mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi katika bara hilo tangu Vita vya pili vya Dunia. Urusi pia imepata hasara kubwa, huku wanajeshi wake wapatao 40,000 wakiuawa, kukamatwa au kujeruhiwa na angalau majenerali saba wa Urusi kuuawa na vikosi vya Ukraine - hata ingawa miji mingi mikubwa ya Ukraine imesalia chini ya udhibiti wa Kyiv. Katika kile kilichoonekana kama juhudi za kuokoa uso wake, maafisa wa jeshi la Urusi walitangaza hivi karibuni kwamba watabadilisha mkakati wa kuzingatia upya juu ya "kulikomboa" eneo la mashariki la Donbas.

Wakati huo huo, Urusi iko kwenye mazungumzo na Ukraine jijini Istanbul. Rais wa Ukraine Zelenskyy alionyesha maendeleo katika hotuba yake ya video mnamo siku ya Jumanne, wakati akijitolea kuendeleza juhudi za vita, "Tunaweza kusema kwamba ishara tunazosikia kutoka kwa mazungumzo ni chanya, lakini ishara hizo hazizimi milipuko wala makombora ya Urusi." Viongozi wa Magharibi vile vile walikataa kushawishiwa na dalili za kubadilika kwa Urusi. Rais wa Marekani Joe Biden alisema, "Tutajua wanachofanya, lakini, kwa sasa, tutaweka vikwazo vikali... Tutaendelea kuwapa wanajeshi wa Ukraine uwezo wa kujilinda wenyewe, na tutaendelea kufuatilia kwa karibu kile kinachoendelea.” Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, alisema, "Kuna kile Urusi inachosema na kile ambacho Urusi hufanya ... Tunazingatia cha pili, na kile ambacho Urusi imekuwa ikifanya ni ukatili kwa Ukraine na watu wake." Gazeti la Washington Post liliripoti, ‘Afisa mkuu wa Pentagon anayesimamia wanajeshi wa Marekani barani Ulaya, Jenerali Tod D. Wolters, alisema wakati wa kikao cha Kamati ya Seneti ya Huduma za Silaha Jumanne kwamba anaweza kuthibitisha ripoti za vikosi vya Urusi kujiondoa katika eneo karibu na Kyiv. Lakini katika mkutano na waandishi wa habari baadaye siku hiyo, Kirby aliashiria Urusi ilikuwa ikifanya mabadiliko, sio "kujiondoa halisi." Kulingana na The Guardian, 'Msemaji wa Boris Johnson, waziri mkuu wa Uingereza, alisema Uingereza imeona ishara za "kupunguzwa kidogo" kwa shambulizi la Urusi karibu na Kyiv, lakini akaongeza: "Tutamhukumu Putin na serikali yake kwa vitendo vyake, sio kwa maneno yake ... Hatutaki kuona chochote chengine isipokuwa kujiondoa kamili kwa vikosi vya Urusi kutoka eneo la Ukraine.”'

Ni umbile la mfumo wa Kirasilimali wa kiliberali wa kisekula wa Kimagharibi kutathmini mafanikio ya sera ya kigeni kwa kuzingatia manufaa ya kimada pekee, bila kujali gharama ya kibinadamu. Hii ni kwa sababu Wamagharibi wenye mtazamo wa uwezekano wa uhalisia huitazama imani ya kidini kuwa ya kubahatisha, na hivyo kutenganisha dini na mambo ya maisha, badala yake wakiegemeza maamuzi yao maishani juu ya mahesabu ya kimada ya kidunia pekee, kwani ulimwengu wa kimada ndio kitu pekee wanachoweza kukubali kwa yakini kuwa ni hakika. Kuiingiza Urusi katika vita nchini Ukraine, licha ya makumi ya maelfu ya maisha kupotea kila upande, ni ushindi kwa nchi za Magharibi. Hii ni kinyume na Uislamu, ambao uliotawala mambo ya dunia kwa zaidi ya miaka elfu moja na kuasisi mtazamo uliojengwa juu ya maadili wa sera ya kigeni ambayo umekuja kuathiri namna dola zote duniani zinavyojiendesha kimataifa. Mabaki ya mtazamo huu uliojengwa juu ya maadili yapo katika matamshi matupu ya sera ya kigeni ya Magharibi lakini kwa kiasi kikubwa yamekosekana katika utekelezaji halisi wa Magharibi. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utasimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) itakayounganisha ardhi zote za Kiislamu, kukomboa maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu, kutabikisha sharia ya Kiislamu, kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kubeba ulinganizi wa Uislamu kwa ulimwengu mzima. Dola ya Khilafah, kuanzia siku ya kusimamishwa kwake, itajiunga na safu za dola kuu kwa sababu ya ukubwa wa saizi yake, idadi kubwa ya raia, rasilimali nyingi, siasa za kijiografia zisizo na kifani na mfumo wa kipekee wa Kiislamu. Dola ya Khilafah itakabiliana, kuzidhibiti na kuzituliza dola nyingine kubwa na kuregesha dunia katika amani na ustawi jumla uliokuwepo kabla ya kuibuka kwa Magharibi mbeberu kafiri

Imran Khan wa Pakistan Apatiliza Mgogoro wa Ukraine Kubakia Hai Kisiasa

Mnamo tarehe 24 Februari 2022, siku ambayo Urusi iliivamia Ukraine, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan alikuwa jijini Moscow kwa ziara iliyopangwa kwa muda mrefu kukutana na Putin, akitarajia kupata mafanikio ya sera ya kigeni kwa kufanya ziara rasmi ya kwanza ya kiserikali kwa raisi wa Pakistan katika miongo miwili. Mwanasiasa aliyekomaa angepata njia ya kupanga upya ziara hiyo, kwani mzozo wa Ukraine wakati huo ulikuwa tayari umekola moto. Mnamo tarehe 21 Februari, Urusi ilikuwa imetambua rasmi Donetsk na Luhansk, ndani ya Ukraine, kama vyombo huru na kuamuru vikosi vya Urusi "kudumisha amani" huko. Marekani, kwa kujibu, ilikuwa tayari imetangaza vikwazo vya awali kwa Urusi. Hata hivyo, Imran Khan, akiwa na hamu ya kupata mafanikio nje ya nchi ili kusaidia nafasi yake iliyodhoofika nyumbani, badala yake alisonga mbele na ziara hiyo kama ilivyopangwa, akionyesha Pakistan kama isiyoegemea upande wowote katika mzozo kati ya Urusi na Magharibi. Sasa, akikabiliwa na mvutano wa kutokuwa na imani naye nyumbani unaotishia kumuondoa madarakani, Imran Khan anadai kuwa ni Amerika ndio inayounga mkono upinzani wa Pakistan kwa sababu ya sera yake ya kigeni dhidi ya Marekani.

Kwa hakika, Imran Khan ameunga mkono kikamilifu malengo ya sera ya nje ya Marekani ya muda mrefu kwa Pakistan. Amerika kwa jumla haina shida na vibaraka wake kuungana na Urusi au China, na kwa kweli inaona hili kama chanzo chenye manufaa cha uwezo wa kujiinua juu ya dola hizo kuzitumia wakati wowote Amerika inaotaka. Chini ya Imran Khan, Pakistan imeendeleza kikamilifu sera yake ya kutogombana na serikali ya India ya BJP ambayo pia inafuata maagizo ya Amerika. Waziri Mkuu wa India Modi aliweza kuchukua hatua za kurekebisha hali ya Kashmir ndani ya katiba ya India bila kuogopa mzozo wowote na Pakistan juu ya suala hilo. Vile vile, ilikuwa chini ya Imran Khan ambapo Pakistan ilishinikiza sehemu ya uongozi wa Taliban kufanya mazungumzo na Amerika kupitia afisi yao ya Doha.

Kwa kweli, Imran Khan ni kibaraka wa maslahi ya kigeni kama vile walivyo viongozi wake wa upinzani bungeni. Siasa za Pakistan zinasimamiwa na jeshi kwa niaba ya mabeberu makafiri wa Marekani. Haijalishi sana kwa Amerika nani anakuwa Waziri Mkuu. Hakika, ilikuwa ni kwa uungwaji mkono mkubwa wa jeshi la Pakistan uliowezesha PTI ya Imran Khan kuingia madarakani, chama kilichokusanywa vilivyo na jeshi lenyewe kwa kushinikiza wanachama wa vyama vingine kujiunga nacho. Ikiwa jeshi limeondoa uungaji mkono kutoka kwa Imran Khan, sio kwa sababu ameikasirisha Amerika lakini kwa sababu ameliudhi jeshi kuhusiana na mambo ya ndani.

Wakati huo huo, jeshi kwa mara nyingine tena limeashiria utiifu wake kamili kwa maslahi ya Marekani. Kulingana na Bloomberg, 'Pakistan inatafuta kupanua uhusiano wake na Marekani na China, mkuu wa jeshi lenye nguvu la nchi hiyo alisema, siku mbili baada ya Waziri Mkuu Imran Khan kuushutumu utawala wa Biden kwa kupanga kuipindua serikali yake madarakani kwa kuunga mkono kura ya kutokuwa na imani naye Bungeni.' Mkuu wa Jeshi, Jenerali Qamar Javed Bajwa alisema katika hotuba yake mnamo Jumamosi, "Tuna historia ya uhusiano wa muda mrefu na bora wa kimkakati na Marekani, ambayo inasalia kuwa soko letu kubwa zaidi la kuuza nje." Pia alisema, "Pakistan inafurahia uhusiano wa karibu wa kimkakati na China unaoonyeshwa na kujitolea kwetu kwa Ukanda wa Kiuchumi wa Pakistan. Tunataka kupanua uhusiano wetu na nchi zote mbili bila kuathiri uhusiano wetu na wengine."

Umma wa Kiislamu unaendelea kutawaliwa na tabaka la vibaraka wa kisiasa ambalo utiifu wake uko kwa mabeberu makafiri wa Magharibi. Lakini kwa idhini ya Mwenyezi Mungu wakati umekaribia kwamba tabaka hili lote litapinduliwa na Waislamu watatoa ahadi ya utiifu wao kwa Khalifa muongofu ambaye atatabikisha Uislamu na kusimamiwa na kuhesabiwa na Ummah kwa msingi huu pekee.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu